TANZIA Kuga Peter Mziray afariki dunia Hospitali ya Rabininsia. Alikuwa mgombea urais 2010

TANZIA Kuga Peter Mziray afariki dunia Hospitali ya Rabininsia. Alikuwa mgombea urais 2010

Dah! Aisee.

Kuga Mziray alikua mshikaji wangu sana. Nimekua nae sana maeneo ya Kinondoni. Kuga alikua akifika DDz ananipigia sim tukajumuike, au kwa John Feza ananipigia kama niko maeneo ya jirani tukapige stori na kubadilishana mawazo

Ni mkubwa sana kwangu, sawa na mzee ila tulikua tunaelewana sana, tulitokea tu kufahamiana maeneo ya starehe. Alikua na vyombo vyake vya muziki nadhani vilikua hapo hunters kama sijakosea, akawa akaniomba nimtaftie mnunuzi.

Nimesikitika sana. Duniani kweli tunapita.

Poleni sana ndugu wafiwa.
Kweli Dunia tunapita ..Ni kweli Kama unavyosema ..Nimefahamiana nae 2001 ni Kati ya Watu ambao nawaheshimu sana..Alikua Rafiki,Kaka...Nadhani Kama ni Vyombo Kuna kipindi Alikua anamiliki restaurant Mikocheni (Oshin) ..Tangu nimeondoka Tz 2007 sikuonana nae tena..Mungu amlaze Mahala pema Peponi.
 
Pumzika kwa amani Peter Kuga Mzirai. Mchango wako ulioutoa kwa maendeleo ya taifa hili tutaendelea kuukumbuka.
 
Daaaaah! Pole kwa ndugu na jamaa zake wa karibu! Kabla sijaiona picha, nilifikiri ni yule ANAYEVAAGA KOFIA! Sijui anatoka mkoa wa Pwani, ambaye huwa anawakaba wapinzani wenzie!
Acha tu bro.
Yule anaitwa Fahmi Dovutwa
 
Kweli Dunia tunapita ..Ni kweli Kama unavyosema ..Nimefahamiana nae 2001 ni Kati ya Watu ambao nawaheshimu sana..Alikua Rafiki,Kaka...Nadhani Kama ni Vyombo Kuna kipindi Alikua anamiliki restaurant Mikocheni (Oshin) ..Tangu nimeondoka Tz 2007 sikuonana nae tena..Mungu amlaze Mahala pema Peponi.
Nimesikitika sana mkuu. Mziray alikua down to earth man, mimi kwangu ni sawa na mzazi wangu ila baada ya kuinteract mara moja mbili akawa mshikaji wangu sana. Kila wkendi alikua lazima anitafte tubadilishane mawazo.

Mara ya mwisho nilionana nae mwaka 2015. Baadae nikaondoka Dar es salaam, nimerejea mwaka jana 2017 June, hatunaonana toka mwaka 2015 ila kuna siku tuliwasiliana kwenye sim, nadhani ni mwanzani mwa mwaka 2016 au late 2015.

Alikua na live band yake iliyokua ikipiga hvyo vyombo, baadae akaidismantle ndio akawa natafta mahala pa kuvikodisha au kuviuza, akaniomba nimtaftie mahala ambapo anaweza kukodisha au kuuza.
Alikua mtu mwema sana.

Maisha ya hapa Duniani tunapita. Pumzika kwa amani Peter Kuga Mziray.
 
kirerenya Dah--poleni wafiwa wote, poleni Watanzania...niliwahi kuongea naye wakati fulani mambo ya siasa...dah..RIP
 
Hebu rudia tena kwenye CV mwaka 1983 alikuwa chuo cha Lumumba Urusi!!
 
Hapa ndipo nnapoona siasa ikipoteza vipawa, kwa elimu ya huyu jamaa naona kama hakutumika ipasavyo, anaonekana ana elim adhim sana lkn bahat mbaya sana hakuweza kutumika vyema na inawezakua ni kutokana na imani yake kisiasa
 
Daaaaah! Pole kwa ndugu na jamaa zake wa karibu! Kabla sijaiona picha, nilifikiri ni yule ANAYEVAAGA KOFIA! Sijui anatoka mkoa wa Pwani, ambaye huwa anawakaba wapinzani wenzie!

Yule ni Hashim Rungwe Spunda mkuu yupo bado ni Mwanasheria
 
Hakika safari hii ni yetu sote.

RIP.
 
Back
Top Bottom