Kufuta namba ya simu ya marehemu inauma sana

Miaka 3 mm nina namba ya swahiba wangu mkubwa huu ni mwaka wa 10 sasa
Alifariki mwaka 2010 lkn chakushangaza miaka yote hiyo mpk sasa hiyo namba tigo hawajawahi kumpa mtu mana nikiwa na huzuni napigaga lkn najibiwa haipatikani

Kwa mm siwezi kufuta namba ya marehemu aisee
Tangu nianze kumiliki simu sijawahi futa namba za marehemu nina namba za ndugu zaidi ya 7 kila nikijaribu kufuta nashindwa aisee
Mm namba muhimu nasave kwenye laini hata nikiwa na kitochi nakuwa nayo namba yako so katika hiyo phonebook ya SIMCARD nina namba za marehemu si chini ya 7
 
Yeah upo sawa maybe I will see her again ...in heaven I hope so [emoji17][emoji17][emoji853]
Utamuona[emoji4]
Hakuna namna tutafika Mbinguni pasipo kufa ..

Jitahidi Sasa utengeneze njia zako ili uweze kufika Mbinguni kumuona..I hope yupo huko.. swali wewe je ntafanikiwa kwenda njia aliyopo?

Mungu hakosei ..yatupasa kushukuru
 
Mimi ninazo mbili hata text message sijafuta na za mwisho zote zilikuwa ni kunishukuru 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Namba ya mzee sijaifuta hadi leo na simu yake ninayo mpaka sasa naitumia ikiwa na line yake. Naitumia kulipia dstv, luku na maji kama ambavyo alipendelea enzi za uhai wake.
 
Sijafuta namba ya marehemu baba. Mwaka wa pili hii unaisha toka mauti yamkute. Ni siifuti kabisa. Acha ikae tu maana kuna wakati naona kabisa "Baba calling...."
 
Namba ya marehemu dada yangu nimeifuta mwaka jana.
Ni baada ya miaka mi4 kupita.

Kuna muda nilikuwa naiangalia na kujipa matumaini ya kusadikika kwamba itaita.

Siku naifuta nililia sana Sana.
Nililia mno.
Very sorry,
 
Mimi nilikua na simu ya Marehemu Baba sikuwahi kuizima... Wiki Moja baada ya Mzee kufariki, baadhi ya marafiki zake mshua wakawa wanapiga sasa, nikawa naogopa hata kupokea nikazani labda hawana taarifa au wanatest kma ipo hewani.
End of the day, line nilitoa... Namba ipo mpaka kichwani
 
poleni sana wote mlio poteza wapendwa wenu inauma sana.

nilimpoteza rafiki yangu wa shule mpaka leo naumia,maana alikuwa hawezi pitisha siku ajani text wasap,fb ama text za kawaida.
 
Sidhani Kama nitaweza futa namba za wazazi wangu..juzi nimeangalia namba ya Mama nilikuwa natamani hata iite angalau aniambie chochote dah!!..sijui kama nitafuta namba zao.
Pole sana best
 
Dani.eniumiza sana hii.
 
Poleni sana!
Mimi huwa na delete Kabisa,maisha inatakiwa yaendelee huku tukiwaombea walale pema peponi.
Sitaki stress.
 
Sitaki kukumbuka maana nitaumia zaidi,,nafutaga mapema sana,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…