Kizibo
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 4,033
- 8,805
Usinibishie hichi nilichoandika hapa Nipo kwenye business mwaka wa kumi nauzoefu mkubwa naona jinsi biashara za mtaani zinavyoshindwa kukua au kushindwa kuleta matokeo
Kuna makosa madogo yanayofanyika katika upangaji wa bei za bidhaa
Mfano mkoa niliopo energy ya mo madukani mengi wanauza 500 faida yake ni 10%-15% wafanyabiashara makini ukienda kwenye duka lake anauza energy hiyo hiyo kwa 600 faida ya 20%-25 kaongeza sh 100 mteja hawezi kuondoka sababu ya ongezeko hilo nazani umeona gap hilo la faida hapo utapojifunza kwanini biashara moja lakini wanaofanikiwa ni wachache
Hii shilingi 100 inayoongezeka ni kubwa sana kwa mfanyabiashara anayezingatia mauzo yake ya mwezi mzima au mwaka
Unafanya biashara gani na wapi ulipo??
Kwa ujumla ulichoandika hakitekelezeki kwenye maisha ya mtaani.
Kwanza unatakiwa ufahamu hii rule 1 kuhusu wateja, kwamba WATEJA WANA TABIA YA KUAMBIANA/KUSANUANA/KUPEANA TAARIFA.
Mteja anaweza kuacha duka mtaani kwake akafata bidhaa duka mtaa wa 2 kisa tu punguzo la sh 50