Kufungua kesi ya Utapeli wa kiroho dhidi ya ndugu Boniphace Mwamposa

Kufungua kesi ya Utapeli wa kiroho dhidi ya ndugu Boniphace Mwamposa

Nimekusudia kufungua kesi ya utapeli na ulaghai wa kiroho dhidi ya anayejiita mtume Boniphace Mwamposa. Nina ushahidi wakutosha na mashahidi kadhaa ambao ni waumimi wake walio tapeliwa kwa njia hiyo hiyo.

Je, kisheria utapeli wa kiroho unatambulika ikiwa kuna ushahidi?
Utashindwa hiyo kesi utasikilizwa halafu itawekwa kapuni, huyo mwampsa alifanya Ibada wakafa watu ishirini palepale, hata kama yeye hakuhusika angeitwa na uchunguzi ungefanyika kama lile gorofa pale kariakoo ilivyokuwa.
Badala yake jumapili iliyofuata alikuwa kanisani kwake kama kawaida na hilo jambo hakuligusia mpaka leo. Ina maana wajenzi huru wana mtandao mkubwa sana kila mahali. Kama unafuatilia TB joshua ghorofa lake liliuwa watu kibao. Kilichofuata Rais wa Nigeria alienda kwa TB joshua kumpa pole na ilaishia hapo.

Mi nakushauri achana nae,utakufa unajiona.

Yaani ile kumwamini na kuingia pale kuomba msaada wake tayari wewe huna " power" ya kupambana nae.
Wale sio matapeli tu ni wachawi, wajenzi huru wa digrii au kiwango cha juu mfano wa TB Joshua. Kaa mbali.

Sisi walokole tumejitahidi kuwaelimisha kuhusu hawa watu mnatuona wajinga. Sasa angalia umechsnganyikiwa unakuja kuomba msaada JF.

Unachoweza wewe ni kutoa stori yote hapa ili watu wengine wasinaswe. Kabla ya hapo tubu dhambi na umkubali kumfuata Yesu kama sis. Ili uwe na ulinzi kamili toka kwa Mungu mwenyewe. Usiende tena kwa Mrume na Nabii yeyote . ShortCut zinawaponza. Sisi wenzako tunatembea na kutafuta hela tukilindwa na Yesu huku tunajua kuna wafanyabiashara wenzetu au majirani wanategemea uchawi, majini, chuma ulete n.k. kuna gharama za kiroho kumfuata Yezu na kupata ulinzi,ikiwa ni pamoja na kejeli ns dharau.
 
Mtu anamuomnbea raisi na wakuu wa mikoa mpaka hao majaji halafu ukamshtaki, bwanamdogo hujipendi.
 
Back
Top Bottom