Wakuu,
Leo Tanzania inaweza kuingia kwenye historia muhimu sana kwenye ulimwengu wa michezo. Tunatakiwa kuishinda Lesotho kwa namna yeyote ili tuweze kushiriki michuano mikubwa kabisa barani Africa ambayo tulishiriki Zaidi ya miaka 38 iliyopita.
Watanzania wote tusimamishe kila kitu na kuonesha kila namna ya kuiunga mkono timu yetu ya Taifa. Masaa haya machache tuchafue mitandao ya kijamii na mitaani kuonesha mshikamano wetu nyakati muhimu kama hizi.
Hii mechi ya leo si ya kawaida bali ni vita ambayo tukishindwa ni taifa limeshindwa na tukishinda ni taifa limeshinda. Heshima ya ushindi wa leo itaiweka nchi kwenye ramani kubwa Zaidi kimichezo na Zaidi itabadili uelekeo wa michezo na hasa nafasi ya wachezaji wetu kupata fursa Zaidi kwenye Nyanja za kimataifa.
Kila lakheri timu ya taifa ya Tanzania, nendeni mkapiganie nchi kwa nguvu zenu zote. Wanajeshi wetu wengi wamemwaga damu zao kuipigania heshima ya taifa letu na nyie mtambue mnawajibu sawa na huo kwaajili ya Tanzania.
Taifa zima leo limeweka matumaini yote mikononi mwenu, kaipiganieni Tanzania na mlete heshima ambayo vizazi vyote vitawakumbuka kuwa nyie ndio mliorudisha heshima ya nchi baada ya miaka 38 kushindwa kushiriki michuano hii mikubwa.
"We will stand and fight here. If we can't stay here alive, then let us stay here dead." General Sir Bernard Montgomery
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars ….