"Nendeni nchi jirani au kwingine mkaangalie, mimi niliwahi kuingizwa ndani mchana kwenda kulala kutokana na hali mbaya ya usalama. Hapa kwetu Idara inafanya kazi kubwa, nchi imetulia," alizidi kuikingia kifua na kuwararua wakosoaji.
Katika kuonyesha jinsi idara hiyo inavyofanya kazi kwa ufanisi, Ngonyani alitaka Serikali kuongezea mishahara watumishi wa TISS na kuongeza, "hawa vijana tunashinda nao hapa hadi saa 4:00 usiku wanaangalia usalama halafu tunawasema hawafanyi kazi!"
"Tena nasema waongezewe mishara, vijana wanafanya kazi nzuri na kubwa ya kulinda nchi. Tunapaswa kuwapa nguvu siyo kuwalaumu siyo sahihi hata kidogo," alisisitiza Ngonyani (Maji Marefu)
Nionavyo:
Ikiwa jambo limesemwa na upinzani kwao ni Ovu hata kama kuna chembe za ukweli. Lakini likianzishwa na Mwenzao hata kama nikulisha sumu nchi watashangilia, Nakumbuka walivyomkingia kifua Chenge kwa Umoja wa maslahi ya Chama chao.
Nafika mbali zaidi BAE wanapokataa kuirudishia chenji serikali kwa harufu ya ufisadi serikalini Bunge limethibisha kwamba kweli serikali ni Mafisadi kwa kumkingia kifua Chenge ilhali ushahidi uko wazi.
HONGERENI USALAMA WA TAIFA KWA KULINDA AMANI YETU.
Binafsi namheshimu kuwa ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wa jimbo lake pasipo kujali kiwango cha elimu ya dunia, bali uwezo wake kwa uwakilishi kwa wanajimbo lake.Pia ni mtaalamu wa mambo ya jadi,ambayo pia yana nafasi yake kwenye jamii ya kiafrika na mchango wake kwa waafrika ambao ni utamaduni wetu wa kiafrika ambao unaheshimika kwa ndani [Private] wakati nje [Public] wanaukebehi,haswa wasomi wenye malengo ya upotoshaji,na ambao ni wateja wakuu wa sekta hii.
Ni aibu kwa jamii haswa wanaoitwa waastaarabu [Civilized] kusema ni washiriki wa jadi hiyo,yani mambo ya kijadi.Na kwa kuwa ni mambo ambayo jamii imekuwa ikiyakwamisha kiuwazi na hivyo kuyapa kipaumbele kibinafsi na kuweka kinga kuwa si jambo la kufahamika kwa jamii kwa upana wake na mchango wake katika KUDIDIMIZA MAENDELEO YA TAIFA HILI.
Kwa upande wake DK Ngonyani aka
Maji Marefu ni Mtaalamu kwenye fani yake ya JADI ambayo mimi kwenye upande huo sina ujuzi wowote na uelewa wa mambo yake, Tunafahamu uwepo wa mambo ya JADI kuwa yamekuwepo toka vizazi na uenda uwepo wake utaendelea kuwepo kututambulisha kuwa ndio moja ya uthibitisho kuwa tu Waafrika.Kwa waliopata kufika Nchi ya HAITI mambo hayo yako wazi kiasi kuwa kuna viini macho [Vodoo] zinauzwa waziwazi unachagua nini unataka,ni moja ya mambo makubwa yanayopatikana katika kanchi hako kadogo lakini kenye historia ya aina yake Duniani katika mambo ya Vodoo.
Hivyo sina cha kumlaumu kiongozi huyu kwa kuwa uwezo wake wa kuelewa [Intellectual ability] umefikia kikomo katika upana mzima wa hicho kinachoita USALAMA WA TAIFA,ingawa nae anao mchango wake mkubwa tu wa kuisaidia idala hiyo kama Mtanzania mwenye lengo jema la kuleta ustawi wa Watanzania.
Kwa waelevu [Intellectuals] huyu nae ana nafasi kubwa sana,tena katika kipindi hiki cha watendaji wengi katika utekelezaji wa majukumu yao wanapokutana na vitisho vya vodoo.
Asidharauliwe kwa fani yake bali apuuzwe kwa uelewa wake katika jambo zima la upeo wa mada husika kwa kuzingatia kuwa uwezo wake wa elimu umefikia kikomo.