hapo ndoambapo tumeshindwa kuelewana nimesemea kulingana na mleta mada hapo juu kuchangiwa harusi ni jambo la kawaida sababu tumelikuta na tunaendelea kuchangishana
Na mimi nakwambia hivi, jambo kuwa la kawaida kwa sababu umelikuta, ni utamaduni wetu, si hoja.
Tungetumia mantiki hiyo, kusingekuwa na maendeleo yoyote yanayobadilika kwa kubadilisha utamaduni katika jamii.
Tujadili uzuri au ubaya wa jambo, tusijadili jambo ni la kawaida tumelikuta, ni utamaduni wetu, na tunaliendeleza.
After all, kawaida ya jana inaweza kuonekana si kawaida leo, kwa sababu jamii inaenda ikijiongeza na tamaduni zinabadilika.
Ndiyo maana kuna tamaduni za kutahiri wanawake zilionekana kawaida zamani, leo zinaachwa.
Kwa hivyo, kama tunataka kukubali au kukataa kitu, tujadili uzuri au ubaya wa kitu.
Tusiweke hoja ya "huu ni utamaduni wetu, tumeukuta na tutauendeleza".
Kwa sababu, kwanza, kitu kuwa utamaduni haimaanishi automatically ni kizuri.
Tulikuwa na tamaduni Watemi wa makabila wakifa wanazikwa na watu walio hai.
Siku hizi huo utamaduni wa kuwa na watemi tumeuondoa, tumeazimia kujenga nchi isiyo na matabaka ya watemi.
Lakini pia, hata kama ni utamaduni ambao hapo awali ulikuwa mzuri, dunia inabadilika.
Inawezekana utamaduni huo ulikuwa mzuri katika dunia ya ujima huko nyuma, lakini leo katika dunia ya teknolojia ukawa mbaya. Hautuendelezi, unatubwetesha tusiendelee kwenda na dunia ya leo, unatubakisha kwenye ujima.
Kwa hivyo hata kama utamaduni ulikuwa mzuri hapo awali, hiyo si sababu ya kuendelea nao tu kwa sababu tu "huu ni utamaduni wetu tunauendeleza".
Inabidi tuuchunguze na kuangalia kama unatufaa au hautufai.