Kugusana gusana kwa wanandoa sio kwa tendo la ndoa pekee

Kugusana gusana kwa wanandoa sio kwa tendo la ndoa pekee

Baadhi ya wanandoa hutomasana pale tu wanapotaka kufanya tendo la ndoa. Huo sio upendo bali ni shughuli.

Upendo wa kweli huambatana na kushikana shikana mikono bila sababu na hukumbatiana kwa sababu tu.

Mguse mpenzi wako - bila sababu. Mdada, mkalie kwenye mapaja huyo mubaba wako mkiwa sebuleni.

Mubaba ukikaliwa kwenye mapaja acha kushangaa shangaa, nawe gusa uso wa mkeo, shika mikono yake, endelea kujibu mapigo kwa kumshika shika nyashi yake.

Usisubiri muingie chumba cha kulala ndio muanze kugusana gusana...... Gusaneni kila siku. Kwa kucheza. Kwa upendo. Kugusana si mchezo wa mbele bali ni muunganisho wa moyo.

Kugusana gusana ni uponyaji kabisa.

Mkukumbatie jikoni. Peaneni busu mkiwa kwenye korido. Shikaneni mikono wakati mnatazama TV.

Hivyo ndivyo mapenzi yanavyokaa hai. Mapenzi ya kimwili hujenga usalama wa kihisia.

Mkiwa kitandani, msilale kama wageni. Gusanisheni miguu.

Mshirika wako si mto wa kutupa kando ,mkilala pasipo kugusana nafasi iliyowatenganisha inaweza kuwatenganisha mioyo. Kugusana ni sawa na kusema, "Niko hapa."

Hali hiyo inatuliza, Inafariji na Inaunganisha, Huwezi kujenga urafiki bila Kugusana gusana.

Endeleeni kugusana - kila siku, kwa upole, kwa kucheza. Gusaneni, jamani.

Ndivyo mapenzi yanavyopumua.

Msisubiri kugusana siku ya kupiga mtanange pekee.

Hali hiyo inatuliza, Inafariji na Inaunganisha, Huwezi kujenga urafiki bila Kugusana gusana.

Endeleeni kugusana - kila siku, kwa upole, kwa kucheza. Gusaneni, jamani.

Ndivyo mapenzi yanavyopumua.
Hapa ni kabla ya kumpa marejesho au baada? Toa maelekezo kabisa.
 
Back
Top Bottom