KUFUNGIWA REDIO IMAAN NA NYINGINEZO: haki haijatendwa!

KUFUNGIWA REDIO IMAAN NA NYINGINEZO: haki haijatendwa!

scramble

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
1,593
Reaction score
257
Tumo katika nchi inayofuata sheria. nchi yoyote ile lazima iongozwe kwa kufuata sheria. TCRA ni chombo kinacho simamia vyombo vya habari vya kielektroniki hasa redio na televisheni. kina mamlaka ya kuonya au hata kufungia chombo cha habari kinacho kiuka maadili ya utangazaji.

redio imaan ya morogoro na kwa neema fm ya mwanza zimefungiwa na kamati ya maudhui (content committee) iliyo chini ya TCRA. clouds fm ya dsm imeonywa na kutozwa faini ya 5,000,000/=. sababu iliyo tolewa ya kuifungia redio imaan ni kuhamasisha waislamu wasishiriki katika sensa ya mwezi agosti mwaka jana. kuhusu kwa neema fm imeelezwa kuwa imehamasiha kwa zaidi ya miezi 4 wakristo wasile nyama iliyochinjwa na waislamu hadi uhamasishaji wao ukasababisha watu kuuana!. clouds fm inasemekana walicheza clip ya askofu wa marekani aliekua akiunga mkono ushoga. watangazaji waliiunga mkono kauli yake na kusema kuwa mashoga waruhusiwe. ni haki yao.

lengo lango ni kuizungumzia redio imaan huku nikiakisi redio nyingine mbili. ni takriban miezi 7 tangu sensa ya watu ifanyike. kwa mujibu wa bbc jana jioni, mkurugenzi wa redio imaan alipohojiwa alisema kuwa redio yake ilikua ikiripoti maoni ya watu kuhusu kipengele cha dini kuwekwa kwenye dodosa za sensa. alisema kuwa japo kila mtu ana uhuru wa kuisikiliza redio imaan lkn imewalenga sana waislamu. waislamu ndiyo wenye redio na michango yao ndiyo inaifanya redio iwepo. alisema kuwa waislamu walijenga hoja kuwa wanabaguliwa katika mambo mengi hasa ajira serikalini kwa madai kuwa ni wachache. wao wanaamini ni wengi. walitaka kwenye dodosa kiwekwe kipengele cha dini ili ukweli ujulikane kama zifanyavyo nchi nyingine. alisema kuwa mada ilianzishwa na watu wakawa wanapiga simu kuchangia mada hiyo.

aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita, hajawahi kupokea barua kutoka TCRA ikimuonya kuhusu mada ya sensa! inakuaje afungiwe ghafla bila hata karipio!? alisema vipindi vya redio imaan vimekua vikiendeshwa kwa ueledi na kwa kuzingatia taaluma ya utangazaji. redio imaan haijawahi kuhamasisha mtafaruku, kuhatarisha amani na kusababisha vifo vya raia. imekua daima ikieleza na kuripoti ukweli kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia hapa nchini.

MY TAKE:
ukiangalia kosa la kwa neema fm, utagundua kuwa uhamasishaji ulikua wa wazi na hadi ulikaidi amri ya serikali ya kuomba uchinjaji uendelee huku suluhu ikitafutwa. redio ilipuuzia agizo la serikali na kuendelea na uhamasishaji bila ya kuangalia madhara yake. matokeo yake watu wakauana! inakuaje clouds fm inayo shabikia ushoga ipewe karipio na kutozwa faini lakini redio imaan inafungiwa! watu kudai haki ya kutambuliwa katika dodosa za sensa na wanaohamasisha ushoga ni yupi anaekiuka maadili na katiba ya nchi?

kazi kwenu wadau kutoa majibu yenye hoja zilizo kwenda shule!

naomba kuwasilisha!
 
Hapo naona umeitetea redio Imani tu. Kimsingi ilitakiwa iwe imefungiwa hata kabla ya mambo ya sensa hayajaanza kuwa public

jenga hoja mkuu. kama umewahi isikiliza taja kitu kilicho kukera ambacho redio imaan ilikitangaza. toa mifano. kuho ndiyo kujenga hoja
 
Kuna siku nilisikiliza nilifaidika sana na Mawaidha, ila kuna siku nyingine sikufurahishwa na maudhui ya yale waliyokua wanayasema na sijaisikiliza mpaka leo. Hata wewe unajua ila unataka kufanya watu wasumbuke tu.:smile-big:

Hata kabla ya sensa, wamekuwa wakilinganisha idadi ya watumishi waliopo kwenye taasisi za serikali kuwa hapa pana waisilamu wachache kuliko wakristu. Sasa huo ni uchochezi kwamba kuna mtu au watu walikuwa wanatoa ajira kwa upendeleo, jambo ambalo ukweli wake ni kwamba ajira zinatolewa kwa qualifications alizonazo mtu.
 
huu uswahili. nimeandika juu kuwa nasubiri mwenye ushahidi wa ukiukwaji wa maadili autaje. na kuhusu hilo la sensa unasemaje? jadili kama upo JF siyo kijiweni au klabuni tafadhali. tumia kichwa!
 
Hapo naona umeitetea redio Imani tu. Kimsingi ilitakiwa iwe imefungiwa hata kabla ya mambo ya sensa hayajaanza kuwa public

Ahsante mkuu kwa kuliona hili. Radio Imana na Neema zimehukumiwa kwa waliyotendwa, si kwa dhana!! Sote tumesikia redio hizi zikitenda yanayotuhumiwa dhidi yao. Demokrasia isiyo na mipaka ni uendawazimu!!!

Ni kweli pia wakati Radio Neema inashutumiwa kwa issue ya kuzugumzia uchinjaji, Radio Iman imezungumzia mengi ikiwa ni pamoja na "mfumo kristu", Baraza la Mitihani, dhana ya waislamu kuonewa, nk. Ajenda nyingi zimekuwa ni kuonesha waislamu wanaathiriwa na wasiokuwa waislamu na wasiokuwa waislamu wanapaswa kutoa nafasi kwa waislamu kutekeleza matakwa yao ya kidini bila kujali mahitaji ya kidini ya wasiokuwa waislamu.

Kwangu mimi, hukumu hii imelenga kuadhibu watu wanaovunja misingi ya haki ya utaifa usiokuwa na mipaka ya kidini!! Taifa hili si linalofikiria maswala ya kidini tu. Linapaswa kuwa linalofikiria "co-existence" ya watu kiuchumi, kisiasa, kijamii na kadhalika!!

Tunalalamikia kupotezwa kwa misingi ya utaifa, tusiwe wanafiki na kuona sasa kila mtu ana haki ya kidemokrasia ya kufanya chochote atakacho kwa msingi wa dini!!
 
Al shaabab mmeanza, yaani hamkosi pakuanzia. TUMEWACHOKA BHANA!
 
Radio iman nilitegemea ingefungiwa tuu, wana mada ngumu sana katika masuala ya kuongelea dini nyingine. mm naona wakifunguliwa waweke muda mwingi kusoma kitabu chao cha dini na sio kuwazungumzia majirani za wa dini nyingine. naomba msiandamane kwa kweli, tulieni mjipange upya, bado mna muda wa kujipanga na sipati picha kama radio neema ya mwanza isingefungiwa ungekuta maandamano kila kona. Sasa kwa sasa mtu anaweza kupima uvumiivu wa hizi dini mbili..haihitaji tuition kujua kitakachoendelea.
 
Hata kabla ya sensa, wamekuwa wakilinganisha idadi ya watumishi waliopo kwenye taasisi za serikali kuwa hapa pana waisilamu wachache kuliko wakristu. Sasa huo ni uchochezi kwamba kuna mtu au watu walikuwa wanatoa ajira kwa upendeleo, jambo ambalo ukweli wake ni kwamba ajira zinatolewa kwa qualifications alizonazo mtu.
acha uwongo wewe
 
.... mkurugenzi wa redio imaan alipohojiwa alisema kuwa redio yake ilikua ikiripoti maoni ya watu kuhusu kipengele cha dini kuwekwa kwenye dodosa za sensa....
Kwani sheria inasemaje? Radio ina uhuru wa kuripoti chochote tu? Hakuna mipaka?
 
redio za namna hiyo zifungiwe maisha, sioni sababu ya kufungiwa kwa muda
 
Hata kabla ya sensa, wamekuwa wakilinganisha idadi ya watumishi waliopo kwenye taasisi za serikali kuwa hapa pana waisilamu wachache kuliko wakristu. Sasa huo ni uchochezi kwamba kuna mtu au watu walikuwa wanatoa ajira kwa upendeleo, jambo ambalo ukweli wake ni kwamba ajira zinatolewa kwa qualifications alizonazo mtu.[/Q hii redio imefaulu kupanda mbegu ya chuki miongoni mwa wtz adhabu iliyotolewa haitoshi
 
Ahsante mkuu kwa kuliona hili. Radio Imana na Neema zimehukumiwa kwa waliyotendwa, si kwa dhana!! Sote tumesikia redio hizi zikitenda yanayotuhumiwa dhidi yao. Demokrasia isiyo na mipaka ni uendawazimu!!!

Ni kweli pia wakati Radio Neema inashutumiwa kwa issue ya kuzugumzia uchinjaji, Radio Iman imezungumzia mengi ikiwa ni pamoja na "mfumo kristu", Baraza la Mitihani, dhana ya waislamu kuonewa, nk. Ajenda nyingi zimekuwa ni kuonesha waislamu wanaathiriwa na wasiokuwa waislamu na wasiokuwa waislamu wanapaswa kutoa nafasi kwa waislamu kutekeleza matakwa yao ya kidini bila kujali mahitaji ya kidini ya wasiokuwa waislamu.

Kwangu mimi, hukumu hii imelenga kuadhibu watu wanaovunja misingi ya haki ya utaifa usiokuwa na mipaka ya kidini!! Taifa hili si linalofikiria maswala ya kidini tu. Linapaswa kuwa linalofikiria "co-existence" ya watu kiuchumi, kisiasa, kijamii na kadhalika!!

Tunalalamikia kupotezwa kwa misingi ya utaifa, tusiwe wanafiki na kuona sasa kila mtu ana haki ya kidemokrasia ya kufanya chochote atakacho kwa msingi wa dini!!

kuna ubaya wowote kuzungumzia mfumo uwe wa kiislamu au kikristo? mtu kusema anaonewa ni kosa!? waislamu walichunguza na kuona kuwa baraza la mitihani lilifelisha watoto wa kiislamu makusudi katika mtihani wa islamic knowledge. baraza lilikiri na kusema lilikua kosa la kompyuta. pana madai kuwa katika bodi ya NECTA na wana kamati hakuna muislamu hata mmoja. redio ya kiislamu kuongelea suala hilo ni majungu / kosa!?

kwa nini kwa mwanasiasa kuchunguza jambo ni sahihi lakini kwa redio ya dini kuchunguza tatizo linalo athiri dini husika kwa hoja kwa liwe kosa?

naomba unijibu kuhusu madai yaliyotolewa dhidi ya baraza la mitihani. je madai haya yanahatarisha amani?
 
RADIO Imaan, elimu bila mipaka huu msemo sii sahii lazima elimu iwe na mipaka huwezi fundisha mambo ya ndoa radioni kama wanavyofanya, unamfundisha nani?? IFUNGWE.. IFUNGWE. ELIMU LAZIMA IWE NA MIPAKA
 
Ahsante mkuu kwa kuliona hili. Radio Imana na Neema zimehukumiwa kwa waliyotendwa, si kwa dhana!! Sote tumesikia redio hizi zikitenda yanayotuhumiwa dhidi yao. Demokrasia isiyo na mipaka ni uendawazimu!!!

Ni kweli pia wakati Radio Neema inashutumiwa kwa issue ya kuzugumzia uchinjaji, Radio Iman imezungumzia mengi ikiwa ni pamoja na "mfumo kristu", Baraza la Mitihani, dhana ya waislamu kuonewa, nk. Ajenda nyingi zimekuwa ni kuonesha waislamu wanaathiriwa na wasiokuwa waislamu na wasiokuwa waislamu wanapaswa kutoa nafasi kwa waislamu kutekeleza matakwa yao ya kidini bila kujali mahitaji ya kidini ya wasiokuwa waislamu.

Kwangu mimi, hukumu hii imelenga kuadhibu watu wanaovunja misingi ya haki ya utaifa usiokuwa na mipaka ya kidini!! Taifa hili si linalofikiria maswala ya kidini tu. Linapaswa kuwa linalofikiria "co-existence" ya watu kiuchumi, kisiasa, kijamii na kadhalika!!

Tunalalamikia kupotezwa kwa misingi ya utaifa, tusiwe wanafiki na kuona sasa kila mtu ana haki ya kidemokrasia ya kufanya chochote atakacho kwa msingi wa dini!!
kila mtu ana haki ya kuabudu. Amna mwenye haki ya kumzuia mwengine kufanya ibada ikiwa anafata kitabu cha imaan yake
 
Back
Top Bottom