Katika nchi yetu (Tanzania) kuna idara kuu tatu zinazoshughulika na kazi ya upelelezi/ uchunguzi. Idara hizo ni idara ya upelelezi wea makosa ya jinai (CID) idara ya Intelijensia ya jeshi (M I) na idara ya usalama wa Taifa. Idara hizi zinajitegemea na kila moja ina majukumu tofauti. Hata hivyo katika mazingila na nyakati maalumu, idara hizo hufanya kazi kwa kushirikiana ili kukamilisha shughuli fulani maalumu.
1. Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (CID).
Kama lilivyo jina lake, idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (Criminal Investigation Department) inashughulika na upelelezi wa makosa ya jinai, kama wizi, ujambazi wa kutumia silaha, mauaji, biashara haramu ya madawa ya kulevya, wizi wa kalamu (fraud) na makosa mengine mengi kama yalivyo ainishwa katika 'penel code'. Aidha idara hiyo pia inahusika na ukaguzi wa maeneo ya tukio (crime scene) na inao wataalamu wa kazi hiyo (forensic experts)
Aidha idara hii ndio inayohusika na kufanya uchunguzi wa mashitaka yote yanayofikishwa katika vituo vya polisi kwa ajili ya kupata ushahidi wa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani na kuwatia hatiani wavunjao sheria. Kutokana na majukumu ya askari wa CID hulazimika kuwa karibu sana na wananchi kwani kazi ya idara hii haifanywi kwa siri. Maafisa wa CID huwajibika kutoa ushahidi mahakamani kwa kesi zote walizo fanya uchunguzi.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]DCI Robert Manumba
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hata hivyo idara hii inao askari wachache wa kificho (under cover) ambao hufanya kazi ya kujipenyeza katika vikundi vya uhalifu (k.m wauza madawa ya kulevya, wezi wa mabenki n.k) kwa lengo la kupata taarifa za ndani za wahalifu hao. Kwa vile askari hawa pamoja na wengine wote wa idara hii hawavai sare na mara nyingi hubeba silaha (bastola) wananchi wanao wafahamu hudhani kuwa askari hawa pia ni maafisa wa idara ya usalama wa Taifa. Lakini ukweli ni kwamba askari wote wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (CID) ni waajiliwa wa jeshi la polisi na muda wowote na kwa sababu yoyote askari wa CID wanaweza kuhamishiwa katika idara nyingine za jeshi hilo kama kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), kikosi cha usalama barabarani (Trafic Police) au polisi wa kawaida (General duty)
Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai inaongozwa na Kamishna wa polisi Robert Manumba ambae katika kipindi chake ameonesha kuimudu ipasavyo kazi yake kwa kuboresha utendaji kazi wa idara hiyo, na kuinua morali wa askari walio chini yake. Makao makuu ya CID yako eneo la posta mpya katika jengo la wizara ya mambo ya ndani mahali yalipo makao makuu ya jeshi la polisi.
2. Idara ya Intelijensia ya jeshi la wananchi (Millitary Intelligence).
Hii ni idara ya usalama ya jeshi la wananchi wa Tanzania. Ingawa idara hii haitajwi tajwi sana, na wala haifahamiki sana miongoni mwa wananchi wengi, Idara hii ndio idara kubwa zaidi ya usalama PENGINE kuliko idara nyingine yoyote ile nchini. Idara hii hufanya kazi zake kwa usiri wa hali ya juu kama ilivyo idara ya usalama wa Taifa, na mara nyingi maafisa wa idara hii hushirikiana na maafisa wa Idara ya usalama wa Taifa katika kazi mbali mbali.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mkuu wa Majeshi Jenerali Mwamnyange
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kazi kubwa ya idara hii ni kuangalia usalama wa nchi ndani na nje ya jeshi, kuangalia usalama wa mipaka, kugundua njama za maadui wanaotaka kuvamia nchi yetu kijeshi, kufuatilia viashilia mbali mbali vinavyo onesha kuwepo kwa hali ya uadui kati ya nchi yetu na nchi jirani. Aidha katika kipindi cha migogoro, idara hii huwajibika kuchunguza na kujua uwezo wa adui ili kuwasaidia makamanda kuweka mikakati ya ushindi.
Idara hii pia huhusika na kufuatilia mwenendo wa maafisa wa jeshi na wapiganaji ili kulinda nidhamu ya jeshi, na kuwapasha makamanda habari kuhusu hatua za kuchukua ili kuinua morali kwa maafisa na wapiganaji.
Kwa sababu maafisa wa idara hii wako ndani na nje ya vikosi vya jeshi, mara nyingi wananchi wa kawaida hudhani maafisa wa idara hii pia ni maafisa wa idara ya usalama wa Taifa kwa sababu hawavai sare (walio nje ya vikosi vya jeshi) na mara nyingi hufanya kazi zinazo fanana na zile za idara ya usalama wa Taifa, na mara nyingine kwa kushirikiana na maafisa wa idara ya usalama wa Taifa.
(c) Idara ya usalama wa Taifa (TISS)
ITAENDELEA...
Angalizo: Mwandishi wa makala hii HANA UHUSIANO wowote na Idara ya Usalama wa Taifa
wala idara nyingine zilizotajwa katika makala hii.
Kwa maswali au maoni bofya kisanduku cha maoni.
Tembelea
www.mwana-dikala.blogspot.com upate uhondo zaidi!