scramble
JF-Expert Member
- Nov 29, 2012
- 1,593
- 257
Tumo katika nchi inayofuata sheria. nchi yoyote ile lazima iongozwe kwa kufuata sheria. TCRA ni chombo kinacho simamia vyombo vya habari vya kielektroniki hasa redio na televisheni. kina mamlaka ya kuonya au hata kufungia chombo cha habari kinacho kiuka maadili ya utangazaji.
redio imaan ya morogoro na kwa neema fm ya mwanza zimefungiwa na kamati ya maudhui (content committee) iliyo chini ya TCRA. clouds fm ya dsm imeonywa na kutozwa faini ya 5,000,000/=. sababu iliyo tolewa ya kuifungia redio imaan ni kuhamasisha waislamu wasishiriki katika sensa ya mwezi agosti mwaka jana. kuhusu kwa neema fm imeelezwa kuwa imehamasiha kwa zaidi ya miezi 4 wakristo wasile nyama iliyochinjwa na waislamu hadi uhamasishaji wao ukasababisha watu kuuana!. clouds fm inasemekana walicheza clip ya askofu wa marekani aliekua akiunga mkono ushoga. watangazaji waliiunga mkono kauli yake na kusema kuwa mashoga waruhusiwe. ni haki yao.
lengo lango ni kuizungumzia redio imaan huku nikiakisi redio nyingine mbili. ni takriban miezi 7 tangu sensa ya watu ifanyike. kwa mujibu wa bbc jana jioni, mkurugenzi wa redio imaan alipohojiwa alisema kuwa redio yake ilikua ikiripoti maoni ya watu kuhusu kipengele cha dini kuwekwa kwenye dodosa za sensa. alisema kuwa japo kila mtu ana uhuru wa kuisikiliza redio imaan lkn imewalenga sana waislamu. waislamu ndiyo wenye redio na michango yao ndiyo inaifanya redio iwepo. alisema kuwa waislamu walijenga hoja kuwa wanabaguliwa katika mambo mengi hasa ajira serikalini kwa madai kuwa ni wachache. wao wanaamini ni wengi. walitaka kwenye dodosa kiwekwe kipengele cha dini ili ukweli ujulikane kama zifanyavyo nchi nyingine. alisema kuwa mada ilianzishwa na watu wakawa wanapiga simu kuchangia mada hiyo.
aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita, hajawahi kupokea barua kutoka TCRA ikimuonya kuhusu mada ya sensa! inakuaje afungiwe ghafla bila hata karipio!? alisema vipindi vya redio imaan vimekua vikiendeshwa kwa ueledi na kwa kuzingatia taaluma ya utangazaji. redio imaan haijawahi kuhamasisha mtafaruku, kuhatarisha amani na kusababisha vifo vya raia. imekua daima ikieleza na kuripoti ukweli kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia hapa nchini.
MY TAKE:
ukiangalia kosa la kwa neema fm, utagundua kuwa uhamasishaji ulikua wa wazi na hadi ulikaidi amri ya serikali ya kuomba uchinjaji uendelee huku suluhu ikitafutwa. redio ilipuuzia agizo la serikali na kuendelea na uhamasishaji bila ya kuangalia madhara yake. matokeo yake watu wakauana! inakuaje clouds fm inayo shabikia ushoga ipewe karipio na kutozwa faini lakini redio imaan inafungiwa! watu kudai haki ya kutambuliwa katika dodosa za sensa na wanaohamasisha ushoga ni yupi anaekiuka maadili na katiba ya nchi?
kazi kwenu wadau kutoa majibu yenye hoja zilizo kwenda shule!
naomba kuwasilisha!