Kufunga ndoa kwangu kumeniondolea marafiki wengi

Hii comment yako naenda kuiwekea lamination kabisa
Asante.

Watu wengi wanajua hayo, isitoshe uchumi wa wengi hauruhusu michango, tena siku hizi unapangiwa kabisa viwango vya kuchangia.

Ila wengi wanaoneana aibu kuambiana ukweli kwamba michango hii ni mizigo sana.
 
Hivi wazee wetu huko nyuma walikuwa na michango kama hivi sasa? Huwa nashangaa sana mtu anataka kuoa lakini ametageti michango kutoka kwa watu ili kufanikisha harusi yake utafikiri tutakuwa tunato**** wote.

Mimi najipanga kuwa na ka harusi ka watu wasiozidi 10 ukoondoa ndugu. Na sitaki mchango wa mtu..

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Umesema suala la kuendeleza utamaduni bila kujadili uzuri au ubaya wa utamaduni.

Kama unaweza kula mavi kwa sababu ni utamaduni wenu tu, sina cha kujadiliana nawe zaidi.

Nikijadiliana nawe zaidi unaweza kuniambukiza kipindupindu cha akili buree.
hapo ndoambapo tumeshindwa kuelewana nimesemea kulingana na mleta mada hapo juu kuchangiwa harusi ni jambo la kawaida sababu tumelikuta na tunaendelea kuchangishana
 
Word[emoji108]
 
hapo ndoambapo tumeshindwa kuelewana nimesemea kulingana na mleta mada hapo juu kuchangiwa harusi ni jambo la kawaida sababu tumelikuta na tunaendelea kuchangishana
Na mimi nakwambia hivi, jambo kuwa la kawaida kwa sababu umelikuta, ni utamaduni wetu, si hoja.

Tungetumia mantiki hiyo, kusingekuwa na maendeleo yoyote yanayobadilika kwa kubadilisha utamaduni katika jamii.


Tujadili uzuri au ubaya wa jambo, tusijadili jambo ni la kawaida tumelikuta, ni utamaduni wetu, na tunaliendeleza.

After all, kawaida ya jana inaweza kuonekana si kawaida leo, kwa sababu jamii inaenda ikijiongeza na tamaduni zinabadilika.

Ndiyo maana kuna tamaduni za kutahiri wanawake zilionekana kawaida zamani, leo zinaachwa.

Kwa hivyo, kama tunataka kukubali au kukataa kitu, tujadili uzuri au ubaya wa kitu.

Tusiweke hoja ya "huu ni utamaduni wetu, tumeukuta na tutauendeleza".

Kwa sababu, kwanza, kitu kuwa utamaduni haimaanishi automatically ni kizuri.

Tulikuwa na tamaduni Watemi wa makabila wakifa wanazikwa na watu walio hai.

Siku hizi huo utamaduni wa kuwa na watemi tumeuondoa, tumeazimia kujenga nchi isiyo na matabaka ya watemi.

Lakini pia, hata kama ni utamaduni ambao hapo awali ulikuwa mzuri, dunia inabadilika.

Inawezekana utamaduni huo ulikuwa mzuri katika dunia ya ujima huko nyuma, lakini leo katika dunia ya teknolojia ukawa mbaya. Hautuendelezi, unatubwetesha tusiendelee kwenda na dunia ya leo, unatubakisha kwenye ujima.

Kwa hivyo hata kama utamaduni ulikuwa mzuri hapo awali, hiyo si sababu ya kuendelea nao tu kwa sababu tu "huu ni utamaduni wetu tunauendeleza".

Inabidi tuuchunguze na kuangalia kama unatufaa au hautufai.
 
Hata Mimi ungenipoteza kama Rafiki.

Huu upumbavu Wa kuchangishana Harusi sijui unapaswa ufe Mara moja. Binafsi huwa sichangii mtu Harusi, kwa maana sikuomba mchango kwa mtu pia.
 
Hata Mimi ungenipoteza kama Rafiki.

Huu upumbavu Wa kuchangishana Harusi sijui unapaswa ufe Mara moja. Binafsi huwa sichangii mtu Harusi, kwa maana sikuomba mchango kwa mtu pia.
Jamii ikijiongeza utamaduni huu utakufa wenyewe.

Tunavyozaliana, Dar es salaam hivi karibuni itafikia population ya watu milioni 10.

Hapo hata kama ukitaka kuchangia watu itabidi uwe na mshahara wa pili wa kuchangia watu tu. Maana utashindwa kuamua umchangie nani na umuache nani.

Kitendo cha kumchangia huyu na kumuacha huyu tayari ni lawama.

Ufumbuzi wa tatizo ni kuacha kuchangia.

This is like one big unregulated Ponzi scheme.
 
Mambo yao waachie wenyewe yasikuumize kichwa...
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
MKUU UMEPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI.
HADI UMEPANIKI BRAZA[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]...smh.
Harusi ni jambo la furaha (yako mwenyewe). Halafu ukae unategemea watu kisa uliwachangia. Unaona sasa wao hata hawakuogopa kukunyima michango yao!!! Ushajifunza[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
well said,case closed
 
NILICHOKISEMA MIMI NI MARAFIKI WA KARIBU IMAGINE MTU ULIKUA KWENYE KAMATI YA NDOA YAKE NA SIKU UNAFUNGA NDOA AUTOMATIC UKIWAZA WATU WAKUJA KUSHEREHEKEA NAO NAE YUMO CHA KUSHANGAZA UNAMPIGIA SIMU HAPOKEI

KINGINE AS SAID 80% BURGET YA NDOA YENYEWE ILIKUA NI PESA YANGU NA WALA CKUFANYA SHEREHE KUBWA AMBAYO SINA UWEZO NAO WHAT I DID I JUST PICKING CLOSER FRIENDS

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
huu ni umasikini uliopitiliza,,, raha zako wewe iwe tabu kwa wengine!?

dogo tafuta pesa
 
Naunga mkono maelezo yako, ila huu utamqduni ambao tumeukita iko hata ya kuubadilisha , hii ni kulingana na mwenendo wa maisha ya sasa. Mfano; mtu atatumia zaidi ya milioni 10 kwa ajili ya sherehe ya harusi, je hebu mpe mtu anae- straggling na maisha hiyo million 10 uone baada ya mwaka atakuwa kwenye level gani. So guys, we have to think about this. Ni bora tuchange ili akaanzie maisha na sio kula na kunywa kwenye li ukumbi la kifahari halafu baada ya siku kadhaa mnaulizana kodi imeisha tukamkope nani. NO si sawa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja.

Tatizo kuna watu washachanga sana wakisubiri na wao kuchangiwa, na hao ukiwaambia tunaondoa utamaduni huu, wataona umewaonea.

Kwa sababu wao walichangia wengine kwa madhumuni ya kuchangiwa.
 
Naunga mkono hoja.

Tatizo kuna watu washachanga sana wakisubiri na wao kuchangiwa, na hao ukiwaambia tunaondoa utamaduni huu, wataona umewaonea.

Kwa sababu wao walichangia wengine kwa madhumuni ya kuchangiwa.
Hapo ni kweli mkuu, ila ipo haja ya kuliangalia kwa undani jambo hili.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…