Kufuturishana Wabunge Dodoma ni rushwa, ni nchi gani nyingine ina huu utaratibu?

Kufuturishana Wabunge Dodoma ni rushwa, ni nchi gani nyingine ina huu utaratibu?

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Wabunge waache huu utaratibu wa kufuturishwa kule Dodoma, Bunge linazidi kuwa too low sana, Juzi niliona Benki ya CRDB inawafuturisha, sasa chukulia kwamba Benki ikajikuta kwenye kashifa kubwa za pesa, hawa Wabunge wataanza kuona aibu ya kuishughurikia kisa inawafuturishaga.

Vipi na Majaji na wao wakaitwa sehemu na kampuni au Kiongozi then wa kafuturishwa?

Jana Waziri mkuu kawafururisha Wabunge, huyu ni mmoja wa wanao takiwa kuwajibika kutokana na Ufisadi kwenye report but now anafuturisha wabunge, Wabunge hawa lazima waje kuona aibu kumshughurikia waziri mkuu.

Nimejaribu kuchimbua kuona hata kwa EAC ni wapi kwingine huwa bunge lao linafuriswa kipindi cha mfungo, nikakuta hakuna, nimejaribu kutafuta ni wapi kampuni kubwa zinafuturisha wabunge nako nimekosa.

Kenya wana Makampuni makubwa kwa mitaji kuliko haya yetu ila sijawahi sikia Safaricom au Kenya Comercial Bank inafuturisha viongozi wa kisiasa, kufanya hivyo ni tafasir ya rushwa moja kwa moja.

Kufuturisha watu ni jambo jema, shida ni pale linapo fanyiwa taasisi tena taasisi nyeti sana nchi hii.CRDB angesema anafuturidha wateja wake Dodoma na huko ndani Wabunge wakawemo kama wayeja, hilo lisingekuwa ni tatizo, ila pale Futari inapo kuwa maalumu tu kwa Wabunge hapo ni tatizo.

Na sio hili tu huwa naona mara timu ya bunge inapokea sijui vifaa vya michezo kutoka NMB mara sijui wapi, huu ni ujinga, sijui kama kuna watu wenye akili pale Dodoma wawaambie wakina Spika kwamba inapaswa Bunge kuachana na kupokea aina yoyote ya Zawadi, kama ni jezi wanakosa pesa za kununua jeszi na vifaa vya michezo?

Bunge libakuwa too low sana, lina tia aibu sana na mbaya hakuna anaye shitukia huu utaratibu wa kishamba sana.

Hata kwa wenye Dini yao huko Mashariki ya kati huwezi kuta Wanasiasa eti wanafuturishwa sijui na taasisi gani au Spika anafuturisha wanasiasa wake.

Screenshot_20230413_071430_com.facebook.katana.jpg
Screenshot_20230413_071540_com.facebook.katana.jpg
 
Shida ya ujinga hufanya watu kuwa waelevu wa ujinga wao na hukubali matendo ya kijinga kuwa sehemu ya maisha Yao sio bunge tu taasisi nyingi Tanzania hazijitambui

"Haki ni msingi wa kuinua taifa"
 
Futari gani hiyo inaliwa mezani? Maigizo hiyo futari inaliwa chini weka jamvi au zuria watu wakae chini wale futari
 
Wabunge waache huu utaratibu wa kufuturishwa kule Dodoma, Bunge linazidi kuwa too low sana, Juzi niliona Benki ya CRDB inawafuturisha, sasa chukulia kwamba Benki ikajikuta kwenye kashifa kubwa za pesa, hawa Wabunge wataanza kuona aibu ya kuishughurikia kisa inawafuturishaga.
Katika Uislamu watu muhimu kufuturisha na wale wasio jiweza wenye maisha duni......ila kwa wa bunge pale ni siasa, public relation , connection nk ila sio kiimani.
 
Wanakosea sana kutumia neno sadaka halafu ikajumuisha na neno wabunge.

Lengo hasa la sadaka ni kusaidia wale wasiojiweza. Sasa mbunge unampa sadaka ya nini?

Wangeandika Waziri Mkuu afuturisha wabunge na sio atoa sadaka ya futari.

Ila tuna la kujifunza kama wanadamu, gharama iliyotumika kulisha hao mafisadi ingetolewa nusu yake tu ikapelekwa kwa watoto yatima hakika ingelisha wengi zaidi na dhamira hasa ya sadaka ingetimia.
 
Hapa wewe unaweza kuwa mjinga zaidi tafuta mahali nimepost "KOSA"
We ni mjinga kubali, make kwa comment yako kosa unalo ona ni kufuturishwa juu ya meza, basi, hilo ndio kosa hizo taasisi zinafanya.
 
Yaani unaweza kumfuturisha mtu mwenye mshahara wa 12+... Wakati Kuna waislam wasiojiweza?. Ni upuuzi uliopita kiwango.
 
Wanakosea sana kutumia neno sadaka halafu ikajumuisha na neno wabunge.

Lengo hasa la sadaka ni kusaidia wale wasiojiweza. Sasa mbunge unampa sadaka ya nini?

Wangeandika Waziri Mkuu afuturisha wabunge na sio atoa sadaka ya futari.

Ila tuna la kujifunza kama wanadamu, gharama iliyotumika kulisha hao mafisadi ingetolewa nusu yake tu ikapelekwa kwa watoto yatima hakika ingelisha wengi zaidi na dhamira hasa ya sadaka ingetimia.
Hata kufuturisha tu ni kosa kubwa sana, wapi kwingine usha ona? Au Tanzania ndio nchi pekeee ina Waislam? nitafutie kokote kule Duniani Wabunge wanafuturishwa
 
Hata kufuturisha tu ni kosa kubwa sana, wapi kwingine usha ona? Au Tanzania ndio nchi pekeee ina Waislam? nitafutie kokote kule Duniani Wabunge wanafuturishwa
Nimeliongelea kiimani zaidi ila ukiangalia kiitikadi pia ni kosa kama ulivyosema.
 
Back
Top Bottom