Kufungulia Nchi? Kurudi Kujivunia Umaskini?

Kwani huyo aliyekuwa akifoka kutwa kucha alifanya lipi la maana pamoja na kufoka kwake, kufanya udhalimu na dhuluma za kutisha?
 
Kwa miaka 5+ tulikuwa na rais wa wanyonge na nchi ya wanyonge. Mbona hukuanzisha uzi mkuu kupinga unyonge wetu?
 
Magufuli alikuwa haongezi mshahara, hatoi ajira, hataki wawekezaji, anaua biashara kati ya Tz na nchi jirani, na alikuwa anataka kodi kubwa, sasa hayo yangewezekanaje ndugu yangu? tulikuwa tunaelekea shimoni kwa kasi ya ajabu sana bahati nzuri Mungu akatuokoa
 
Heri ya kuomba kuliko kupora pesa za watu na kuanzisha kodi mpya kwenye vyanzo vile vile vya siku zote
 
Inaonekana Mzee Mwanakijiji ujaelewa maana ya kuifungua nchi na dhana halisi ya umaskini.
 
Mpuuzi sana huyu jamaa hayuko consistent kabisa. Kaandika upumbavu mtupu utadhani wakati wa dhalimu umaskini ulifutika nchini wakati uliongezeka kwa kasi ya kutisha.
 
Kwani kuna siku tulitoka kwenye umasikini?
 
1. Huogopi kuitwa MATAGA?

2. Wewe ni Sukuma Gang!

3. Utaambiwa unamchukia Mama 🤣.

4. Usisahau kuwa huyu Mama hakosolewi! Ukithubutu tu, utaambiwa unamtaka Magufuli ila bahati mbaya harudi tena!
Mama hana tatizo, maana nia haiwezi zidi uwezo... tukumbuke mama wa watu hakuuomba urais wala mama wa watu hakuuomba umakamu wa rais uliompelekea hapo alipo... cha kujiuluza ni mfumo wetu yaani katiba kama kweli ina uwezo wa kutupatia viongozi imara ...
 
Kwa mara ya kwanza faida imeanza kuo ekana ...kwa mara ya kwanza mwez may 2021wafanya kaz wangu 15 nimeweza kuwalipa full salary...nilikiwa nalipa nusu au robo tangu 2018 ..ule mtindo wa kukwapua hela ,kutishana sijui uhujumu uchumi imeisha tangu jamaa 'AFWE'..na kodi stahiki inalipwa..kidogo kidogo nchi inafunguka
 
Unazungumzia Instagram kule kwa akina Amber Lulu, Harmorapa na akina Gigy Money! Kule ambako wamejaa watu wenye ufinyu mdogo wa uelewa ambao chochote utakachowaambia wanakubali na kupiga makofi!!!

Hao wanaotukana hapa ni akina nani kama sio Misukule ya JPM ambayo na yenyewe waliapa kutetea chochote kile kinachomhusisha Jiwe hata kama ni cha kipumbavu!!

Kila mwenye akili timamu bado anakumbuka sakata la clip ya Gwajima aliyokuwa anawahamasisha watu wa kabila lake wapiganie na kuulinda urais wa JPM!

Walivyo wajinga, walidhani na bado wanadhani urais wa JPM ulitakiwa kutetewa na kupiganiwa na watu wa kabila lake! Matokeo yake, wakiona mtu ana misimamo tofauti na Mungu Mtu wao basi lazima waje juu kwa sababu walishaapa kutetea urais wake!!

Kwahiyo kama watu wenyewe unaowazungumzia ndio hao, wapite hata barabarani kutukana kwa sababu kila mwenye akili timamu anafahamu wapo kwenye wakati mgumu unaotokana na ujinga wao!!

Yaani hapa wanatamani Samia kila siku akosee ili waseme "Angekuwepo JPM..." VERY STUPID!!!

Ajabu zaidi, leo hii wakiona chochote kinaachofanywa na Samia kama kilikuwa hakifanywi na Jiwe, basi wanakuja juu kwa sababu wanaamini Samia anajaribu kumkosoa Mungu Mtu wao!!

Ndo unawashangaa hata watu kama Mzee Mwanakijiji! Yaani pamoja na uelewa alionao bado anajitoa ufahamu kana kwamba hafahamu mahusiano na Kenya yalivurugika sana!!! Cha kushangza zaidi, wala sioni cha ajabu alichoongea SSH...

NI nani mwenye akili zake anayeweza kupinga ukweli kwamba Kenya ni one of the biggest business partner in Tanzania?! SSH alikuwa Ikulu for 5 years... sasa kama aliona kulikuwa na mapungufu pahala, kuna tatizo gani kurekebisha?

OH! Ndo kama nilivyosema hapo awali... wanaona anamkosoa JPM... Mungu Mtu ambae alikuwa hafanyi makosa, na kwahiyo yote yaliyokuwa yanafanywa na yeye ni LAZIMA yaenziwe hata kama ni ya kijinga!!!
 
No matter what happens so long as a spade is called a spade...

Sio tunaambiwa kwamba tunafanya yote kwa pesa zetu kumbe kwa mlango wa jikoni tunaomba..., tunawaita watu mabeberu wakati tunapowaomba ni wadau..., tunaleta propaganda na story za vijiweni kuhusu kila shida zetu kwamba ni beberu mtu akiwaza vingine kalipwa na mabeberu...

Yaani binafsi nilichoka kuishi nchi ya Kusadikika au kwenye the Matrix..., bora tu kuishi kwenye uhalisia...
 
Hii nchi ilikuwa imefungwa na nani?

Wakati nchi inafungwa huyu Madam SSH yeye alikuwa wapi na alikuwa nani?

Kwanini hakusimama na kupinga hadharani mipango ya aliyekuwa Boss wake?

Nini maana ya kuwa Mzalendo? Kama kweli huyu Madam SSH ni mzalendo wa kweli kwanini aliacha tu Boss wake aifunge nchi?

Kama aliona TRA wanakusanya kodi za dhuluma, yeye akiwa kama Makamu wa Rais, Mzalendo wa kweli, Muislamu safi, alichukua hatua gani kwa nafasi aliyokuwa nayo?

Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kabla ya kuanza kushabikia "porojo" za huyu Madam SSH. Nasema ni porojo sababu yeye alikuwa ni namba mbili kwenye uongozi wa JPM na kila kilichofanyika kiwe kizuri au kibaya yeye hawezi kujitenganisha nacho.

Nachelea kusema huyu Madam ni mnafiki tu wa kisiasa, wala hana jipya. I presume she'll go down in history as the weakest President this country has ever had. Time will tell.
 
Leo wakulungwa mmemuamulia huyu Mzee! Safi kabisa
 
Changamkia sasa fursa hiyo fungua kiwanda au shamba ,wacha vijineno vya kwenye kanga.Taga nini wewe !!??
 
Nilitaka kugonga likes nyingi hapa; kwa bahati mbaga mfumo hauruhusu zaidi ya moja. Safi sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…