Kufungiwa nyimbo 2 za Diamond: WCB waishtaki BASATA kwa Makonda..

Kufungiwa nyimbo 2 za Diamond: WCB waishtaki BASATA kwa Makonda..

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Daddy is coming!???

Meneja wa WCB, Sallam SK amesema suala la nyimbo 2 za Diamond kufungiwa na BASATA wiki iliyopita hawezi kuliongolea kwa kuwa tayari wamelifikisha kwa Mlezi wa Lebo hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda.

Sallam anasema Makonda huwa ndiye anakagua nyimbo za kundi hilo kabla hazijatoka ili kuona kama zinafaa kimaadili au la, hivyo kama hizo zilizofungiwa zilitoka, maana yake alizipitisha kwa kuwa hazina tatizo..

Inadaiwa kuwa, uamuzi wa kufungia nyimbo za wasanii ambao kwa kiasi kikubwa unaratibiwa na Clouds MG, ulilenga kudhoofisha jitihada za mwanamuziki Diamond Platnumz na kuhujumu album yake inayotarajiwa kuzinduliwa ndani ya mwezi Machi mwaka huu.

Nyepesi nyepesi zinadai kwamba kuna viongozi wa BASATA 'wanatumika' katika mpango huo na N/Waziri wa Sanaa, Juliana Shonza kuingizwa mkenge pasipo kujua.. Na ndio maana hata nyimbo zilizofungiwa zilizua mjadala mkali kutoka kwa wananchi kwa kile kilichoonekana kuwa zimefungiwa kwa kukurupuka!

Kwa wafuatiliaji wa mambo ya burudani hapa nchini watafahamu kuwa kumekuwa na vita baridi katika tasnia hiyo baina ya wasanii (baadhi) na vyombo vya habari kwa sababu za kimaslahi.

Je, Makonda atamudu kuzima fitna hizi ikizingatiwa kuwa yeye ana nguvu za kimamlaka na anahusika kimaslahi?
 
BASATA is shit. Sijui nani aliunda huu upuuzi. Wao wanamake headlines kwa kufunga kazi za watu tu. Hakuna kingine wanachofanya.
Ati maadili ya Tanzania. Hehe bullshit Tanzania kuna maadili yapi?
 
e3e0501cd974bc077719ebfeabf1b4ad.jpg
 
Ukitaka kuona tupu za kuku wee subiri tu upepo uje utaziona bila tatizo.

Ni hatari sana.
 
Mi bado sijaelewa, nyimbo zinapigwa marufuku kivipi, kuziangalia YouTube au kupigwa kwenye kumbi za burudani?
 
Makonda akitaka zitafunguliwa au anaweza akavunga tu

The power of dady to be President
 
Mi bado sijaelewa, nyimbo zinapigwa marufuku kivipi, kuziangalia YouTube au kupigwa kwenye kumbi za burudani?
Hazirusiw kuskika na kuoneshwa kwenye media
Km ipo kwenye Playlist yako home piga utakavyo
 
BASATA is shit. Sijui nani aliunda huu upuuzi. Wao wanamake headlines kwa kufunga kazi za watu tu. Hakuna kingine wanachofanya.
Ati maadili ya Tanzania. Hehe bullshit Tanzania kuna maadili yapi?
maadili truly ya mtanzania ni kukaaa uchi hawajuwe ao
 
basata wanatumika kuishusha wcb lakini awatoweza wcb wanatengeneza mfumo wao
 
Hivi nyimbo kama hainaga ushemeji na mwanaume mashine zinamaadili gani ule wimbo wa jux ñdio waliuwonea kabisa
 
Ama kweli ukiamua kuashetani usiache na ibada zao,jaman ile video ya nyimbo ya mond na Rick rose hawaoni kama inautovu wa nidhamu.
Mbona video za kina migos bado zinapigwa kwenye media za Tz na ndo zinaongoza kwa kuvunja maadili
 
Back
Top Bottom