DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Hali hii imeonekana kwa uwazi nchini Tanzania katika miaka ya karibuni, ambapo baadhi ya vyombo ambavyo kiasili na kisheria vinavyopaswa kuwa mabega ya wananchi kama vile Bunge na vyombo vya habari vimeshindwa kuendeleza wajibu wao ipasavyo.
Matokeo ya hali hiyo ni pamoja na kuziba kwa mianya rasmi ya utoaji maoni na kusikilizwa kwa malalamiko, jambo ambalo limewafanya wananchi kutafuta mbinu nyingine za kujieleza, mara nyingi nje ya mifumo rasmi na bila uhariri, bila mwongozo na bila kutumia sanaa za kitaaluma kama ambavyo ingetokea ndani ya taasisi zenye weledi.
Kwa kawaida, vyombo vya uwakilishi na uandishi vina uwezo mkubwa wa kuchuja hoja, kuzipa muktadha, kuzifanyia utafiti, na kuzitoa kwa namna isiyoumiza wala kupotosha. Wanahabari hutumia mbinu za kitaaluma kuhakikisha taarifa inawasilishwa kwa usahihi, huku wabunge wakitarajiwa kutumia majukwaa yao kupaza vilio vya wananchi kwa hoja zilizotafitiwa na kupimwa. Lakini pale ambapo mifumo hii inapoacha nafasi yake, kinachotokea ni kuongezeka kwa sauti nyingi zinazobeba hasira, kukata tamaa, utata au lugha ambazo viongozi huziona kuwa nzito au kukwaza.
Katika mazingira kama haya, mitandao ya kijamii huibuka kama uwanja mbadala. Wananchi huamua kuandika, kurekodi, kushiriki na kupaza sauti zao bila kujali kama lugha yao inafuata maadili au sheria za mawasiliano. Hii siyo kwa sababu wananchi walio wengi wanapenda kwenda kinyume, bali kwa sababu jukwaa lao la kisheria na kitaasisi "limepooza".
Mfano kwa hivi karibuni imeshuhudiwa kwa wingi, wananchi kutoa malalamiko yao moja kwa moja kwenye kurasa za viongozi au taasisi za serikali, ambapo mbinu hizi huonekana kuwa kali au zisizo na staha kutokana na maoni yanayowasilishwa. Lakini ukali huo mara nyingi ni kiashiria cha kufungwa kwa njia rasmi za kufikisha ujumbe.
Ndiyo maana tunashuhudia ongezeko la manung’uniko pale vyombo vya kusemea wananchi vinapokuwa “freeze”, navyo kushindwa kutimiza wajibu wake kunawafanya wananchi wajisemee wenyewe, ambapo kama hatutakuwa makini, linaweza kuwa hatari zaidi kwa mustakabali wa taifa.
BUNGE
Kwa kipindi cha karibuni, kumekuwepo na malalamiko ya wazi na ndani kuwa Bunge limepoteza sauti ya uwakilishi, hasa katika masuala yanayogusa maslahi ya umma. Badala ya kuwa jukwaa la mijadala mikali, yenye hoja, yenye kutetea wanyonge, limeonekana kukosa uthabiti katika kuibua hoja nzito, kukuza uwajibikaji wa watawala, au kulinda maslahi mapana ya wananchi.
Hatua hii imepunguza imani ya wananchi kwa chombo hiki muhimu ambacho kinatumia gharama kubwa kukiendesha kwa pesa zinazotokana na kodi za wananchi hao hao.
VYOMBO VYA HABARI
Vyombo vya habari, ambavyo vinatajwa kama Muhimili wa Nne usio rasmi, navyo vimeingia katika changamoto zinazofanana. Badala ya kuwa macho, masikio na sauti ya wananchi, sehemu ya vyombo hivyo imeonekana kujikita katika kusifu, kupamba, na kuendeleza simulizi zinazounga mkono watawala kuliko kufuatilia maslahi ya umma.
Uandishi wa kiuchunguzi, ambao ni nguzo muhimu ya uwajibikaji, umepungua na kufanya nafasi ya wanahabari ionekane kama ya kupitisha taarifa rasmi badala ya kupaza sauti za walio wengi.
HITIMISHO
Kwa ujumla, kuzorota kwa uwezo wa Bunge na vyombo vya habari kupaza sauti za wananchi kumezalisha pengo na hatari katika mifumo rasmi ya mawasiliano ya umma, pengo ambalo wananchi wameanza kulazimika kulijaza wenyewe kupitia mitandao ya kijamii na njia nyingine bila kuzingatia mwongozo wa kitaaluma wala kisheria.
Ni muhimu kama Taifa kurejesha nguvu, uhuru na uwajibikaji wa vyombo hivi ili sauti za wananchi zisikike mahali panapostahili, kwa staha, kwa usahihi na kwa manufaa.