Kufungia simu Serikali itapoteza zaidi ya 30% ya kodi toka makampuni ya simu

Kufungia simu Serikali itapoteza zaidi ya 30% ya kodi toka makampuni ya simu

Kuwatupia NIDA lawama kwa zoezi la zimamoto ni kuwaonea,je wanapitia changamoto zipi? Wanna raslimali za kutosha? vitendea kazi je.
Wakifungia line wao ndo watakaoathirika kwa kukosa mapato,kama walivyodhani kuwasomesha watu namba wao wangebaki salama nao wanaisoma hakuna makusanyo yamepungua,check nssf,nhc,nk zilivo hoi baada ya kuziuwa private sector.
JK alikusanya bn 800 clean tax bila kuzipora halmashauri na taasisi zingine mapato yao.
Na je line yako ikifungwa ? Unaweza kuifungua kwa kuisajili baada ya kupata kitambulisho ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi nida tunawafanya mbuzi wa kafara, scape goat, sheria ya tcra cap306 ya 2010 ibara ya 93 ibara ndogo ii hailazimishi mtu atumie kitambulisho Cha nida kusajili simu, hili shinikizo la nida linatoka wapi?

Tumemwona JPM akisajiri simu yake Airtel na hakuna afisa wa nida alikuwa pale kushuhudia hivyohivyo jk kasajiri line yake ya tigo hakuna ofisa wa nida aliyekuwepo kuhakiki taarifa zake.

Hapa napata shida na uwezo wa kufikiri wa watanzania
Sheria ya tcra utambua aina 4 za vitambulisho driving license,national id,passport na kitambulisho cha kura ambavyo navo kuvipata ni lzm uweke fingerprint,kote huko zipo fingerprint zetu Ina maana hawana database hadi watusumbue kutupangisha foleni.
 
Taarifa kamili ipo serikalini kuhusiana na zoezi hili ,kwa maana faida na hasara,yenyewe ndio yenye maamuzi ya nini kifanyike

Zingine ni mbwembwe tu hapa jukwaani
Na Elius Ndabila

Ikumbukwe kuwa kesho ni tarehe 20-1-2020 ambayo ndiyo siku ambayo TCRA wanapaswa kustisha huduma ya laini zote za simu ambazo hajisajiliwa kwa kutumia vitambulisho vya Utaifa vinavyotolewa na NIDA. Kustishwa kwa laini hizo kunakuja baada ya Mh Rais Magufuli kuongeza siku 20 ambapo mara ya kwanza ilitakiwa watu hawa wasimamishiwe huduma tangu tarehe 31-12-2019.

Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa Watanzania wengi hawana vitambulisho wala namba za NIDA hivyo namba zao hazijasajiliwa huku tatitizo kubwa likiwa vijijini. Watu wengi wanaelekeza lawama zao kwa watu wa NIDA ambao wamechelewesha zoezi hili. Inasemekana kuna watu ambao tangu mwanzoni mwa mwaka jana walichukuliwa alama na kupigwa picha lakini hadi sasa hawajui hatima ya vitambulisho vyao wala namba. Kuonyesha kuwa NIDA nao hawako serious juzi nilipigiwa simu na rafiki yangu toka Sumbawanga ambaye alitumiwa ujumbe wa NIDA lakini wa jina la mtu mwingine .

Kufungiwa kwa laini za simu hapo kesho kunaibua maswali mengi huku mgogoro mkubwa ukielekezwa wizara ya fedha. Serikali ya awamu ya tano imejipambanua sana katika adhima ya ukusanyaji wa kodi. Wakati awamu ya nne ilikuwa inakusanya bilioni 800+ kwa mwezi awamu hii ya tano hadi kufikia mwezi desemba ilikuwa inakusanya 1.7 + trillion kwa mwezi. Ongezeko hili la makusanyo ya kodi linatajwa pia kuchochewa na matumizi ya simu. Serikali kupitia wizara ya fedha wamekuwa wanakusany kodi nyingi kupitia watu kufanya miamala kwenye simu na huduma ya kununua vocha ambapo serikali inakata kodi.

Kufungiwa kwa laini za simu kutapunguza makusanyo ya kodi. Wakati Mh Mpango akiwa anafanya juhudi za kukusanya 2 trillion kwa mwezi sasa NIDA wanafanya juhudi za kumrudisha nyuma. Kufungiwa kwa laini ni bomu kubwa kwa Uchumi wa Taifa. Kutoa kuwa na crisis kubwa kwenye makusanyo ya kodi ambayo ilikuwa inapatikana kupitia makato mbalimbali kwenye simu zikiwepo VAT.

TCRA wao watatimiza wajibu wa kisheria kuzuia huduma za laini zote ambazo ni illegal lakini KIUCHUMI inamrudisha nyuma Waziri MPANGO katika vita hii ya Uchumi. Rai yangu bado ni kuendelea kuliomba serikali kutazama up ya suala hili linaloenda kuathiri Watanzania wasio na hatia kwani wenye hatia ni NIDA. Makosa ya NIDA yanaenda kuathiri mamilioni ya Watanzania wengi wasio na hatia. Kuna madhara mengi ya kuwastishia watu huduma ya laini zao nje na mambo ya KIUCHUMI.

Serikali ikiwa Kama mlezi wa watu ninadhani hili Mh Rais alitazame upya. Mwanzo nilishauri ikiwezekana NIDA waende wakajifunze NEC au kauzia mitambo ya NEC kwani Data nyingi zinafanana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna vitu unachanganya....NIDA hawasajili Sim card..wao wanatoa vitambulisho vya Taifa ambavyo hutumika katika zoezi la usajili ..hivyo kama kitambulisho unacho kama hao uliowatolea mfano, utaenda moja kwa moja kwa wakala/ofisi ya mtandao unaotumia na kusajili sim card yako
Kimsingi nida tunawafanya mbuzi wa kafara, scape goat, sheria ya tcra cap306 ya 2010 ibara ya 93 ibara ndogo ii hailazimishi mtu atumie kitambulisho Cha nida kusajili simu, hili shinikizo la nida linatoka wapi?

Tumemwona JPM akisajiri simu yake Airtel na hakuna afisa wa nida alikuwa pale kushuhudia hivyohivyo jk kasajiri line yake ya tigo hakuna ofisa wa nida aliyekuwepo kuhakiki taarifa zake.

Hapa napata shida na uwezo wa kufikiri wa watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna vitu unachanganya....NIDA hawasajili Sim card..wao wanatoa vitambulisho vya Taifa ambavyo hutumika katika zoezi la usajili ..hivyo kama kitambulisho unacho kama hao uliowatolea mfano, utaenda moja kwa moja kwa wakala/ofisi ya mtandao unaotumia na kusajili sim card yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio mie najiuliza Nani aliyewaambia watu waende nida? Mtu ana leseni ana passport ana tin bado anapanga foleni nida? Hivi Yale madarasa ya ngumbalu ya nyerere yaliishia wapi? Ujinga unarudi kwa kasi
 
Usajili unataka kitambulisho cha nida na fingerprint. Huo ndo utaratibu

Kwa sheria ipi? Tusiwafanye watanzania wote wapumbavu na hao wapumbavu wanaenda wanajitambua taratibu, social transformation huanza taratibu, ipo siku ujinga utawatoka Kama sio nyinyi watoto wenu au wajikuu wenu, hakuna nchi iliyokuwa na amani Kama Libya miaka ya sabini leo wako wapi?
 
Wanasema kipaumbele chao ni Usalama wanataka data zako zote zijulikane hili usijekuhatalisha usalama hata ikibidi hata hayo unayoongea wayadukuru wayajuwe usijifiche.Therefore usalama ni zaidi ya uchumi.eti?
 
Kimsingi nida tunawafanya mbuzi wa kafara, scape goat, sheria ya tcra cap306 ya 2010 ibara ya 93 ibara ndogo ii hailazimishi mtu atumie kitambulisho Cha nida kusajili simu, hili shinikizo la nida linatoka wapi?

Tumemwona JPM akisajiri simu yake Airtel na hakuna afisa wa nida alikuwa pale kushuhudia hivyohivyo jk kasajiri line yake ya tigo hakuna ofisa wa nida aliyekuwepo kuhakiki taarifa zake.

Hapa napata shida na uwezo wa kufikiri wa watanzania
Afisa wa NIDA anahusika vipi usajili wa laini za simu? Wao wana namba za kitambulisho cha NIDA, ndio kinatakiwa tu!
 
Unanunua bila kuulizwa post code mkuu. Na vile vile unaweza kwenda kununua used phone maduka ya mitaani na hata Sunday Market.
Hizo lyca mobile unatumia kupiga internal call or outside the country ??
Na hiyo handset unayotumia yenye imei number nayo uliinunua cash bila kuulizwa jina na post code??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unanunua bila kuulizwa post code mkuu. Na vile vile unaweza kwenda kununua used phone maduka ya mitaani na hata Sunday Market.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unanunulia wapi kwa wale wanayo uza used??
Na wanayo uza used ni kwamba ukitoka msala atakaye shikwa ni yeye aliywnunua kwanza, labda utoke ushahidi mwingine kuonyesha yeye sio muhusika bali mtu mwingine kwa kutumia cctv ambazo wenzetu wanazo sisi hatuna, sasa sijui ungependa kusema tunawaharibia watu kazi zao
 
Wacha Mkuu Tabutupu huyo Jiwe ajidanganye

Afunge hizo line za simu, aanze kuona hiyo "impact" yake
Hakuna kitu wala usimtishe, wasiojitambua ndio wamefungiwa line zao, kwanza unachotakiwa kujua waliofungiwa karibu wote ni tegemezi na simu zao ni za umbea tu, hakuna mwenye simu alikuwa anaitumia kwa mambo ya maana akafungiwa line yake
 
Kwani laini zimeshafungwa?!..hii yangu mbona inatamba tu mwanzo mwisho..
 
Back
Top Bottom