Kufuzu AFCON-2019: Stars yashindwa kufunga mahesabu mapema! Yakubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Lesotho

Ila hii post ingewekwa kwenye jukwaa husika la sports and entertainment ingependeza sana!
Siku muhimu kama hizi kwa nchi hili ni jukwaa sahihi. Hata redio za dini leo habari ni hii.
 
Weka na muda wa watch sio maneno tu
 
Lesotho wamekuja hapa bongo tumefungana 1-1, unategemea tukienda kule kwao kuna muujiza?
 
Lesotho wamekuja hapa bongo tumefungana 1-1, unategemea tukienda kule kwao kuna muujiza?
Kwa hesabu hizo hizo, cape Verde walitupiga ngapi kwao alafu hapa kikatokea nini? Kwasasa hizo hesabu hazisaidii bali ni kuitakia kheri vijana tuliowatwisha jukumu hili kwa niaba yetu.
 
Siku muhimu kama hizi kwa nchi hili ni jukwaa sahihi. Hata redio za dini leo habari ni hii.
Sema kwenye jukwaa husika uchangiaji ni mdogo mno. Ushindi hautapatikana kwa maombi wala kwa kuweka akili zetu huko. Kushinda au kushindwa itakuwa ni matokeo tu ya maandalizi endelevu. We can only keep our fingers crossed!
 
Umesema "Tanzania kwenye vita muhimu" iweje tbc hawaonyeshi badala yake ni azam!!!
 
nipo kwenye mtanziko kwenye hili
1.tukipita ccm wataongeza kwenye mafanikio ya jiwe
2.tukitolewa roho itaniuma
ila bora namba 1 itokee halafu tutapambana na ccm humu wakisema ni mafanikio yao
yes,siasa kila mahaliπŸ˜€πŸ˜€
 
Great. Positive vibes only, Tanzania mbele
 
Kwa hesabu hizo hizo, cape Verde walitupiga ngapi kwao alafu hapa kikatokea nini? Kwasasa hizo hesabu hazisaidii bali ni kuitakia kheri vijana tuliowatwisha jukumu hili kwa niaba yetu.
Kwahiyo kumbe ugenini Tz hatuna matokeo mazuri???
 
Wanachokipigania Lesotho ndicho hichohicho tunachokipigania sisi, nawaunga mkono wote katika vita yao. Mmoja ashinde tusonge nae mbele....
 
Kwahiyo kumbe ugenini Tz hatuna matokeo mazuri???
Kwahiyo mpira unaamuliwa kwa ubashiri huo? Basi tungewaweka mbao fc ile mechi ya marudio tuone. Tuwatakie kheri wenzetu tuache maneno maneno kwasasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…