Kufungua vyuo ni kuwajaribia vijana wetu na kuwamaliza waalimu vyuoni

Kufungua vyuo ni kuwajaribia vijana wetu na kuwamaliza waalimu vyuoni

Akili mbovu za namna hii mnazitoa wapi kuanzisha uzi.....? Sisi sote tunashukuru kuwa sasa hatutapoteza mwaka wa masomo....!! Korona ipo tuhimizane kujihadhari nayo....yaani nawa mikono , Barakoa ,sanitaiza, observe distance. Wajameni korona sio ebola...tusipotezeane malengo kwa mitazamo ya kisiasa.
 
Vijana ndio wanajeshi wetu nawasihi wasirudi nyumaa, himahimaaaa!!!!
 
Kama kweli Rais kadhamiria kufungua vyuo bila kuangalia hali halisi ya ugonjwa huu, basi waalimu vyuoni jiandaeni. Taarifa tunazofahamu ni kwamba Vijana wanapambana na ugonjwa huu vizuri zaidi kuliko wazee.

Madarasa ya vyuo vyetu ni kama kambi za wakimbizi. wanafunzi hujaa hadi pomoni na wengine hukosa kabisa nafasi ya kukaa. Mgonjwa mmoja anatosha kuambukiza darsa zima kwa siku moja tu.

Waalimu wa vyuo waliowengi wako kwenye umri hatarishi kwa corona na hawa ndo watakaokutana na vijana ambao sasa watatoka majumbani kwao na kusafiri nchi nzima. Nionavyo waalimu jiandaeni kupigwa na corona.

Hili kidogo linasikitisha maana wanasiasa kule Bungeni na hata maofisini na huko ikulu, wanaogopa mikusanyiko lakini wako tayari kuwajaribia vijana wetu na wataalamu wetu kuanza kuchanganyikana kwenye madarasa ambayo hukusanyika kuliko daladala.
Kama wanaona umri umeenda wastaafu tuuuu
 
Korea kusini baada ya kuzifungua shule zao hatimae wamezifunga tena baada ya wanafunzi kuambukizana tena kwa kasi.
 
Back
Top Bottom