Wanabodi,
Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, maana nimenote baadhi ya viongozi, wanachama, wafuasi wamepigwa na butwaa kwa uamuzi wa wanawake mashoka wa Chadema, kukataa ujinga and did the right thing.
Kitendo cha Chadema kususa kupeleka majina ya wabunge wa viti maalum, ni kufanya kosa, ila kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa, hili kosa la Chadema is a death mistakes hivyo Chadema is almost dead, due to that death mistakes!, uamuzi wa kina Halima Mdes ndio the only hope for survival ya Chadema, wakiwatimua, huku kutakuwa ni kurudia kosa, it's do or die kwa Chadema, warudie kosa wafe, au wakubali matokeo, waendelee kuishi, the choice is yours!.
Kuna wanasiasa wako kwenye siasa, na wametafuta uongozi wa siasa kwa kusaka madaraka tuu, uongozi as a means of livelihoods, lakini kiukweli siasa hawaziwezi, hawazijui wala hawajui uongozi wa umma sio utumishi wa chama ni utumishi wa watu.
Wanabodi, JF ni ukumbi huru wa kuhabarishana, kuelimishana, kuburudishana, na kitu kikubwa zaidi, kusaidiana. Kama kuna kitu unakijua, na unaona kinafanyika ndivyo sivyo, unajitolea kusaidia, na hiki ndicho ninachofanya hapa, kwa kuendelea na zile makala zangu elimishi kuhusu Maslahi ya Taifa...
www.jamiiforums.com
Kwenye bandiko hili, nilieleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya Tanzania, vyama vya siasa sio mali ya viongozi, sio mali ya wanachama, ni mali ya umma, hivyo maamuzi yoyote ya chama lazima yatangulize mbele maslahi ya umma.
Vyama vya siasa kama vilivyo vyama vya wafanyakazi, vina uhuru wa kugoma, kufanya maandamano na hata kususia jambo lolote, ili mradi kugomea huko au kususa huku, kwa kususa huko kuna something tangible they will achieve. Kususa tuu ili mradi kususa bila ku achieve anything nilikuita ni ujinga.
Leo, nimefarijika sana kusoma haya
Naunga mkono hoja, Hongera sana Mhe. Halima Mdee kwa kukataa ujinga na badala yake kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii, KM wa Chadema, JJ.MNYIKA amesema chama kama chama hakija poleka majina.
Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, najua mtaitisha kikao cha Kamati Kuu ya dharura kulijadili hili, nawashauri, msipoteze muda wala msithubutu kuwatimua as waasi, kwasababu hapo ilipo tuu Chadema is almost dead!, ikiwatimua ndio mwisho wa Chadema!. Kwa vile hawa ni the minority, hata mkiwafuta uanachama, Spika atawalinda as the minority ila pia Watanzania wote wenye akili timamu, hawatawaelewa!, this will be a very sad ending for what was used to be Chadema.
Hapo ilipo tayari Chadema is severely and deeply wounded, uchaguzi huu umewaacha with very big injuries, kitendo walichokifanya wanawake hawa wa Shoka kwa kuongozwa na Halima Mdee, its like adding an insult to an injury, Chadema ikiwatimua, nayo will die instantly, waliotimuliwa ndio watasikika, waliowatimua wenzao, ndio wataishia 6ft under!.
Kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Kususa kupeleka majina ni kosa, mimi niliuita ni ujinga!. Kina Halima Mdee wameukataa ujinga huu, kuwatimua ni kurudia kosa!.
Chadema msifanye death mistakes!.
Paskali