Kufungua Bucha la samaki Dar kutoka Ziwa Victoria

Kufungua Bucha la samaki Dar kutoka Ziwa Victoria

Majority wanakula nyama,kwa maisha ya Sasa samaki inaangaliwa kama chakula Cha anasa....

Nyama inapatikana hapa hapa so unaipata fresh na unahakika ya kuimaliza, tofauti na samaki ,inatoka mbali na utokaji wake ni slow kidogo .

UTUNZAJI,ukipata Mtu anayekuletea kutoka Mwanza asipotunza vizuri kwenye 0-2degree kabla ya kusafirisha unaweza pokea mzigo hauna ubora,nadhani unajua ukipataa mzigo mbovu,itabidi uuze Kwa bei ya hasara.,hapa wateja ni wafanyabiashara wa kukaanga samaki mara nyingi Huwa wanafurahia hii sana...kuwauzia wateja wa kula nyumbani Huwa changamoto sana....

KUTAPELIWA,unaweza kuwa na Mtu anakuletea samaki kutoka Mwanza unamtumia pesa ya kutosha karibu mwaka mzima,ila siku isiyo na jina anaweza potea bila taarifa hapo umetuma 6M zako,usimpate tena

Kifupi,samaki inacomplication ila ikikubali inakutoa...
Asante sana
 
Ndiyo; kwani kodi hutokana na mapato. Ukianzisha biashara lakini kwenye quarter ya kwanza ukapata hasara, hutalipa kodi katika quarter hiyo na utakata hiyo hasara kutoka kwenye faida ya quarter ijayo kabla hujalipa kodi
Sijakuelewa ,samahani unaweza kuiwek Kwa Urahisi kidogo
 
Sijakuelewa ,samahani unaweza kuiwek Kwa Urahisi kidogo
Hiyo iko katika lugha rahisi sana, ni kitu gani hakieleweki. Wenzetu hulipa kodi kila baada ya miezi mitatu (robo mwaka au quarter).

Ngoja nijaribu: Kama robo ya kwanza uliwekeza Shilingi 100, lakini mauzo yako yote yakaishia kurudisha Sh 80 tu, ina maana umepata hasara ya Sh 20 kwenye robo hiyo, kwa hiyo hutalipa kodi yoyote. Sasa ukiongezea Sh 40 zaidi kwenye mtaji na kufikisha sh 120 ukaziwekeza tena halafu mauzo yote yakaleta Sh200, ina maana quarter ya pili ulipata faida ya Sh 80. Sasa kwa vile kwenye quarter ya kwanza ulikuwa na hasara ya Sh 20, basi utaikata hiyo hasara ya Sh 20 kutoka kwenye faida uliyopata ndani ya quarter ya pili na kubaki na faida ya Sh 60 tu ambazo ndizo utakazolipia kodi.

Sijui mfano huo umeeleweka?
 
Tanzania ina mambo ya ajabu kweli; yaani unalipa kodi kabla hujatengeneza hela!! Sijui hela za kulipa kodi hiyo hutegenmewa zitoke wapi iwapo hujaanza biashara
Alimaanisha pango la sehemu ya kuuzia naamini.
 
Watu wa Dar mnatutapeli ningeweza kukupa mzigo ila ndio hivyo tena
 
Kwa hapa Dar, je naweza kufungua butcher la samaki wabichi sato, sangara n.K kutoka Mwanza ? Kwa mtaji wa 2 milioni.

Kwa wazoefu na soko la SAMAKI na usafiri pia

Kutoka MWANZA to Dar hiyo pesa inatosha ??

Naomba mnielekeze
Tafuta wateja, uuze kwa oda (online business) mtaji ukikua unafungua bucha.

Usikate tamaa, hiyo inatosha sana kama utakuwa mbunifu.
 
Kwahyo niwanunue alafu niwahifadh nyumbn,nitafute wateja online okok
Nunua jokofu uwe nalo halafu kabla ya kununua samaki, ingia facebook fungua page ya biashara ulipie kama elfu 50 ya matangazo kisha uweke matangazo ukijinadi kuwa unauza samaki. Uweke details zote muhimu kwa ajili ya oda na delivery. Kisha ingia kwa platform zingine kama wasap hiwezi kosa watu hata wa karibu wa kuwauzia, kisha kusanya oda uweke na delivery hadi kwa mteja. Ukipata oda unafanya kuagiza unapakia kwa ndoo inaruka na ndege dk chache inakufikia ikiwa fresh unamuuzia mteja.

Facebook watarusha hilo tangazo kwa watu ambao ni potential hasa wale taarifa zao zinazoendana na kuulizia samaki, Ukiwa unafunga mzigo wa mteja upige na short video halafu unairusha kwa page yako hii itasaidia watu wakuamini.
 
Nakushauri utafute kwanza freezer la size ya kutosha. Halafu unaweza liweka hata nyumbani kwako unapoishi kama haupo Dar then tafuta nyumba ya bei nafuu hata ya kodi ya 60 au 80. Lipia miezi sita. Weka samaki kwenye freezer anza kuuzia wale wauza samaki mabuchani na majirani zako mdogo mdogo hadi mzigo upungue na kuisha.

Fanya hivyo hadi uweze kukuza mtaji na unaweza kwenda kuomba mkopo wa kukuwezesha kupata frame sehemu nzuri na kuweza kuhudumia wateja kwa urahisi zaidi.

Ila ukisema uanze na hiyo mil 2 kufanya biashara hautatoboa mzee.
 
Majority wanakula nyama,kwa maisha ya Sasa samaki inaangaliwa kama chakula Cha anasa....

Nyama inapatikana hapa hapa so unaipata fresh na unahakika ya kuimaliza, tofauti na samaki ,inatoka mbali na utokaji wake ni slow kidogo .

UTUNZAJI,ukipata Mtu anayekuletea kutoka Mwanza asipotunza vizuri kwenye 0-2degree kabla ya kusafirisha unaweza pokea mzigo hauna ubora,nadhani unajua ukipataa mzigo mbovu,itabidi uuze Kwa bei ya hasara.,hapa wateja ni wafanyabiashara wa kukaanga samaki mara nyingi Huwa wanafurahia hii sana...kuwauzia wateja wa kula nyumbani Huwa changamoto sana....

KUTAPELIWA,unaweza kuwa na Mtu anakuletea samaki kutoka Mwanza unamtumia pesa ya kutosha karibu mwaka mzima,ila siku isiyo na jina anaweza potea bila taarifa hapo umetuma 6M zako,usimpate tena

Kifupi,samaki inacomplication ila ikikubali inakutoa...
Budda20
 
Back
Top Bottom