Kufufuka kwa wafu - Ni maajabu yanayoendelea kwa kasi nchini huku wanahabari/jamii wakizipa nafasi ndogo kama habari zinazohitaji uchunguzi wa kina

Kufufuka kwa wafu - Ni maajabu yanayoendelea kwa kasi nchini huku wanahabari/jamii wakizipa nafasi ndogo kama habari zinazohitaji uchunguzi wa kina

Uchunguzi wa nini Hearsay ?..., Hio itakuwa ni kufanya reporting na sio kuchunguza.., huenda baada ya initial observation wakaona dalili za uongo / kupotosha (sasa badala ya kurudi na jibu la shutuma wanawaachia wengine kuripoti kilichojiri / kilichohadithiwa) ndio wewe umekiona hata kukileta hapa....

Na hizi story hazijaanza leo (kuanzia story za Gamboshi, Misukule n.k.) kwahio hakuna uhaba wa reporting...

Thus my point is..., hizi habari zinapata derserved attention hakuna haja ya kuzi-excalate zaidi ya hapo; tuwekeze nguvu kwenye uchunguzi wa mafisadi, tabia nchi, na kwanini si tu masikini with all these resources....
WE NI MCHAWI UNAJARIBU KUPINDISHA MADA
 
Kama una shaka na kifo cha ndugu yako usikimbilie haraka kuzika na kama mkizika usifanye 40.
 
Ushirikina ni mfumo wa maisha ambao serikali ya jamhuri ya muungano hauutambui. Ukitaka kuuthibitisha nenda kwa wanaoutambua.

Hakuna heshima utakayopewa katika kuthibitisha ushirikina maana serikali hauutambui. Labda washirikina ndo wakupe hiyo heshima.
Awautambui lakini viongozi wao ni washirikina.
Kuutambua uchief ni kuamini ushirikina.
 
WE NI MCHAWI UNAJARIBU KUPINDISHA MADA
Kama Uchawi ni kuweza kufanya vitu ambavyo haviwezekaniki kwa hali ya kawaida basi I wish ningekuwa Mchawi...

Ila kama uchawi ni kudhuru wengine its not on my nature..., hata kama ningekuwa nao huo uwezo nisingeutumia...., (Its just tools and depend how you use them) mfano wewe hapo kama umepewa usimamizi wa pesa za UMMA na badala ya kufanya kile kinachotakiwa ukazili basi in my books wewe ni Mchawi
 
Habari za watu kufa na kuzikwa na baadae kupatikana wakiwa hai ni za kushangaza mnooo.

Yaani mtu amekufa kwa kuugua au ajali au ghafla tuu, hospitalini wanahakikisha amekufa na wanatoa cheti cha kifo na mwili mnakadhiwa, mnaenda kuzika na viongozi wa serikali za mtaa, viongozi wa dini na familia wanashiriki na kusema Mungu amempenda zaidi.

Imagine wafiwa wanaomboleza na kusahau kisha baada ya muda marehemu anapatikana yupo hai katika hali tata. Hili jambo ni la kutisha na kushangaza sana na ni jambo linalodhihirisha uwepo watu wengi wanaodhaniwa wamekufa lakini inawezekana kabisa wapo kama walivyopatikana hawa.



Waandishi wa habari nadhani huu ni muda muafaka wa kulifanyia hili jambo habari za uchunguzi wa kina. Uchunguzi ambao utasaidia kujua haswa ni nini kinatokea hadi binadamu anaonekana amekufa, tena kitabibu kabisa mahospitalini, anazikwa na kisha anapatika akiwa hai.



Hizi habari zinagusa uhai wa mwanadamu lakini bahati mbaya hazipewi airtime kivileee na medias rasmi wala zile za udaku wala hazifanyiwi uchunguzi utakaoisaidia jamii mbeleni. Badala yake habari Zinazokik ni zile za Connections (ngono) na hapa ndio utagundua nguvu gani imeshikilia mitandao ya kijamii



Mungu atusaidie kumtafuta yeye na nguvu zake

Watakuwa wanafufuliwa na Yule anayejiita askofu pale Kawe, lakini hebu ngoja mmmmmh hivi Amina chifupa ndo alikuwa mbishi kufufuka enh?
 
Shida ni kwamba ukisema upekenyue hizi habari kwa undani malamka zitakuandama kwamba unapromote ulozi..
Na hili litakuwa tatizo lingine baada ya kuzuia freedom of expression, hakuna hata freedom of exploration. Halafu unategemea kupromote innovations? No wonder research nyingi ziko stooni, hakuna hata wa kuzifanyia kazi. Tunasuribiri wachina na watu wengine waseme "chanjo hazina madhara", na sisi tukariri "Hazina madhara", hata kama tunakufa, hatutakiwi kulia kwa kuwa jirani anacheka!. Kuna mengi ya kufadhaisha.
 
Back
Top Bottom