Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Utakufa kwanza wewe mchumiatumbo na kuiacha CHADEMA. Chama sio viongozi wala wabunge chama ni wanachama
 
Hakuna chama kitakuja kukishinda CCM as long as polisi wako upande wao.
Wananchi option yetu sasa ni msaada wa wazungu hakuna namna, na kwa hili nawaunga mkono Lissu & Zitto kwa 110%.
Wazungu watakupa msaada gani mkuu, jana tu ulifurahia EU kuijadili Tanzania 🇹🇿 leo wabunge wa chama kinachopinga uchaguzi kimepeleka timu uwanjani.Nguvu ya wazungu itatoka wapi?? Wazungu wenu waambieni wajue hii ni Tanzania 🇹🇿 na watanzania wako nyuma ya viongozi wao.
 
Sitaki kusikia tena hiki chama.

Kuanzia leo

1.Sitakuwa na chama.
2.Sipigi kura, mpaka ipatikane katiba mpya na tume huru.

CHADEMA mmenipa hasira isiyomithilika.
 
Hivi kuna mtu anaamini Mnyika na Mbowe hawajui haya?

Yani Mdee afanye vitu kama hivi bila baraka za Mbowe?

Anachofanya Mnyika ni kuwa confuse wafuasi wao wasijue washike lipi lakini ukweli ni kwamba kila kitu kina baraka za Mbowe na Mnyika
 

Mkuu leo ndio rasmi CHADEMA imegeuka kuwa NCCR, tutabaki wapinzani wa kweli bila kutegemea chama chochote cha siasa.
 
Hivi kuna mtu anaamini Mnyika na Mbowe hawajui haya?

Yani Mdee afanye vitu kama hivi bila baraka za Mbowe?

Anachofanya Mnyika ni kuwa confuse wafuasi wao wasijue washike lipi lakini ukweli ni kwamba kila kitu kina baraka za Mbowe na Mnyika

Kwa taarifa yako Mbowe na Mnyika wanajua kila kitu, na hata kulegea kwao walianza toka walipoenda kutaka muafaka. Toka wakati ule nilijua rasmi Mbowe na genge lake hawana jipya, imani pekee tuliyokuwa nayo ilikuwa ni kwa Tundu Lisu. Hata kujitokeza kupiga kura ilikuwa ni kwakuwa Lisu karudi. Kama sio ujio wa Lisu tusingejitokeza kupiga kura. Uzuri tunaweza kufanya upinzani bila kutegemea chama chochote cha siasa.
 
Sisi ni wapinzani na tutaendelea kuwa wapinzani bila kutegemea chama chochote, cdm tuliwaunga mkono maana waliwakilisha mitazamo yetu. Ila kwakuwa wameamua kushirikiana na shetani, basi wasitegemee tena support yetu.
 
CHADEMA haiwezi kufa sababu ya usaliti wa wajinga wachache

Mkuu hata NCCR haijafa, lakini mvuto haina tena. Rasmi cdm imeingia kwenye kundi hilo. Tutapambana na ccm bila kutegemea Chama chochote cha siasa. Chama kisicho na msimamo hakina nafasi kwetu.
 
Niliwahi kuipenda ile CHADEMA ya Dkt. Slaa, yule ndiye alikuwa katibu mkuu mwenye maono.

Nyakati zake CHADEMA ilikuwa ni ya mipango, mikakati na yenye ushawishi kwa vijana, wasomi na ilibeba uhalisia wa jina lake.

Baada ya kumsaliti Dr.Slaa 2015 CHADEMA ilijifia, walipoteza ushawishi tena kwa wanachama wake. Hasa baada ya Lowassa kurudi CCM.

Sasa hivi CHADEMA kimekua chama cha kuombea Tanzania na wananchi wengi ambao hata siasa hawazishabikii iangukie kwenye matatizo ya uchumi, diplomasia. Yaani ni kupinga kila kitu kwa sababu tu ya mtazamo wa JPM.
 
Peleka umbea huu CCM
 
Unaboa sana siku hizi,umekuwa kama simbilisi hajulikani yupo kindi gani kama ni panya au sungura.
 
Kuwa kichaa sio lazima uvue nguo . Wewe unawashauri Chadema umeombwa na nani huo ushauri uchwara wako . Mpaka Chadema kinafika hapa kilipo miaka 28 wewe ushauri wako ndio ulikifikisha hapa? . Kifupi tunafukuza wote walindwe na Ndugai lakini legacy ya chama lazima ilindwe . Pole kwa magaidi kusmua kutumia akaunti yako ili kukuvunjia heshima yako , di ndio mlivyokubaliana kule ulikoitwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…