Kuhamishwa kwa Wamisai Ngorongoro, tumechelewa lakini tumpongeze Rais Samia. Tujifunze Canada na tusahihishe

Ukweli lazima usemwe!

Suala la Serikali kuwahamisha Wamasai katika eneo hifadhi ya Ngorongoro ni uamuzi sahihi kwa faida ya nchi kwa miaka mingi ijayo.

Ngorongoro isipolindwa kwa Wananchi kuondolewa ndani ya miaka 10 tu Ngorongoro itakufa na haitokuwepo tena.

Serikali inawajengea nyumba watu hawa, inawapa mashamba huko Msomera, inawapa mpaka hati za umiliki suala ambalo kiuhalisia hakuna Serikali kwenye Afrika hii itakufanyia hivi.

Tuseme ukweli, uamuzi wa Serikali kuilinda Ngorongoro kwa kuwandoa Wamasai ni uamuzi sahihi na lazima ulindwe kwa gharama zote.
 
Je, huko Canada pia hotels na lodges zimezagaa hifadhini?
Je, huko Canada pia walikiwa na mpango wa kuchimba madini?
 
Je, akili ni kuwaondoa Wamasai ili ulete utitiri wa wawekezaji wa hoteli na wachimba madini?
Je, kati ya shughuli za Wamasai na shughuli za hoteli na migodi shughuli zipi zina athari kubwa kwenye mazingira?
 
Kuna mwaka nilisoma taarifa fulani Wazawa wa Canada wanaidai fidia serikali yao kwa sababu walihujumiwa wakati wa kufanyiwa civilization mana walichukuliwa kwa nguvu kutoka katika makazi yao na kuwekwa katika hostels. Inaonekana malalamiko yapo mpaka leo. Je, ndio hao unaowazungumzia?
 
Tatizo sio kuondoa wazawa kwa ajili ya kutunza mazigira,na utalii udumu.tatizo mnatoa masaii mnaingiza mwarabu aje kuchimba madini gorogoro....mnaruhusu makampuni makubwa kuja kufanya uwindaji?
 
Takataka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…