Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Bro nakujibu wewe kama mwana CCM Na sio kama mwandishi wa habari.

1. Kama ningekua na uwezo ningewatimua uanachama hao wanawake kwa kughushi nyaraka. Kwa sheria Na taratibu wanastahili kushtakiwa na kufugwa.

2. Kama lengo ni kuiua CHADEMA kitakufa ila wafuasi wake hamtawapata. Ningekua Mwenyekiti Wa chama ningeshauri tuvunje chama ili mkose mpira Wa kuchezea.

3. Ni ninii sababu ya CCM kung'ang'ania wapinzani waingie bungeni? Si mlitaka mafiga matatu? Kwa nini tena ghafla mwawataka? Acheni chama kife. Nyie sio wanachama wala wapenzi wala wapinzani wetu lakini mwataka tuendelee kuwepo why?. Let people decide their own path. It will better suit everyone.

I hope you will let it die a natural death. Then may be you can celebrate the victory!!
 
Yaani na wewe Pascal unataka tukwambie ujifunze kuandika!

Jifunze matumizi sahihi ya adjectives na nouns! Nimeona humu mara nyingi tu unaandika hata adjectives tatu zinafatana kwenye sentensi moja!

Sasa hii 'death mistakes'ndio nini sasa. Kwanini usiseme deadly mistakes or fatal mistakes!
Halafu sensationalism yote hii ya nini? Mbona sioni kosa la hao Chadema.
 
Wee Paskali unawaonea huruma wa nini CHADEMA ? hao viumbe wakati wa kampeni walikuwa na kidomodomo sana ,vitisho ,mbwembwe,jeuri kwenye mitandao na majukwaa wakiamini muda wote kuwa wao ndio washindi.

Walijazwa ujinga mwingi ukawaingia.Na wallahi,wanajifanya haki za binaadam lakini wangeshinda tungeokota vichwa vya watu mabarabarani.Halafu eti unawaonea huruma .Hebu na wewe usituudhi na huruma zako,wacha KIFE.
 
Sawa Pasco tabiri zako nyingi huwa zinatimia ila sijui CHADEMA walikufanyiaga nini kiasi ukajiapia hawataingia rahani
Tabiri ipi?
Alisema Lissu hawezi rudi Tz

Alidai zitto atakua KUB

Alidai upinzani umekufa na kampeni zitakosa watu.

Acheni kumpa sifa asizostahili, yye huwa anafanya probability ya obvious things. Kma ana uwezo wa kuona mbali ilikuaje aliambulia kura 1 huko Kawe?

Pascal Mayalla is overrated, PERIOD
 
Pascal, hili la viti maalum ilikuwa leverage kwa CHADEMA, ndio maana CCM wakawa wanahaha kila saa hadi kuja na ngonjera kuwa kuna mfumo dume.

CHADEMA kuwa ndani ya bunge sasahivi wanaeffect ndogo kuliko ambavyo wangeendelea kutokuwepo.

For survival ni heri CHADEMA wasiwepo ndani ya bunge ila wakabaki na leverage waliokuwa nayo. Through leverage many things can be accomplished, cause mtu ukiwa na leverage juu ya mtu, hiyo ni silaha.
Wewe ndio umetoa hoja ya kisomi mkuu. Nimekuelewa sana
 
Ka Mayalla kaliambulia kura 1 pale Kawe, hakapendwi na wananchi wa Kawe! Kwetu Mayalla ni njaa (in Mh. Mungu's voice)!
 
Kaka yangu Pasco naona andiko lako limeegemea kwenye mlengo wa kiitikadi zaidi.
Nionavyo mimi, kilichofanyika kina maslahi makubwa kwa upande wa waliofacilitate ilo litokee ambao ukitaka kuwajua unganisha dot za jinsi Mh. aliyetoka gerezani alivyotoka toka na zile kauli za muapishaji na si maslahi ya taifa.

Nakubaliana na ww ni kwa maslahi ya taifa wabunge wa viti maalum toka CDM waingie bungeni, lakini kuingia kwao kungetokana na maridhiano ya pande zote kungekuwa na afya kwa umoja na amani ya nchi yetu. Ingawa lengo linaweza kuwa jema lakini njia iliyotumika inaweza kuwa limeongeza nyufa katika taifa letu ambazo tusipofikiria kuziziba kwa kiburi cha hawa watatufanya nini, sisi tuna kila kitu, kinaweza kutupelekea kujenga ukuta huko tunapoelekea. Nakuhakikishia kuna wengi hawapendi hiki kinachoendelea lakini hawana la kufanya wanabaki na maumivu yao ndani kwa ndani.
 
Hivi Bado hujapata uteuzi tu ukitulizee
Pasco,hawezi pata teuzi yoyote kwani Magufuli kaamua kuwapa Unaibu Waziri akina Mdee na wenzake...

Nasikia Ijumaa Baraza jipya la Mawaziri litatangazwa na ndani yake watakuwemo akina Halima Mdee...

Cjajua Magufuli atatumia Kanuni ipi kuwateua wadada hao, ngoja tusubiri tuone kwani "lisemwalo lipo".
 
Wanasiasa hawana future nje ya siasa. Kazi yao ni kupiga debe...kutumbua mali na kufanya starehe, huku wakishindwa ishauri Serikali ifanyeje kuajiri mamilioni ya wapiga kura huko mtaani.

Tizama sasa wanavyoumbuka. Waende wakajiajiri tuone.

Nyamafu.
 
Anaesema anajua siasa alishindwa kupenya kura za maoni CCM; sasa unaweza kutoa ushauri gani kwa Chadema wakati kuwashawishi wajumbe wa Kawe -ccm ulishindwa?

Watanzania tuna vituko sana.
 
Ninafikiri siasa ni mahesabu. Ukikosea unapotea kwenye ulingo wa siasa.CHADEMA watch out! Safari hii by all standards you may perish miserably in the history of mult party politics. Pelekeni viti maalum msionekane waasi wa katiba na utawala bora kwenye macho ya wananchi.
Huijui history ya cdm??
 
Anaesema anajua siasa alishindwa kupenya kura za maoni CCM; sasa unaweza kutoa ushauri gani kwa Chadema wakati kuwashawishi wajumbe wa Kawe -ccm ulishindwa?

Watanzania tuna vituko sana.
Si kushindwa tu, bali aliambulia kura moja tu, dadeki.
 
Tabiri ipi?
Alisema Lissu hawezi rudi Tz

Alidai zitto atakua KUB

Alidai upinzani umekufa na kampeni zitakosa watu.

Acheni kumpa sifa asizostahili, yye huwa anafanya probability ya obvious things. Kma ana uwezo wa kuona mbali ilikuaje aliambulia kura 1 huko Kawe?

Pascal Mayalla is overrated, PERIOD
Ila wajumbe wa ccm si watu kabisa, yani kabisaa mtu kama Paskal watu wanapiga spana anaambulia kura moja?
 
Hii ni stage III ya the communist Party of China "The art of political war", kuna stages 10, stage ya III tuu, Tuna chemka.

Stage III inasema :

a) Unatakiwa katika any political contest mshindani wako umpige sana achakae na adhalilike , na umwache hajitambui na hata kuomba msaada ashindwe kwa kuwa hajui anahitaji nini na afanye nini.

( you have to strike hard and once to eliminate you leave him for dead, the impact must be beyond self examination )

b) Hata ikitokea amejikusanya kurudisha shambulizi, mashambulizi yake hayo yawe hafifu mno kiasi hayawezi kuwa na madhara na bila kulenga.

c) Lazima umwachie makovu makubwa (in his body politics and leadership) ambayo akitaka kuyatibu haraka basi makovu hayo yatamuuwa.

Na muda si mrefu stage IV inakuja na tunaweza tusibaki salama.

Stage IV naweka akiba nitaishusha muda muaafaka.

Wanateremsha scripts tuu, wanaroho mbaya sana CCM.
 
2624063_IMG-20201125-WA0019.jpg
 
Hapo ilipo tayari Chadema is severely and deeply wounded, uchaguzi huu umewaacha with very big injuries, kitendo walichokifanya wanawake hawa wa Shoka kwa kuongozwa na Halima Mdee, its like adding an insult to an injury, Chadema ikiwatimua, nayo will die instantly, waliotimuliwa ndio watasikika, waliowatimua wenzao, ndio wataishia 6ft under!.

Kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Kususa kupeleka majina ni kosa, mimi niliuita ni ujinga!. Kina Halima Mdee wameukataa ujinga huu, kuwatimua ni kurudia kosa!.
Chadema msifanye death mistakes!.

Paskali

Pascal Mayalla
sijuhi huw aunatumia nini kufikiri,
Embu tujiulize hawa ndio wakwanza kufukuzwa?
je walipofukuzwa hiko chama kiliishia wapi?
Hivi ushafikiria 2025 hawa wanawake washoka wataweka sura zao wapi wakienda kuomba kura?
Je kwasasa wataishi wapi kw ausaliti walioufanya?
Nasikia wanlindwa! Je ulizi wa nini sasa na hawa ni chaguo la wananchi ?
 
Mheshimiwa,

Nimeiba sehemu ya bandiko Lako na kulibandika Kwenye ukurasa wangu wa Uzalendo wa Kitanzania.

Wanabodi,

Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, maana nimenote baadhi ya viongozi, wanachama, wafuasi wamepigwa na butwaa kwa uamuzi wa wanawake mashoka wa Chadema, kukataa ujinga and did the right thing.

Kitendo cha Chadema kususa kupeleka majina ya wabunge wa viti maalum, ni kufanya kosa, ila kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa, hili kosa la Chadema is a death mistakes hivyo Chadema is almost dead, due to that death mistakes!, uamuzi wa kina Halima Mdes ndio the only hope for survival ya Chadema, wakiwatimua, huku kutakuwa ni kurudia kosa, it's do or die kwa Chadema, warudie kosa wafe, au wakubali matokeo, waendelee kuishi, the choice is yours!.

Kuna wanasiasa wako kwenye siasa, na wametafuta uongozi wa siasa kwa kusaka madaraka tuu, uongozi as a means of livelihoods, lakini kiukweli siasa hawaziwezi, hawazijui wala hawajui uongozi wa umma sio utumishi wa chama ni utumishi wa watu.

Kwenye bandiko hili, nilieleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya Tanzania, vyama vya siasa sio mali ya viongozi, sio mali ya wanachama, ni mali ya umma, hivyo maamuzi yoyote ya chama lazima yatangulize mbele maslahi ya umma.

Vyama vya siasa kama vilivyo vyama vya wafanyakazi, vina uhuru wa kugoma, kufanya maandamano na hata kususia jambo lolote, ili mradi kugomea huko au kususa huku, kwa kususa huko kuna something tangible they will achieve. Kususa tuu ili mradi kususa bila ku achieve anything nilikuita ni ujinga.

Leo, nimefarijika sana kusoma haya

Naunga mkono hoja, Hongera sana Mhe. Halima Mdee kwa kukataa ujinga na badala yake kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii, KM wa Chadema, JJ.MNYIKA amesema chama kama chama hakija poleka majina.

Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, najua mtaitisha kikao cha Kamati Kuu ya dharura kulijadili hili, nawashauri, msipoteze muda wala msithubutu kuwatimua as waasi, kwasababu hapo ilipo tuu Chadema is almost dead!, ikiwatimua ndio mwisho wa Chadema!. Kwa vile hawa ni the minority, hata mkiwafuta uanachama, Spika atawalinda as the minority ila pia Watanzania wote wenye akili timamu, hawatawaelewa!, this will be a very sad ending for what was used to be Chadema.

Hapo ilipo tayari Chadema is severely and deeply wounded, uchaguzi huu umewaacha with very big injuries, kitendo walichokifanya wanawake hawa wa Shoka kwa kuongozwa na Halima Mdee, its like adding an insult to an injury, Chadema ikiwatimua, nayo will die instantly, waliotimuliwa ndio watasikika, waliowatimua wenzao, ndio wataishia 6ft under!.

Kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Kususa kupeleka majina ni kosa, mimi niliuita ni ujinga!. Kina Halima Mdee wameukataa ujinga huu, kuwatimua ni kurudia kosa!.
Chadema msifanye death mistakes!.

Paskali
 
Back
Top Bottom