Kuhamishwa kwa Wamisai Ngorongoro, tumechelewa lakini tumpongeze Rais Samia. Tujifunze Canada na tusahihishe

Dunia itambue kwamba, Ndugu zetu Wamasai Wanateseka.

Wamasai ni wahanga wa Serikali ambayo imeshindwa kuwapa haki ya kumiliki na kuishi katika ardhi yao. Ni muhimu kuwawajibisha wale walio madarakani kwa matendo yao na kutetea haki za Jamii zilizotengwa.
 
Maamuzi ya miaka 100 ijayo huwaga sio maamuzi ya kucheka na nyani. Kilichofanywa na Rais Samia ni urithi wa Tanzania.
 
Ni muda muafaka wa kumpongeza Rais Samia kwa kuwahamisha Wamasai na wakazi wengine ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kulingana na maamuzi kama hayo yaliyowahi kufanyika Canada na Marekani...
Na "SIASA TUNAIGA CANADA???....
 
Mambo ya kuiga sijui Canada, sijui India sijui Cuba sijui Dubai nk...yanatoka wapi.

Kama tunaiga tuige na siasa zao pia na demokrasia yao.

Sio nusunusu....
 
Mambo ya kuiga sijui Canada, sijui India sijui Cuba sijui Dubai nk...yanatoka wapi.
Kama tunaiga tuige na siasa zao pia na demokrasia yao.
Sio nusunusu....
Demokrasia sio chupa ya Coca-cola lazima ifanane kila mahali. Demokrasia inatakiwa kufuata utamaduni wa eneo husika. Demokrasia ya mzungu ushoga unaruhusiwa ,je kwako ni sawa?
 
Kuandika uongo nikazi ngumu sana, inabidi ushushe gazeti Ili kujaribu kueafanya wasomaji wauine kama unafanana na ukweli lakini haiwezekani.
 
Mkimaliza kuuza Ngorongoro na Loliondo uzeni na mlima Kilimanjaro msisahau na Saanane Island hata ikulu ya Magogoni nayo msiache kuipiga bei,, siku umbumbumbu ukituisha tukute kila kitu ni cha wazungu na waarabu,,
Wasiwasi wako tu....[emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mara moja hii umeshachanganyikiwa na kupwagaza maneno namna hiyo ?!!! [emoji1787][emoji1787]

Kweli NGO's zimeshikwa pabaya.....mkuu hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho....

Serikali iko sahihi kuangalia maslahi mapana zaidi ya wachache humo Ngorongoro [emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Stop the Genocide
[emoji15][emoji15][emoji15]
Umeanza na "personality disorder" na kugeuka haraka kuwa na "psychosis" ?!!! [emoji1787][emoji1787]

Genocide gani ambayo the so called "perpetrators" wanawaacha wamasai wa maeneo mengine ?!!!

Genocide gani ambayo "perpetrators" wanawahamisha wengine kwenda kuishi MSOMERA HANDENI?!! [emoji1787]

Mirembe vitanda havitoshi na wengine kuzagaa humu mitaani ?!! [emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Njaa imekupanda kichwani wewe
 
Huyo mleta mada ni zaidi ya zwazwa
 
[emoji15][emoji15][emoji15]
Umeanza na "personality disorder" na kugeuka haraka kuwa na "psychosis" ?!!!
Ati ndi hoja hiyo?
[emoji1787][emoji1787]

Genocide gani ambayo the so called "perpetrators"
Hamna cha the so called hapa. Ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikiongozwa na Rais wake
wanawaacha wamasai wa maeneo mengine ?!!!
Usijifanye mbumbumbu
Genocide is happening!
Genocide gani ambayo "perpetrators" wanawahamisha wengine kwenda kuishi MSOMERA HANDENI?!!
Watu wa Handeni nao wameanza kurudisha kadi za CCM huko kwa "perpetrators"
[emoji1787]

Mirembe vitanda havitoshi na wengine kuzagaa humu mitaani ?!
So what, people won't notice the difference? We acha, kama Kusema Serikali ya Tanzania inahusika katika maangamizi ya wamasai loliondo na morogoro inafungua vitanda mirembe, so let it be.
! [emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
STOP THE GENOCIDE.
 
Ukweli ni kwamba Uhifadhi wa Serengeti wa leo hauwezi kulinganishwa na uhifadhi wa Canada au nchi yeyote ile kati ya karne hizo za 17 na 18, au kwa mantiki ya mleta mada, kuwafurusha Wamasai huko.
Kuna tofauti.

Uhifadhi wa Serengeti unatokana na kutambua thamani ya ecolojia ambayo ni makazi ya jamii ya Wamasai. Itoshe, mradi wa uhifadhi ulilenga kulinda usawa wa asili wa mazingira, kuzuia ujangili(ambao sasa ni kinyume au kinzani na baadhi ya malengo; umepewa kibali sasa kufanya ujangili), haijalishi-uhifadhi huo ulilenga kusaidia maendeleo endelevu na elimu kwa watu wa eneo hilo, yaani Wamasai. Serikali imeahindwa kufanya hivyo, sasa inawaangamiza. Waingereza na Wafaransa walipora na kuangamiza kila kitu huko.....

Pia, Historia inatuambia Canada katika karne ya 17 na 18 iligibikwa na unyonyaji wa maliasili na kuhamishwa kwa watu wa asili na walowezi wa Ulaya. Wakoloni hao wa kutoka ulaya walifika huko sio kwa uhifadhi bali kuanzisha biashara, mashamba ya kulima na vituo vya kijeshi kwa malengo ya kutawala-sawa na wanaofanya Waarabu Ngorongoro sasa na mawakala wake Serikalini.

kwa hiyo,
historia ya ukoloni wa Canada ulisukumwa zaidi na maslahi ya wachache na yaliharibu mazingira na watu wa Asili wa huko, they commited Gonocide. Hii haina tofauti na hawa wa sasa kufanya hayo hayo, sasa unawezaje kudai tuwaige Waingereza na Wafaransa waliovamia Canada na kusababisha maafa ya mazingira, maafa ya watu asili wa Canada?
 
Anawahamisha ili wafanye nini ? Kwangu mimi the End might Justify the means kama wanapunguzwa / Sio kumaliza wote ili watunza mazingira well and good ila kama wanahamishwa ili The highest bidder afanye yake watu wapate 10% hilo halina tofauti na wale jamaa waliokuwa wanauza ndugu zao kama watumwa...
 
Demokrasia sio chupa ya Coca-cola lazima ifanane kila mahali. Demokrasia inatakiwa kufuata utamaduni wa eneo husika. Demokrasia ya mzungu ushoga unaruhusiwa ,je kwako ni sawa?
Utamaduni wa TZ yenye makabila zaidi ya 100 ni upi?
Tunataka Katiba mpya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…