Yani alienda mtu kutoa hela akakosea password, wakamwambia aondoke aende nyumbani baada ya masaa 24 atapata ujumbe wa kumwambia sasa anaweza kuendelea na huduma,
Muda ukapita hakupata meseji yoyote akaamua kurudi tena pale ofisi ya airtel mlimani city,
Kufika pale wakamwambia azunguuke kidogo madukani atapata ujumbe wa kurekebisha,
Wakati anazinguuka dukani akapigiwa simu mtu akajitambulisha kutoka airtel mlimani city,
Akamwambia unatatizo hili, sasa fuata maelekezo yangu,
Akafuata maelekezo sababu alitoka hapo muda si mrefu, kumbe ndo anaibiwa ,
Kutahamaki hela haipo.
Akawafuata wakaanza kumbabaisha hadi leo.
Lakini watailipa ile hela nakwambia,
Kwanza cha kujiuliza yule mwizi amejuaje shida ya Yule mwananchi?
Sent using
Jamii Forums mobile app