kuna ubaya wowote kuzungumzia mfumo uwe wa kiislamu au kikristo? mtu kusema anaonewa ni kosa!? waislamu walichunguza na kuona kuwa baraza la mitihani lilifelisha watoto wa kiislamu makusudi katika mtihani wa islamic knowledge. baraza lilikiri na kusema lilikua kosa la kompyuta. pana madai kuwa katika bodi ya NECTA na wana kamati hakuna muislamu hata mmoja. redio ya kiislamu kuongelea suala hilo ni majungu / kosa!?
kwa nini kwa mwanasiasa kuchunguza jambo ni sahihi lakini kwa redio ya dini kuchunguza tatizo linalo athiri dini husika kwa hoja kwa liwe kosa?
naomba unijibu kuhusu madai yaliyotolewa dhidi ya baraza la mitihani. je madai haya yanahatarisha amani?
Sidhani kama ni sahihi mahali kusema kwamba mahali ambapo hakuna Muislam au hakuna mkristu hata mmoja anayefanya kazi hapo basi jamii iliyokosa muumini hapo hawatotendewa haki,tujaribu kuwa chanya naenda hospitali ya Bakwata ambayo wafanyakazi wake wote ni waislamu hakuna mkristu then niseme sitotibiwa kwa sababu mimi ni mkristu?Au sitopewa nafasi ya shule kama mtoto wangu ni mkristu na shule ni ya waislamu?Nadhani kama ni seminary naweza nisiulize maswali mengi lakini kama ni shule ya kawaida ikawa na ubaguzi hapo nitajiuliza,vinginevyo siwezi kuwa na mawazo hasi.
Hilo ninakukatalia kwa asilimia mia,watanzania tuwe na mawazo chanya,wamekosea ni makosa ya kibinadamu lakini tusiweke sababu za kwa kuwa hakuna mfanyakazi wa dini ya kiislamu ndio sababu,siyo sahihi hata kidogo.
Na kwa upande mwingine sidhani kama Scramble uko sahihi pia kusema baraza la mitihani halina hata muislamu mmoja sidhani kama ni kweli,utakuwa unaupotosha umma.
Kwa wakristu pia sifikiri kwa kuwa Rais ni muislam,makamu muislam,Judge mkuu ni muislamu,IGP muislamu na blahblah halafu wakristu waseme sababu hawa ni waislamu wote then wakristu hawatendei haki siyo kweli na sidhani kama kuna ukweli ndani yake.
Kama Redio imekosea kwa kukiuka sheria za nchi iache ijitetee yenyewe na ikiri makosa yake na kutokurudia,tusiweke udini kwenye sheria za nchi,nchi ni ya kwetu sote na wote tuna haki ya kuishi nakuabudu tutakavyo ili mradi tusivunje sheria.
Sheria zetu hazifuati dini yoyote basi sote tuziheshimu,hakuna sababu ya mkristu kumtukna,kumdhihaki au kumkashifu muislamu kwa sababu ya imani yake na pia kwa upande wa waislamu hawana haki ya kutukana,kudhalilisha wala kukashifu ukristu nchi ni yetu sote.
Ambaye anaona sheria za Tanzania hazimtendei haki na angependa kufuata sharia basi aende kwenye nchi wanayofuata misingi hiyo, vivyo hivyo kwa wanaotaka nchi yetu iendeshwe kwa mlengo wa dini ya kikristu.