Sitakaa nisahau siku ambayo mshikaji wangu mmoja alipewa dili LA kwenda kuchukua watu moshi walioenda kwenye sendoff kuwarudisha arusha,mshikaji alipokuwa anafanya job kaachiwa funguo za magari tajiri na familia wamesafiri,mshikaji akatoka na Cruiser akaacha simu rehani kwa mlinzi Wa getini akapewa mshiko Wa mafuta kwa mkataba kuwa akirudi anarejesha hela anakomba simu yake.
Mshikaji akaenda moshi akawachukua RAIA,wakati wanarudi akala mzinga akaua watu kadhaa na yeye akafa pia.
Asubuhi mlinzi akakabidhi Lindo hakujua kama kuna Msiba akaenda home kwake,sisi tukapata taarifa kuwa mshikaji kachomoka na ajali.
Dah usiku kama SAA nane hivi siku ya pili mlinzi akapekuwa simu y marehemu akakuta no za watu ambao wanawasiliana na marehemu Mara kwa Mara si akaniichomoa,akanipigia kwa simu ya marehemu SAA mane usiku mana ilikuwa na hela ya kupiga.
SAA nane nasikia simu inaita nhriiii nkashtuka usingizini nkachukua simu niipokee dah kucheki marehemu ndo ananipigia sikumbuki simu ilifikaje sakafuni na ubabe wangu wote niliogopa hasa.
Nje ya mada ila nimekbuka hiki kisa.kilichosaidia alivyoona sipokei akatuma SMS hivi unahabari Fulani kafariki?.miaka zaidi ya kumi mpaka Leo Nina no yake,though haipatikani ila sijafuta bado.