Kufuatia mvua zinazoendelea nimegunduwa tiles zinaingiza maji, nini tatizo?

Kufuatia mvua zinazoendelea nimegunduwa tiles zinaingiza maji, nini tatizo?

Uko sahii, kwenye uchochoro wa fire escape kuna asili ya chemchem kweli.

Sasa swali maji kupenya tiles kwa mara ya kwa wiki hii inaweza sababu kuu kuwa ni crack au nini?

Na kumaliza tatizo ni lazima uzifumuwe tiles zote uanze moja?
Tiles ni kawaida kupitisha maji kama chini pamejaa maji huwa zinapitisha, sina hakika kama kuna tiles ambazo haziruhusu maji kupita. Labda wataalamu wa ujenzi watusaidie

Hilo la tiles kupitisha maji nimeliona mara kadhaa , Yani tiles inakuwa kama ngozi ya mtu kukiwa na joto inatoa jasho , na tiles zina vinjia vidogo vya kupitisha vijisehemu vya maji
 
Sababu kuu ni water table imepanda kwa sababu ya mvua nyingi zinazoendelea, yamepenya na kuleta nyufa ambazo zinaruhusu maji kutoka juu. Si unajua maji yana tabia ya kutafuta njia!!

Solution ni kutindua, kuondoa tiles na kutengeneza mfumo mzuri wa kuruhusu maji yakipanda(rising table water) yawe yanatoka kupitia mashimo, wanaita sump pump.
 
Kwanza
Hiko sidhani kama ni jambo la kulalama,Yani shukuru kwamba ulipata fundi mwenye uwezo.mana
  • kwa hesabu za kihandisi,nyumba yatakiwa ikae takribani miaka 20 kabla ya kufanyiwa marekebisho makubwa.
  • Nyumba nyingi za sasa hazitimizi hata miaka 10,utakuta ubovu kila sehemu.
Pili
Utatuzi wa tatizo hapo
  • Ita mtaalam wa ujenzi aje akague tatizo ili ajue chanzo ni kipi,ukubwa wa tatizo
  • Mtaalam atakupendekezea njia za utatuzi.

Ni ngumu hapa watu kukupa sababu kamili kwani
  • Maelezo yako bado hayajitoshelezi
  • Hakuna hata picha ya kuonesha mazingira ya nje ya jengo na sehemu ya tiles
  • Ushauri mwingi utakao gewa hapa ni makisio,na unaweza kukuingiza mkenge.
 
Umenieleza kitaalam, ila swali je hiyo crack imetokea mwaka huu? Maana miaka yote 24 sijawahi kuona hali hii.
Inategemea tunarud ktk ule usem wa usipoziba nyufq utajenga ukuta.

Crack inaweza isiwe ktk tiles ikaw ktk kingo au ktk ile mistar inayotenganisha tiles means CEMENT imezidiw uwezo au kuna katundu tu..

Kumbuka unaweza jenga sehem yenye chemchem pia au ikaw chemchem mpy ipo discovered hapo.. perhaps.

Cha kufanya ita fundi, aje abomoe tiles kadhaa hapo au chumba kizima aweke zingine.. simple and longterm solution.
 
Hii nyuma nimejenga mwaka 2000 Kwa kufuata vigenzo vyote vya ufundi.

Nimeshangaa hizi mvua za mwaka kuna chumba nikiingia nakuta wet kuna majimaji, naagiza papigwe deki pakaushwe nikija tena nakuta wet majimaji hapo ndio sasa naamini maji yanatokea chini yanapenya taratibu kwenye tiles na Mimi sijajenga mabondeni, tatizo ni nini hapo na nifanyaje?
umeshapata solution?
 
Back
Top Bottom