KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018, Novemba 17 2015: Algeria vs Tanzania

KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018, Novemba 17 2015: Algeria vs Tanzania

Mi ni Simba ila nimesema ninavyodhani ndo ingekuwa, Algeria wamefika sana golini!
Lakini Mkwasa angemuacha Ally Mustafa kwa kuwa sababu kubwa ya Algeria kufika golini sana ni upungufu ktk ulinzi baada ya kadi nyekundu, Mkwasa angeingiza kiungo Mkabaji idadi ya goli zingepungua kidogo!


Kumbe lengo lilikuwa ni kupunguza idadi ya goli za kufungwa?! teh! teh!
 
Mbona Brazil alipigwa goli 7 na Ujerumani tena kwao? Tena ilikuwa ni Kombe la Dunia, haya mambo ya Kuingiza SIASA na UDINI kwenye kila kitu hayana maana kabisa na hayafai kutumika kwa nchi inayotaka maendeleo ya kweli.
 
Jamani mafanikio ya Mpira hayahitaji kuunda kamati za ushindi ndani ya mwezi moja utegemee kuitoa Algeria hizo ni siasa, ndiyo maana wenye akili zao walijitoa kwenye hiyo kamati tunahitaji kuandaa watoto wadogo kwa mategemeo makubwa mbeleni siyo zima moto hii yetu
 
Kwa kandanda walilocheza hapa nyumbani ni wazi kikosi sio kibaya kivile wanahitaji marekebisho madogo hasa kwenye saikoloji ya wachezaji waweze kujitambua na kujua wafanye nini na kwa wakati gani.

Nadhani hilo ndo kubwa wanalotuzidi hao wengine. Mechi ya hapa nyumbani timu ilitumia nguvu sana kwenye half ya kwanza na kiukweli wangekuwa makini wangepata si chini ya goli 5 kwa uchache.

Lakini kipindi cha pili wakati algeria walibadilika kwa kuongeza kasi na umakini, stars walianza kwa umakini mdogo na spidi ndogo iliyokuwa inapungua kadiri muda ulivyokwenda kitu ambacho kimekuwa tatizo la muda mrefu kwa tim hii ndo maana ikawa rahisi kupoteza mechi ile
 
Back
Top Bottom