Kufungua vyuo ni kuwajaribia vijana wetu na kuwamaliza waalimu vyuoni

Kufungua vyuo ni kuwajaribia vijana wetu na kuwamaliza waalimu vyuoni

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,319
Reaction score
3,128
Kama kweli Rais kadhamiria kufungua vyuo bila kuangalia hali halisi ya ugonjwa huu, basi waalimu vyuoni jiandaeni. Taarifa tunazofahamu ni kwamba Vijana wanapambana na ugonjwa huu vizuri zaidi kuliko wazee.

Madarasa ya vyuo vyetu ni kama kambi za wakimbizi. wanafunzi hujaa hadi pomoni na wengine hukosa kabisa nafasi ya kukaa. Mgonjwa mmoja anatosha kuambukiza darsa zima kwa siku moja tu.

Waalimu wa vyuo waliowengi wako kwenye umri hatarishi kwa corona na hawa ndo watakaokutana na vijana ambao sasa watatoka majumbani kwao na kusafiri nchi nzima. Nionavyo waalimu jiandaeni kupigwa na corona.

Hili kidogo linasikitisha maana wanasiasa kule Bungeni na hata maofisini na huko ikulu, wanaogopa mikusanyiko lakini wako tayari kuwajaribia vijana wetu na wataalamu wetu kuanza kuchanganyikana kwenye madarasa ambayo hukusanyika kuliko daladala.
 
Hali halisi ni ipi??


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama kweli Rais kadhamilia kufungua vyuokwa hali ilivyo sasa hivi, waalimu jiandaeni. Taarifa za kitaalamu ni kwamba Vijana wanapambana na ugonjwa huu vizuri kuliko wazee. Madarasa ya vyuo vyetu ni kama kambi. wanafunzi hujaa hadi pomoni na wengine hukosa kabisa nafasi ya kukaa. Mgonjwa mmoja anatosha kuambukiza darasa zima kwa siku moja tu!

Waalimu wa vyuo walio wengi wako kwenye umri hatarishi kwa corona na hawa ndo watakaokutana na vijana ambao sasa watatoka majumbani kwao na kusafiri nchi nzima. Nionavyo waalimu jiandaeni kupigwa na corona.

Inasikitisha, maana wanasiasa kule Bungeni na hata maofisini na huko ikulu, wanaogopa mikusanyiko lakini wako tayari kuwajaribia vijana wetu na wataalamu wetu kuanza kuchanganyikana kwenye madarasa ambayo yalishazidiwa wingi wa wanafunzi.
 
Ni mapema sana kutabiri hayo maafa kutokea. Ngoja tusubiri huo muda ufike ili ukweli ujulikane.
 
tmp-cam-721743764.jpg
 
Only time can rule out our judgment
Tatizo woga umezidi
Acha vijana wapate Elimu jamani
Watakaa hivi mpaka lini??
 
Vyuo vitafunguliwa lakini haitakuwa kienyeji hivyo unavyowaza wewe,au hujui kuwa mkuu wa nchi mwenyewe naye ana watoto...?
 
Mkuu,

Chuo kikifunguliwa sitaenda darasani.. Nitawalipa Hela kidogo ili wanifanyie usajili then narudi zangu home.. Sitokaa hostel... Nitaenda kweny test tu
 
Back
Top Bottom