Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,072
Daddy is coming!???
Meneja wa WCB, Sallam SK amesema suala la nyimbo 2 za Diamond kufungiwa na BASATA wiki iliyopita hawezi kuliongolea kwa kuwa tayari wamelifikisha kwa Mlezi wa Lebo hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda.
Sallam anasema Makonda huwa ndiye anakagua nyimbo za kundi hilo kabla hazijatoka ili kuona kama zinafaa kimaadili au la, hivyo kama hizo zilizofungiwa zilitoka, maana yake alizipitisha kwa kuwa hazina tatizo..
Inadaiwa kuwa, uamuzi wa kufungia nyimbo za wasanii ambao kwa kiasi kikubwa unaratibiwa na Clouds MG, ulilenga kudhoofisha jitihada za mwanamuziki Diamond Platnumz na kuhujumu album yake inayotarajiwa kuzinduliwa ndani ya mwezi Machi mwaka huu.
Nyepesi nyepesi zinadai kwamba kuna viongozi wa BASATA 'wanatumika' katika mpango huo na N/Waziri wa Sanaa, Juliana Shonza kuingizwa mkenge pasipo kujua.. Na ndio maana hata nyimbo zilizofungiwa zilizua mjadala mkali kutoka kwa wananchi kwa kile kilichoonekana kuwa zimefungiwa kwa kukurupuka!
Kwa wafuatiliaji wa mambo ya burudani hapa nchini watafahamu kuwa kumekuwa na vita baridi katika tasnia hiyo baina ya wasanii (baadhi) na vyombo vya habari kwa sababu za kimaslahi.
Je, Makonda atamudu kuzima fitna hizi ikizingatiwa kuwa yeye ana nguvu za kimamlaka na anahusika kimaslahi?