Mgagaa na Upwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 13,481
- 28,116
Baba yangu alifariki 2017 Mama yangu alifariki may mwaka jana,namba zao zote bado sijazifuta,hali ya kuondokewa na wapendwa uisikie tu usiombe ikukute kwani maumivu yake hayasemeki
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daah inauma sana.Awe mume, mke, mtoto, mzazi babu au bibi hata rafiki au mpenzi. Marehemu akisha kufa inauma sana kufuta namba zake za simu. Wakati ule wa simu za mezani za Shirika la Posta na Simu, jirani zetu walifiwa na mama yao ambae ndiye alikua na akaunti ya simu.
Walikaa miaka mingi wakilipa ankara kwa jina lile mpaka siku ilitokea matatizo, Posta walimuomba mwenye ankra aende ofisini. Baba alikwenda, alijibiwa tunamtaka mwenye jina. Aliwajibu kuwa mwenye jina ni mke wangu alifariki miaka mitano iliyopita.
Waliomba kuona cheti cha kifo na kujiridhisha, mzee aliambiwa ni kosa la jinai kuendelea kutumia jina la marehemu. Ilibidi jina la ankra kubadilishwa.