Kufundisha Watu Kura ya Ndiyo (Serikali), Hapana (Maaskofu,UKAWA) ni Sahihi?

Upuuzi mwingine wa Serekali ya Ccm ni kuwaambia watu wasome katiba waielewe wakati wamechapisha nakala milioni 2, sasa sijui watakaopga kula ni hao tu mil2!
 
Watu wahamasishwe tu kujitiokeza kwa wingi kupiga kura na viongozi wa serikali na dini.

Lakini viongozi wa vyama vya siasa ruksa kueleza wanataka watu wapige upande gani.

Ila nadhani kuna tatizo la viongozi hasa wa dini kuchanganya mambo kisa eti wamemsikia raisi kasema watu wapige kura ya ndiyo.Raisi ni mwenyekiti wa CCM taifa.Akiongea mambo ya kutaka watu wapige kura ya ndiyo anaongea msimamamo wa chama chake yeye akiwa kiongozi wa chama.

Lakini inapofika askofu ambaye anaongoza kanisa lenye wanachama wa UKAWA ,CCM na wasio na vyama naye akajitosa eti kupigia debe eti kura ya ndiyo au hapana hapo anakuwa hajui vizuri kazi yake kama kiongozi wa dini kwa waumini wake wenye vyama tofauti na misimamo tofauti ya kisiasa.Maaskofu ni vizuri wabakie kwenye majoho yao siasa wawaachie waumini.Askofu awaambie tu waende kupiga kura kwa kadri ya dhamiri zao kisha aendelee kuwaswalisha wakishatoka kupiga hiyo kura sawasawa na dhamiri zao.

With due respect mkuu,

Kikwete na serikali yake wangelikuwa wanawaambia wana-ccm wapige kura ya ndiyo wala isingekuwa taabu. Lakini wanawaambia watanzania (wakiwemo ukawa na wasiokuwa na vyama) kwamba wapige kura ya ndiyo.

Pili, yeyote anayeelewa falsafa ya uongozi bora anatambua pia kwamba huwezi ukatenganisha kiongozi wa imani na kiongozi wa serikali juu ya jukumu la uhuru, amani na ustawi wa jamii. Wote majukumu yao kwenye ustawi wa jamii yanafanana. Tofauti tu ni jukwaa gani linatumika. Hivyo basi jukwaa moja linapopiga kampeni zisizokuwa balanced ni lazima jukwaa la pili liweke balance hiyo ili mzani wa haki uendelee kusimama. Na hicho ndicho maaskofu walichofanya.

Tatu, amani isipokuwepo hata nyumba za ibada zitakosa waumini na hivyo kukwamisha kazi za viongozi wa imani. Hivyo basi, viongozi wa imani wanayo haki ya kuongoza na kukemea hasa pale hatari inapokuwa dhahiri.

Mwisho, serikali husimamia mwili na dini husimamia roho. Kama ambavyo haiwezekani kutenganisha mwili na roho na bado mtu akabaki kuwa binadamu kamili ndivyo ilivyo vigumu kutenganisha dini na serikali kwenye jambo linalomhusu binadamu yuleyule.

Yatosha maovu yake kwa siku!
 
Rais pia ni kiongozi wa nchi na yeye alipaswa kusisitiza watu wajitokeze kupigia kura katiba pendekezwa kwa kadri ya uelewa wao na c kusema wapigie kura ya ndio mkuu

Inategemea anapoongea wakati huo kavaa kofia ipi ya chama au serikali.Huwezi mfunga mdomo akivaa kofia ya chama asiongee hivyo ni sawa na kumvua uenyekiti wa chama wakati kachagulliwa kihalali hadi msajili wa vyama vya siasa anamjua yeye kuwa ndie mwenyekiti wa CCM.

Akiwa kofia la Uraisi atahamasisha watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura wanayoitaka.Akiwa katika kofia la CCM atahamasisha watu wajitokeze kwa wingi wapige kura ya ndiyo.Kofia zote zake na ana uhalali nazo.Hivyo akiongea inabidi umtizame aongea kama mwenyekiti wa CCM au kama Raisi.
 
Watu wahamasishwe tu kujitiokeza kwa wingi kupiga kura na viongozi watendaji wa serikali na dini.

Lakini viongozi wa vyama vya siasa ruksa kueleza wanataka watu wapige upande gani.

Ila nadhani kuna tatizo la viongozi hasa wa dini kuchanganya mambo kisa eti wamemsikia raisi kasema watu wapige kura ya ndiyo.Raisi ni mwenyekiti wa CCM taifa.Akiongea mambo ya kutaka watu wapige kura ya ndiyo anaongea msimamo wa chama chake yeye akiwa kiongozi wa chama.

Lakini inapofika askofu ambaye anaongoza kanisa lenye wanachama wa UKAWA ,CCM na wasio na vyama naye akajitosa eti kupigia debe eti kura ya ndiyo au hapana hapo anakuwa hajui vizuri kazi yake kama kiongozi wa dini kwa waumini wake wenye vyama tofauti na misimamo tofauti ya kisiasa.Maaskofu ni vizuri wabakie kwenye majoho yao siasa wawaachie waumini.Askofu awaambie tu waende kupiga kura kwa kadri ya dhamiri zao kisha aendelee kuwaswalisha wakishatoka kupiga hiyo kura sawasawa na dhamiri zao.

Hapo kwenye red, Mmmmh, ww lazima ni wa mlango tofauti na baraza la Maaskofu. Wao hawaswali wana sali. Acha udini angalia hoja.
 
Kikwete na serikali yake wangelikuwa wanawaambia wana-ccm wapige kura ya ndiyo wala isingekuwa taabu. Lakini wanawaambia watanzania (wakiwemo ukawa na wasiokuwa na vyama) kwamba wapige kura ya ndiyo.

Mwisho, serikali husimamia mwili na dini husimamia roho. Kama ambavyo haiwezekani kutenganisha mwili na roho na bado mtu akabaki kuwa binadamu kamili ndivyo ilivyo vigumu kutenganisha dini na serikali kwenye jambo linalomhusu binadamu yuleyule.

Wapiga kura siku zote ni wengi kuliko wanachama wa vyama.Hivyo kiongozi wa siasa awe UKAWA au CCM kuwaomba watanzania na si wanachama wao tu wapige kura ya ndio au hapana ni sawa si kitu cha ajabu.Sababu ukitizama hata wabunge ,madiwani na raisi wanaowapa kura wengi si wanachama wa vyama vyao! unakuta chama eneo kinawanachama 100 kura za mbunge au raisi 1,000.Sio ajabu na nawaomba vyama vyote waendelee nalo tu.

Kuhusu mipaka kama ulivyosema kuna mwili na roho ni sawa.Lakini kila upande ni vizuri ukakaa eneo lake.Naogopa kiongozi wa kiroho akitoka akaenda kwenye upande wa mwilini aweza kukutana na vichaa walio mwilini sana wakafunua kanzu ya kiongozi ya dini na kuchungulia ndani kuna nini na kuanza kukufuru kwa watakachoona humo.Hivyo ni vizuri Kiongozi wa dini akajibakia kibla,au altareni au madhabahuni akiendelea na mambo yake ya rohoni kuliko kujitosa kichwa kichwa kwenye mambo ya siasa ambayo yanajulikana kabisa kuwa ni mchezo mchafu.
 
not_yet_uhuru tambua kwamba serikali ni kaizari na maaskofu ni watumishi wa bwana..serikali kufundisha wananchi wapige kura ya ndio wako sahihi kabisa kwa kuwa katiba ni mtoto wao waliyemuasisi na wanataka kumhalalisha lakini ikitokea watumishi wa bwana wanaingilia serikali na kuwadanganya waumini kwamba ati watapata dhambi wakipiga kura ya ndio hapo unapaswa kutia shaka uadilifu wa hao watumishi wa bwana kwani wameenda kinyume na usemi wa "ya kaizari mpe kaizari na ya Mungu mpe Mungu". watuache tuisome kwani dunia yetu chaguo letu sisi ndio tutaamua tupige kura ya ndiyo au hapana

Tusijidangaye...siku [Serikali] Kaisari atakapokengeuka na kuharibu amani na utulivu kwa kulazimishia dhuluma badala ya Haki ...Serikali hiyo iyo atageukia Kanisani [Dini] na kuwaomba wahamasishe, wawafundishe waumini wao kuombea Amani na kuacha ghasia...Hapo Kaisari atakuwa anaingilia Mungu au? Walipoanza kuivuruga Rasimu ya 2, bunge lilianza kuvurugika, wasiwasi ukajaa nchi nzima...Serikali hiyo hiyo iliyowatusi Viongozi wa Dini, iliwageukia na kuwaomba waalike waumini wao wote waombe Amani isipotee! Walipoipitisha kwa hila, walianza kuwasuta Viongozi wa dini na kuwaambia wakae kimya...! What a nonsense! Kaisari anapohitaji kukamilisha Hila a utawala wao...Dini inatumiwa kama nyenzo kuwavuta waumini wamshabikie Kaisari na kulinda udhalimu...ila inapotokea Dini kuwaelimisha Watu kuipinga Dhumula hiyo, Kaisari anaigeuka dini na kusema inahatarisha amani...TUWE NA AKILI, TUFIKIRI, TUTAFAKARI na kutenda HAKI. KURA YA 'NO' ndiyo Sahihi.
 
Baba Askofu Cardinali Pengo alipotoka na naamini hadi sasa atakuwa ameshagundua kosa lake kwenye hili na naamini ataliachia baraza la maaskofu na na Jukwaa la wakristo wafanye vyema kazi yao iliyotukuka. ukitaka kujua kuhusu hili hutamsikia tena Cardinali Pengo akiuongelea suala hili hadharani !!

Imeandikwa rushwa hupofusha; huwa kawa kipofu atang'ang'ana nalo tuuuu
 
Wapiga kura siku zote ni wengi kuliko wanachama wa vyama.Hivyo kiongozi wa siasa awe UKAWA au CCM kuwaomba watanzania na si wanachama wao tu wapige kura ya ndio au hapana ni sawa si kitu cha ajabu.Sababu ukitizama hata wabunge ,madiwani na raisi wanaowapa kura wengi si wanachama wa vyama vyao! unakuta chama eneo kinawanachama 100 kura za mbunge au raisi 1,000.Sio ajabu na nawaomba vyama vyote waendelee nalo tu.

Kuhusu mipaka kama ulivyosema kuna mwili na roho ni sawa.Lakini kila upande ni vizuri ukakaa eneo lake.Naogopa kiongozi wa kiroho akitoka akaenda kwenye upande wa mwilini aweza kukutana na vichaa walio mwilini sana wakafunua kanzu ya kiongozi ya dini na kuchungulia ndani kuna nini na kuanza kukufuru kwa watakachoona humo.Hivyo ni vizuri Kiongozi wa dini akajibakia kibla,au altareni au madhabahuni akiendelea na mambo yake ya rohoni kuliko kujitosa kichwa kichwa kwenye mambo ya siasa ambayo yanajulikana kabisa kuwa ni mchezo mchafu.

Tumeaminishwa miaka mingi kwamba siasa ni mchezo mchafu, SIYO KWELI!!!!! Siasa ni nzuri sana kama ambavyo dini ni nzuri sana. Walio wachafu ni wale walioko kwenye siasa.

mwili hauwezi kwenda bila roho, hali kadhalika roho bila mwili. Tusitake kutenganisha mwili na roho kisa tu kuwafurahisha wachafu wanaotuaminisha kuwa siasa ni chafu.

Kama unataka kuwa neutral kwa kuweka uwanja sawa, basi serikali iache kupigia kampeni ya ndiyo katiba pendekezwa na maaskofu waache kupigia kura ya hapana katiba pendekezwa ili wananchi waisome na kuamua kwa utashi wao. Nje ya hapo, hakutakuwa na mwenye moral authority ya kumkataza mwenzake kufanya anavyoona inafaa.

Tusisahau pia kwamba katiba ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa. Sasa watawala wanaposhadidia kupiga kura ya ndiyo, kunanini nyuma ya pazia???
 
Upuuzi mwingine wa Serekali ya Ccm ni kuwaambia watu wasome katiba waielewe wakati wamechapisha nakala milioni 2, sasa sijui watakaopga kula ni hao tu mil2!

Upo sahihi Mkuu...ndiyo maana tunasema, Wanaoishabikia kura ya Ndiyo kwa kutokuelewa, wakae chini watambue machache yafuatayo! Katiba Pendekezwa ilikamilika karibia miezi 8 iliyopita, wameshindwa kuchapisha nakala milioni 5 tu hadi leo, au wamevuta muda au kukataa kuwakabidhi wafadhili au taasisi za ndani ziwachapishie kwa miezi 8 na kusambazia wananchi waielewe, kuna hila gani hapo? Hata Wabunge wenyewe, baadhi yao walilalamika waziwazi kuwa hawajawahi kuiona hiyo nakala. Then, je, Vijijini wanaelewa nini kuhusu Katiba Mpya? Elimu haipo, hakuna lolote, Watawala wamechelewesha makusudi kabisa kuwaelimisha wananchi, na pia isitoshe wamefanya wawezavyo kukwamisha raia wasielimishwe! Pia Mfumo wa BVR wanaotumia kuandikisha Wapiga kura umejaa hila, udhaifu, vifaa havikuandaliwa, na kila anayejua hayo anaona nchi inakopelekwa...ni gizani! Kwa hiyo mtu akisema kura iwe ya NDIYO, amepotoka mno, hajatafakari, na anapelekwa tu kama upepo! Yafaa apuuzwe mno!! Kura ni ya 'HAPANA', au 'NO'
 
CCM itabaki na BAKWATA yao coz hawajitambui mashehe ubwabwa
 
Watu wahamasishwe tu kujitiokeza kwa wingi kupiga kura na viongozi watendaji wa serikali na dini.

Lakini viongozi wa vyama vya siasa ruksa kueleza wanataka watu wapige upande gani.

Ila nadhani kuna tatizo la viongozi hasa wa dini kuchanganya mambo kisa eti wamemsikia raisi kasema watu wapige kura ya ndiyo.Raisi ni mwenyekiti wa CCM taifa.Akiongea mambo ya kutaka watu wapige kura ya ndiyo anaongea msimamo wa chama chake yeye akiwa kiongozi wa chama.

Lakini inapofika askofu ambaye anaongoza kanisa lenye wanachama wa UKAWA ,CCM na wasio na vyama naye akajitosa eti kupigia debe eti kura ya ndiyo au hapana hapo anakuwa hajui vizuri kazi yake kama kiongozi wa dini kwa waumini wake wenye vyama tofauti na misimamo tofauti ya kisiasa.Maaskofu ni vizuri wabakie kwenye majoho yao siasa wawaachie waumini.Askofu awaambie tu waende kupiga kura kwa kadri ya dhamiri zao kisha aendelee kuwaswalisha wakishatoka kupiga hiyo kura sawasawa na dhamiri zao.
teh teh, kwa hiyo mkuu katiba ni ya wanasiasa tu? Pole sana mkuu!
 
Kwenye suala hili la katiba maaskofu wako sahihi. Katiba ni ya watu wote, wenye dini na wasio na dini. Maaskofu bado wana haki ya kushiriki katika mambo ya taifa lao, hii ni haki ya kikatiba!
 
Wanaosmema hapana so far ni UKAWA, Maaskofu, wanaharakati wengi vs ndiyo ambapo ni Serikali na CCM pamoja na vyama vidogo nje ya UKAWA!
Mpambano ni mkali sana! Tusubiri hatma ya yote!
 
Wapiga kura siku zote ni wengi kuliko wanachama wa vyama.Hivyo kiongozi wa siasa awe UKAWA au CCM kuwaomba watanzania na si wanachama wao tu wapige kura ya ndio au hapana ni sawa si kitu cha ajabu.Sababu ukitizama hata wabunge ,madiwani na raisi wanaowapa kura wengi si wanachama wa vyama vyao! unakuta chama eneo kinawanachama 100 kura za mbunge au raisi 1,000.Sio ajabu na nawaomba vyama vyote waendelee nalo tu.

Kuhusu mipaka kama ulivyosema kuna mwili na roho ni sawa.Lakini kila upande ni vizuri ukakaa eneo lake.Naogopa kiongozi wa kiroho akitoka akaenda kwenye upande wa mwilini aweza kukutana na vichaa walio mwilini sana wakafunua kanzu ya kiongozi ya dini na kuchungulia ndani kuna nini na kuanza kukufuru kwa watakachoona humo.Hivyo ni vizuri Kiongozi wa dini akajibakia kibla,au altareni au madhabahuni akiendelea na mambo yake ya rohoni kuliko kujitosa kichwa kichwa kwenye mambo ya siasa ambayo yanajulikana kabisa kuwa ni mchezo mchafu.
teh teh, kwa hiyo katiba ni ya wanasiasa tu?
 
Ccm wananihamasishaje kusoma katiba ambayo haitokani na maoni yangu??

OMBI KWA MAASKOFU.
Msiwazuie kwenye kusanyiko, tangazeni kuwapiga marufuku kukomunika (sacramenti) sadaka zao ni chukizo na dhihaka machoni petu, hawana stahili ya kupata maombezi ya kanisa n.k

Kwa maana wamelitukana kanisa hivyo wamepungukiwa na utukufu duniani.
 
Tume ilifanya kazi nzuri sana mpaka wakampoteza mtetea haki za wanyonge Dr. Mvungi. Kazi yao ikaenda kuchakachuliwa na watu wasio na maadili mema fisadi Chenge na wenzake. Sasa mimi na marafiki zanu wote tutapiga kura ya HAPANA!
 
Back
Top Bottom