Nkwesa Makambo
JF-Expert Member
- Aug 26, 2011
- 4,763
- 1,319
HATA KAMA UKO USALAMA WA TAIFA,HATUKUPIGI WALA HATUKUFUKUZI HAPA JF,Endelea na somo lako zuri tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.


Nakubaliana na wewe Mzee wa Rula.Kuna tatizo kubwa linaloikabili idara hii ni usiri wa mapendekezo yao, mimi naamini idara hii inafany kazi vizuri kwa kufuata weledi lakini ikumbukwe wao ni watu wa kushauri kwa kutumia vigezo na suala la kuamua lipo mikononi mwa serikali. Mapungufu mengine waliyoyataja wachangiaji nayakubali.
Waasisi wa TISS ni akina hayati Emil Mzena kwa kweli kipindi chake idara iliweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa, leo tatizo na changamoto inayoipata idara ni huu ubazazi wa ajira, waliomo ndani wanawapigia pande ndugu zao,hali hii inapelekea kuajiriwa wa koo fulani tu utadhani ndio warithi wa nchi hii, watu ambao uwezo wao ni mdogo katika kazi hii wakati Mzena alihahakikisha ajira inafanyika kiumakini sana wanatazamwa wenye vipaji vya kazi hii, leo wenye vipaji vya hii kazi wanaachwa nje kwa kuwa hawana ndugu ndani ya idara wa kuwapigia chapua waweze kuajiriwa, kwa muktadha kama tunataka idara irejee katika ile heshima ya mwanzo basi mabadiliko makubwa yafanyike pia Mzena alihakikisha uwiano wa makabila, leo tunaona walio wengi ndani ya idara ni wahehe,wabondei,wabena na wanyakyusa je uko wapi uadilifu? je makabila mengine hayana haki?
Mkuu, ninakugongea THANKS kwa angalizo lako.
Mkuu, ninakugongea THANKS kwa angalizo lako.
Ukichukulia Idara ya Usalama wa Raia na Mali zao, na Idara ya Usalama wa Taifa, ni kweli kuwa (baadhi ya) Watendaji wametoka katika maadili ya kazi zao na kujishughulisha na mbwembwe, sifa na hata uhalifu. Tumeona wanajeshi wakivamia wananchi eti kwa sababu mwenzaokwa sababu alinyimwa bia ya bure katika baa, akaanza kurusha makonde na wananchi wakarjitetea. Nimewahi kumwona Usalama wa Taifa mmoja ambaye kwa kuwa alikuwa hataki kutoa nauli kwenye daladala, ulitoa pingu na kumwonyesha kondakta. Raia mwema anaogopa kwenda kushitaki polisi au kutoa ripoti kwani wanaweza kumgeuza shamba la bibi. Hii ni aibu na kuidhalilisha Idara ya Usalama wa Taifa. Usalama wa Taifa wamekuwa usalama wa kulinda maslahi yao na baadhi ya viongozi. Hata ukupitia sheria ya kuanzishwa kwa Idara ya TISS, utagundua kuwa uteuzi wa Mkuu wa Idara unafanywa kisiasa kuliko kiutendaji. Ikiwa Rais ndie anayeteua Mkuu wa Idara, siku akija rais mwengine anateua mtu wake, kwa mujibu wa utashi wake.
Ukweli utabaki pale pale kuwa nchi inahitaji walinzi, inahitaji wapiganaji, inahitaji habari za kuisaidia nchi kujilinda, lakini kwa kukosa maadili katika shughuli zao (hapa nasisitiza neno "baadhi yao"), wamekuwa kero, aibu na hatari kwa taifa.
kwani wao wako juu ya sheria? Ni wakati sasa wananchi kutambua haki zao, hawawezi kukunyanyasa tu eti ni usalama wa taifa kwa mambo binafsi. Sasa usalama wa taifa na kuingilia social life wapi nawapi bwana!asanteni kwa taarifa muhimu kama hizi ni kweli na mm naboreka sana na hii hali ya watu kujitapa mitaani me uwt na kutuchukulia warembo wetu kisa utanifanya nn nitakupa skendo