Kufuzu AFCON-2019: Stars yashindwa kufunga mahesabu mapema! Yakubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Lesotho

Tulaumu kwa hoja...hivi hawa wachezaji wanakiwango kweli cha kucheza timu ya Taifa..hatuwezi kupiga hata pasi tatu..sawa pamoja na uwanja kutusumbua jinsi ulivyotengenezwa lakini kiwango hata cha umiliki wa mpira kilikuwa kibovu tena tushukuru mwalimu kaanzisha kikosi cha kulinda lisingukuwa lile kosa la mabeki kusababisha kona ya kufungwa leo tulistahili sale ya bola bila...bado tupo mbali kisoka.."amacha"
 
Ndio maana nawapendaga wale wa wazee na makomandoo wa Yanga na Simba kocha akipanga kikosi cha hovyo hawachelewi kumpa makavu na pengine kumpangia kikosi kabisa. Huu upuuzi eti tunamuachia mgeni apange kikosi eti kuheshimu professionalism hauna manufaa
 
Ningekuwa rais hao ningewapa kazi ya kusafisha vyoo vyote vya shule za msingi za kata. Wameenda kulitia pilau maharage yaliyochacha.
 
Siku tumewapiga Cape Verde mbili za mkwezi haya maneno hayakuwepo,hiyo ndiyo hurka ya mwanadamu anajitazama yeye kwanza, Lesotho waliihitaji pia hiyo nafasi kuliko mnavyofikiria.
Toa maoni yako kuhusu kikosi cha leo na kile kilichoifunga cape verde
 
Kwa ujumla Tanzania tumekosa watu sahihi kwenye maeneo mengi, na kwenye michezo hasa mpira ndio kabisa, hatuwezi kuwa na wachezaji wazuri ingali tuna ligi mbovu. Pia viongozi wetu na sisi tumekuwa na mihemko ya ushindi isiyokuwa halisi.
 
Baada ya timu kufanya vibaya. Je Kocha Emmanuel Amunike bado anafaa kuinoa Stars?
 
hapa matokeo yasipotangazwa Kama yalivyoletwa haendi mtu Afcon
 
Ushauri wangu kwa TFF.
1. Vunjeni mkataba na benchi la ufundi ili muokee hela mnazowalipa mishahara
2. Vunjeni hio timu ili wachezaji warudi kwenye kalabu zao wacheze kwa amani bila ya kuharibu na kupangua pangua ratiba ya ligi
3. Katika mechi dhidi ya Uganda wapeni nafasi wale watoto wa u17 ili wapate mazoezi mazuri ya kujiandaa na mashindayo yao ya mwakani kwa kuwa wao ni wenyeji
4. Mechi na Uganda hakuna sababu ya kuwatumia tiketi za ndege wachezaji wanaocheza nje hizo hela tumieni kuwaandaa hawa vijana wa u17
5. Tupunguze kuongea sana tujikite kwenye vitendo.
 
Siyo kuinoa tu inabidi akatiwe tiketi ya kwenda Nigeria moja kwa moja asije bongo
 
Hongereni sana Taifa Stars,
- Kuna wanaodhani mlikuwa mnapambana na kuku,

Kuna waliodhani kushinda ni kama "kuona shimo tu na kulenga",

Kuna waliodhani kushinda ni pesa tu "mkijazwa mahera" mambo yatakwenda,

Kuna waliodhani kushinda ni kuleta siasa ndani ya timu!

Hawakujua timu ni mikakati na mipango ya muda!

Hawakujua raha ya ushindi ni mipango sio matokeo!

Wanasihasa hawa......!!

Ki ukweli mmepambana na mmshindwa kiume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…