Kufuzu AFCON-2019: Stars yashindwa kufunga mahesabu mapema! Yakubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Lesotho

Naona hii Taifa Stars sasa itawekwa chini ya CDF Gen Mabeyo.
 
Kulikuwa Hakuna haja ya kuwaanzisha sonso na sebo tena upande wa ulinzi Sonso hajawah kuanza mechi hata moja leo anamuanzisha pia Sebo hajawah anza. Leo anawapa kikosi cha Kwanza tena ugenini mechi unayotaka matokeo. Nyoni angekaa 2 na Gadiel 3 pale kati Mkude.kweli kamerooon hyo tunaiona kwa macho
 
Habari zenu. Moja kwa moja
Katika kitu nilichokigundua toka naangalia mpira mara ya kwanza mpaka sasa
Kama ligi ya nchi husika ni mbovu baasi hata timu ya taifa ni mbovu ni wazi ligi yetu ni mbovu kabisa hakuna
Timu ya kuleta changamoto Africa itakayowezesha wachezaji kwenda mbali sasa je iweje taifa star
.
Timu makini haisubiri iwepo nyumbani ndio ishinde je kam upo katika mashindano japan ambapo sio nyumbani
Utashinda karibuni maoni na ushauri
 
Nakupa LIKE no matter ntaonekana naunga mkono uchochezi, sincerely umenikosha.. usatrumpjr
 
Taifa Stars ingeshinda leo ingefuzu moja kwa moja Fainali za mataifa bingwa ya Afrika baada ya miaka zaidi ya 30
Lakini ukiangalia fainali za kipindi hiki zimekuwa diluted, kwa maana badala ya mataifa 16 kama ilivyokuwa kawaida ingekuwa mataifa 24
Ila ingeshinda na kufuzu,

Lakini kwa wengi dilution hiyo isingetazamwa, kingetazamwa ni kitisho cha Rais Magufuli kuwa wangezitapika hela endapo wasingefuzu

Rais wetu mpendwa, John Magufuli alipooita Timu ya Taifa Ikulu aliwapa Sh. Milioni 50 na kuwaambia wasingeshinda hiyo hela wangeitapika kwa namna nyingine, pia aliwaambia alikuwa anafikiria ku deploy jeshi ndio liwe timu ya Taifa...


Basi kitisho hicho kingetumiwa kama propaganda kuwa Watanznia tunafeli kwenye mambo mengi tu sababu hatujatishwa vizuri.

So ingekuwa ni mwendo wa kutisha kila mahali bila kujali mipango

So kwa kuwa hatujashinda pengine tutajifunza kuwa mafanikio ni process na sio kitu cha short term kinachotokana na vitisho
 
kuna raia alikuwa analalamika kijiwe kuwa kocha leo kapanga kikosi cha kise,,, sasa nimeamini kwamba!
 
Kulipigania taifa hakuihitaji motisha ya rais.
Kunahitaji kujua wajibu wako tu kama raia wa nchi husika.
Kwasababu Rais alishaona mapungufu ya kiuzalendo kwa wachezaji ndio maana akafanya vile.
Sawa sawa na mtoto kushika nafasi ya kwanza darasani na kuzawadiwa japokuwa kuna madarasa mengine yanamngoja.
 
Hapana wachezaji wetu ni wazalendo sana tu sema hawana uwezo kupambana tu.
Kwasababu Rais alishaona mapungufu ya kiuzalendo kwa wachezaji ndio maana akafanya vile.
Sawa sawa na mtoto kushika nafasi ya kwanza darasani na kuzawadiwa japokuwa kuna madarasa mengine yanamngoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…