Not_Yet_Uhuru
JF-Expert Member
- Oct 11, 2010
- 1,304
- 432
Wadau wa JF Great Thinkers,
Kwa wale wanaotaka kuutambua ukweli ili ukweli uwaweke huru na wadumu ktk nuru hiyo daima wataafikiana na uwazi na wataukubali ukweli hata kama unawaumiza saana, watajua ndio mwelekeo wa haki.
Tangu mwaka jana, mara baada ya kumalizika kwa bunge maalumu la katiba, serikali ya ccm ilifanya matamasha, kuhamasisha na kusherehekea 'katiba pendekezwa' kuwa 'ccm wameshinda' dhidi ya 'wapinga rasimu ya 2 ya katiba' kama ilivyowasilishwa na jaji joseph sinde warioba. Hii ikimaanisha kuwa ccm walianza kusherehekea [hadi kucheza taarabu bungeni waziwazi] hata kabla ya kuanza kunadi kwa wananchi ili waelewe kilichoandikwa ndani ya chapisho hilo waliloliita 'katiba pendekezwa' na pia mikakati iliwekwa kuhakikisha kuwa chapisho hili halisambazi mapema sana, halichapishwi nakala nyingi sana, na haliwafikii wengi saana [tofauti na walengwa wa ccm], hii yote ni kuhakikisha kuwa mikakati ya watawala kuelekeza watu waipigie kura ya ndio inafanikiwa siku na wakati utakapofika. Siyo hivyo tu:
* Kikwete mwenyewe na makamu wake kupitia serikali yake yote iliandaa bajeti ya mabilioni ili kuhakikisha vyombo vya habari [hasa vinavyomilikiwa na serikali, na hasa tbc1, magazeti, radio na vile vingi vya binafsi ila vinavyoendeshwa 'kinjaa njaa' kuwa upande wa kuwaelekeza na kuwafundisha wananchi la kufanya] vinaandaa programu kabambe kuhamasisha na kuwaelekeza wananchi popote waipigie katiba pendekezwa kura ya ndiyo!!! Toka mwaka jana hadi leo hii 'mafundisho' hayo na 'maelekezo' hayo ya kupiga kura ya ndiyo yanaendelea!! Ukweli ni uhuru na hatuwezi kufumbia macho unafiki au woga utokanao na watawala, au wapambe wao wanaohemea ktk meza zao ili kushibishwa na kusahau utu wao.
Je, hayo yote yaliyofanyika kwa aidi ya miezi 7, hayakuwa mafundisho, maelekezo na kuingilia uhuru wa mwananchi kusema ndiyo au hapana?? Kwa nini serikali haikuwaelekeza kuwa wasome machapisho hayo ili siku ya kura 'waamue watakavyo'?? Bali inasema wazi wazi kuwa waipigie kura ya ndiyo?? Unafiki! Mhashamu kardinali pengo hakupata ufahamu wa 'matenddo haya maovu' ya serikali na ccm kuingilia 'akili au dhamira' za wananchi [ambao ndio waumini wake pia] kuwaelekeza wapige kura ya ndiyo badala ya kujiamulia wenyewe? Upofu huo!
* Baraza la maaskofu na jumuiya za makanisa ya kikristo yaliyotoa tamko rasmi hivi karibuni la kuwaelimisha waumini na watanzania wote waiosome katiba pendekezwa [ambayo hata hivyo imefichwa-fichwa, tena wasioielewa, na imevurugwa mambo muhimu] na kuipigia kura ya hapana ili 'kuikataa' ni tamko na fundisho sahihi kabisha ni la haki, elimu sahihi, na iliyojaa ukweli na unayoutenga unafiki pembeni na kueneza nuru itawale ili taifa lipate chombo sahihi, na kamilifu kinachoitwa katiba ya wote. Maaskofu na viongozi hawa wa dini walichelewa sana kutoa tamko au mafundisho yao maana serikali ilianza toka mwaka jana, ndipo ukawa nao wakaikabili serikali na ccm kwa kuwaelekeza wafuasi wa wasiipigie kura! Lakini ukweli ni kuwa baraza la maaskofu na jumuiya za makanisa ya kikristo tanzania, wapo sahihi, wapo ktk haki na tunawaomba wasimamie waliyoyasema na kuyaelekeza makanisa yote tanzania nzima, waumini wao wasimame imara kupiga kuwa ya 'hapana'!
Haki inajibiwa kwa haki, na sio dhuluma! Kama serikali imetumia miezi zaidi ya 7 kuwafundisha wananchi wapige kuwa ya 'ndiyo' basi viongozi wetu wa dini wapo sahihi kuwafundisha waumini wao wapige kura ya 'hapana' angalau kwa hizi wiki chache zilizobakia, ili haki ikamilike! Kuwakemea maaskofu kwa tamko lao ni unafiki, upofu na woga wa kuukwepa ukweli, au 'kujipendekeza kwa kaisari'. Mh askofu mkuu kardinali pengo angetambua kuwa kushirikiana na 'kaisari' [serikali] kuwapokonya watauwa haki, 'kuwanyima kauli' au kuwaingiza wtu ktk giza nene kama la kuipa nchi katiba mbovu...hii dhambi haitafutika usoni pako daima!! Hii ni kwaresma...tutende haki-kwa-haki.
Nawasilisha kwa mjadala!