Kufeli Mitihani siyo kufeli maisha

Kufeli Mitihani siyo kufeli maisha

Nikiwa katika matembezi mara nikasikia mlio wa honi ya gari kugeuka nakutana na jamaa niliyesoma naye darasa moja, [Class mate] Aliposhusha kioo cha gari na kunisabahi, Nikabaki nashangaa, Jamaa kwa muonekano wa haraka haraka yupo vizuri kiuchumi, Mavazi ya gharama na Micheni ya dhahabu.

Nikakumbuka huyu jamaa darasani alikuwa mmoja wa vilaza, yaani kupata zero ilikuwa kawaida sana.

Je, wewe umewahi kukutana na hali kama hiyo?

Kweli kufaulu mitihani siyo kufaulu maisha, na kufeli mitihani siyo kufeli maisha.

Kwa kifupi maisha hayana formula, Anything is possible by the way.
Sasa unaomba ajira UN, wanakuambia tuletee cheti original cha form 4,chuo huna!
Hapo umenoa bro! Kufaulu ni muhimu pia, maana kuna milango haifunguki kama huna mavyeti! Unaweza kuwa na uzoefu kama eron musk, na kazi, unajua, lakini kama huna mavyeti! Mashirika ya ki ulaya ulaya, ni vigumu(difficult but possible) kuingia!
Cha muhimu ukienda vitani kuwa na siraha zote.
 
Back
Top Bottom