Kufanya kazi vijijini nilikuwa nasikiaga tu kwa jirani

Kufanya kazi vijijini nilikuwa nasikiaga tu kwa jirani

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
238
Reaction score
954
Yamenikuta natamani kulia, nimepata ajira somewhere jamani chumba ni wadudu tu mda wote hata raha hamna masisimizi kibao hadi kitandani, kipindi cha mvua kinaanza chumba kinavuja, majongoo yanaingiaga ndani unaweza sema Niko nje network hakuna ni baadhi tu ya maeneo network inakamata.

Ajira ajira za vijijini ni mateso hapa ninavyoongea umeme hamna nimebakiwa na asilimia 5% umeme umekata tangu SAA 5 Asubuhi.

Nilikuwa nasikia tu ajira za vijijini sasa najionea kwa macho huduma za kijamii chache mateso!!! mateso!!! Saluni zao za kunyoa sasa ha ha ha jamani jamani mchwa wametawala chumba cha kinyozi hakuna capeti ni vumbi mlangoni limewekwa pazia tu unaweza sema uko mgahawani.
 
Yamenikuta natamani kulia, nimepata ajira somewhere jamani chumba ni wadudu tu mda wote hata raha hamna masisimizi kibao hadi kitandani,kipindi cha mvua kinaanza chumba kinavuja,majongoo yanaingiaga ndani unaweza sema Niko nje ajira ajira za vijijini ni mateso hapa ninavyoongea umeme hamna nimebakiwa na asilimia 5% umeme umekata tangu SAA 5 Asubuhi.nilikuwa nasikia tu ajira za vijijini sasa najionea kwa macho huduma za kijamii chache mateso!!! mateso!!! Saluni zao za kunyoa sasa ha ha ha jamani jamani mchwa wametawala chumba cha kinyozi hakuna capeti ni vumbi mlangoni limewekwa pazia tu unaweza sema uko mgahawani.
Pole Sana Mkuu inaonekana hali sio nzuri

Jaribu kutafuta Sehemu nzuri ambayo haivuji then kabla ya kuhamia piga dawa Farmigation weka kapeti zingatia na usafi hasa kuchemsha maji ya kunywa na kuwa na vyombo visafi.
 
Yamenikuta natamani kulia, nimepata ajira somewhere jamani chumba ni wadudu tu mda wote hata raha hamna masisimizi kibao hadi kitandani, kipindi cha mvua kinaanza chumba kinavuja, majongoo yanaingiaga ndani unaweza sema Niko nje.

Ajira ajira za vijijini ni mateso hapa ninavyoongea umeme hamna nimebakiwa na asilimia 5% umeme umekata tangu SAA 5 Asubuhi.

Nilikuwa nasikia tu ajira za vijijini sasa najionea kwa macho huduma za kijamii chache mateso!!! mateso!!! Saluni zao za kunyoa sasa ha ha ha jamani jamani mchwa wametawala chumba cha kinyozi hakuna capeti ni vumbi mlangoni limewekwa pazia tu unaweza sema uko mgahawani.
Na mkikutana kilabuni maongezi yenu ni...... "Kuku Wangu Ameanza Kutaga Mayai"
 
Kuna zahanati ipo simiyu..ina manesi wawili tu...kila daktari akipangiwa kule anakimbia....
Umeme upo
Network hakuna yakutafta tafta
Wananchi wanaanzia kwa waganga kwanza alafu zahanati
Maji ya bwawani
Kijijini pasikie tu kwa mwenzio..kijana ukienda uko hutoboi
 
Tanzania tunasikitisha sana vijijini.

Kuna kijiji nilienda maji yana rangi ya juisi ya ukwaju na wazawa wanakunywa bila hofu.

Guest niliofikia wanauliza kabisa kama utaoga asubuhi au jioni maana unapata ndoo moja tu kwa kila kutwa moja ya makazi.
 
Back
Top Bottom