Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

NB: VIONGOZI BORA, WATUMISHI NA WANYAKAZI BORA NA WAADILIFU WAKO NA WANA UWEZO MKUBWA SANA WA KULITUMIKIA TAIFA HILI ILA MAZINGIRA YALIYOKO NI HATARISHI ZAIDI KWA MAISHA YAO YA MBELE HAWAJAPATA NAFASI YA KUONYESHA UWEZO WAO.

Ahsante sana ni ukweli kabisa kwa maneno yako hayo hapo juu Derimto
 
Kwa sasa naona kazi zao zimeongezeka tofauiti na enzi za mwalimu.
Watu mtaani wanajisifu eti mimi usalama wa taifa ndo tabu ya kuajili makanjanja zamani ilikuwa issue kujua

mitaani makajanja ni wengi wengine wanajiita Usalama wa Taifa kama njia ya kuaminiwa na kutapeli watu. Mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa popote duniani hatakiwi kujitangaza/kuwa wazi
 
Soma sana magazeti kama Tanzania Daima, Raia Mwema, Mwanahalisi na Sani utakuta matangazo ya nafasi zao za kazi.

Kazi za Usalama wa Taifa hazitangazwi nafikiri watakuwa na utaratibu mwingine tofauti wa kuajiri. Anayeujua atuhabarishe ili mwenzetu apate kazi huko
 
Sio kweli kwamba ukiona gari halina stiker kwenye kioo cha mbele ni la Usalama wa Taifa. Magari yote ya serikali hayana bima wala road licence, nafikiri hii inatokana na ukweli kwamba serikali haiwezi kujitoza kodi yenyewe ingawa katika siku za karibuni kumekuwepo na hoja kwamba bima ni kinga ya abiria hivyo jambo hili linatakiwa kuangaliwa upya. angalia magari kama STG, STJ na SM, SK ya serikali hayana stiker mbele.

Ni hatari kufikiri kwamba kitambulisho chekundu pekee ni alama ya Usalama wa Taifa wakati ofisi nyingi zina vitambulisho vyekundu mbona tutatapeliwa mwaka huu kwa kutuambia rangi ya kitambulisho tu inatosha kujua mtu ni wa usalama wa Taifa. Nina marafiki zangu wana vitambulisho vyekundu nitaanza kuwakimbia kuanzia leo
 
Binafsi naamini kwamba ukitaka kufanya kazi ya kulinda usalama wa Taifa maslahi yasiwe ndio kigezo cha kwanza kwa sababu kazi hii ni ya kiapo tamaa ya fedha isiwe mbele. Hii maanake kwamba Afisa wa Idara hii asinunuliwe kirahisi na maadui bali azingatie kulinda usalama wa nchi yake kwanza.

Ni sawa na kazi ya Upadri au sister wa kanisa katoriki ukiapa kutooa au kutoolewa ni mpaka kufa. Tamaa ya kujenga familia na kupata watoto haina nafasi kwa padri au sister alieomba kazi hiyo kwa hiari yake bila kulazimishwa.
 
Naamini kwamba sio kila mtu anayejitambulisha mtaani kwamba ni usalama wa taifa basi ni kweli ni usalama wa taifa.
 
Raia Mwema: magari yanayoongelewa hapa ni yale yenye namba za njano za kawaida kama T 123 ABC.

Na pia, unasema Usalama wa Taifa hawatakiwi kujitangaza?......ukisoma hizi post hapa utaona kuwa hata wasipojitangaza kufahamika ni rahisi kweli kwa sababu:

1. magari yao, ingawa yana namba siziso za serikali, hayana stickers
2. wanakaa makumbusho
3. wana hivyo vitambulisho vyenye chuma na nembo ya taifa
4. kwa wale wanaolinda viongozi, basi viongozi wakipigwa picha, na wao automatically wanakuwa wamepigwa picha
5. kama raisi anaenda kuhutubia sehemu, wanakuwa kwenye msafara...ukifika unapoenda, na wao wanashuka na wanaonekana waziwazi....wala hawavai "KININJA" kuficha sura.

Sasa unavyosema hawapaswi kufahamika mi sijui unamaanisha nini.......Najua kuna baadhi wanaendesha magari ya kawaida yenye sticker na hawana vitambulisho na wanakaa kwenye nyumba za kawaida na hawamlindi raisi au kiongozi yeyote....hao ndio ambao hawawezi kufahamika.....lakini wenye sifa nilizozitaja hapo juu lazima wafahamike hata wasipojitaja.
 
Ndg Derimto huo ni ufafanuzi murua fanya kazi, vunja mipini shoka zibaki. Hiyo ni kazi kama kazi zingine tena ya uzalendo usijali fedha jali kutumikia nchi yako kwa uzalendo. Usitumikie mafisadi, walipue. History will tell.

Ulinzi na Usalama wa Tanzania ni wa Mtanzania mwenyewe,kila Mtanzania kila Mzalendo na hasa kila Mjamaa. Mwl Julias Nyerere.
 
Naamini kwamba sio kila mtu anayejitambulisha mtaani kwamba ni usalama wa taifa basi ni kweli ni usalama wa taifa.


Raia Mwema mi ningependa kuongezea kuwa HAKUNA usalama wa taifa yoyote ambaye anajitambulisha......actually mi mtu yeyote akinifuata akiniambia ye ni usalama wa taifa wala hanibabaishi.......kwa sababu usalama wa taifa hawana majukumu ya kumfanya lolote mwananchi wa kawaida.....kazi ya kukamata au kuhoji wananchi ni kazi ya POLISI tu!

Kwa hiyo most likely than not....mtu akijitambulisha kuwa yeye ni usalama wa taifa basi ni mwooooongooooo.

au wadau mnasemaje?
 
Kazi ya Usala wa Taifa haiombwi km nyingine. Kinachofanyika ni watu wenyewe wa usalama kufanya recruitment kutoka vyanzo mbalimbali, hususan katika vyuo vya elimu ya juu.

Taarifa na wasifu wa mtarajiwa hufanyiwa utafiti wa kina kabla ya mmoja wao kuwa na direct contact na mtarajiwa. wanaobahatika kupita mchujo wa awali huandaliwa mafunzo. Kinachozingatiwa mwanzo ni intelligence ya mtu, uadilifu na msimamo wake katika mambo ya msingi husuan ya jamii, mapenzi yake kwa taifa lake.

Na kwa vile kazi hiyo ina matawi lukuki basi hata recruitment inafanyika kutegemea mahitaji husika...Lakini good command katika fani yoyote ni kigezo muhimu kwani Hata kazi ya usalama wa taifa essentially inahusu ukusanyaji wa taarifa ( intelligence gathering), uchambuzi wa taarifa zilizokusanywa ( analysis), na enterpreters of the intelligence gathered). Ndio maana kuna watu wanaoitwa majina km informers, data collectors, analysers, undercovers na hata majasusi (spies), ambao hutumwa kazi nje ya mipaka ya nchi.
Huu unaweza kuwa ndio ukweli wenyewe lakini hii ya kwamba TISS wanaua watu napata shida kuliamini. TISS kuwa chombo cha kuua wananchi wake inahitaji maelezo ya ziada na kina ni jambo linalotisha na halihitaji kuaminika haraka bila upembuzi yakinifu.
 
Raia Mwema: magari yanayoongelewa hapa ni yale yenye namba za njano za kawaida kama T 123 ABC.

Na pia, unasema Usalama wa Taifa hawatakiwi kujitangaza?......ukisoma hizi post hapa utaona kuwa hata wasipojitangaza kufahamika ni rahisi kweli kwa sababu:

1. magari yao, ingawa yana namba siziso za serikali, hayana stickers
2. wanakaa makumbusho
3. wana hivyo vitambulisho vyenye chuma na nembo ya taifa
4. kwa wale wanaolinda viongozi, basi viongozi wakipigwa picha, na wao automatically wanakuwa wamepigwa picha
5. kama raisi anaenda kuhutubia sehemu, wanakuwa kwenye msafara...ukifika unapoenda, na wao wanashuka na wanaonekana waziwazi....wala hawavai "KININJA" kuficha sura.

Sasa unavyosema hawapaswi kufahamika mi sijui unamaanisha nini.......Najua kuna baadhi wanaendesha magari ya kawaida yenye sticker na hawana vitambulisho na wanakaa kwenye nyumba za kawaida na hawamlindi raisi au kiongozi yeyote....hao ndio ambao hawawezi kufahamika.....lakini wenye sifa nilizozitaja hapo juu lazima wafahamike hata wasipojitaja.

Asante kwa kunipa ufahamu zaidi.

kuna jamaa aliniambia kwamba Usalama wa Taifa wapo makundi mawili wale wa wazi na wa kificho. Kundi la wazi ndilo hilo la walinzi wa viongozi na wengine ambao sina maelezo zaidi na wengine ni majasusi ambao ni wa kificho. Hata hivyo, suala la watumishi hao kujiweka wazi wao wenyewe ni kinyume na maadili ya kazi yao.

Wanasema hata kwenye ulinzi wa viongozi usije ukadhani walinzi wa wazi wako peke yao bali kuna kundi kubwa la kificho linalochanganyika na wananchi wa kawaida. Kwa kifupi jamaa aliniambia kwamba kuwa Afisa wa wazi na kificho inategemea na aina ya kazi ya ujasusi unayofanya.

Kwa hali hiyo, na mimi naamini kwamba kuwatambua hawa jamaa kwa aina ya majukumu yao sio kigezo pekee kwamba wako wazi kwa kazi zote wanazofanya.
 
asanteni kwa taarifa muhimu kama hizi ni kweli na mm naboreka sana na hii hali ya watu kujitapa mitaani me uwt na kutuchukulia warembo wetu kisa utanifanya nn nitakupa skendo
 
asanteni kwa taarifa muhimu kama hizi ni kweli na mm naboreka sana na hii hali ya watu kujitapa mitaani me uwt na kutuchukulia warembo wetu kisa utanifanya nn nitakupa skendo

Hahahahahahahaha Hiii kali sana
 
recruitment haileweki kuna some people i know wako uko kwa sababu wameunganishiwa na ndugu zao eg parents, uncles etc ambao wanafanya kazi uko
 
Wadau naomba msaada, mi kila siku ninavyosoma vijihabari nazidi kuchanganyikiwa...eti kazi ya UWT ni nini haswa?.....

Chukulia mfano huu wa CIA na Taasisi yetu haitakiwi kuwa mbali na objective hizi
CIA Mission

We are the nation’s first line of defense. We accomplish what others cannot accomplish and go where others cannot go. We carry out our mission by:

  • Collecting information that reveals the plans, intentions and capabilities of our adversaries and provides the basis for decision and action.

  • Producing timely analysis that provides insight, warning and opportunity to the President and decisionmakers charged with protecting and advancing America’s interests.

  • Conducting covert action at the direction of the President to preempt threats or achieve US policy objectives.

Core Values


  • Service. We put Country first and Agency before self. Quiet patriotism is our hallmark. We are dedicated to the mission, and we pride ourselves on our extraordinary responsiveness to the needs of our customers.

  • Integrity. We uphold the highest standards of conduct. We seek and speak the truth—to our colleagues and to our customers. We honor those Agency officers who have come before us and we honor the colleagues with whom we work today.

  • Excellence. We hold ourselves—and each other—to the highest standards. We embrace personal accountability. We reflect on our performance and learn from that reflection.
source https://www.cia.gov/about-cia/cia-vision-mission-values/index.html

Na je? kuna kamati ya usalama ya bunge ambayo inawahoji hawa ndugu zetu wa Usalama wa Taifa?.......

Kwa Tanzania nadhani Kwa kisingizo cha usalama wa Tiafa Bunge halina wigo mpana kujadilia masuala haya hata behind closed door . Bunge likijadili masuala ya USalama yanakuwa sio yale critical. Nio maana mafisadi wanatumia mwanya huo kufanya mambo ya MEREMETA. Uliona PM katika kujibu kasfa hii alivyosema hii ni kampuni iko chini UWT then bunge likafungwa mdomo. Kule UK mpaka Tony Blair na viongozi wengine walitwa wazi kuhojiwa tena openly juu ya Vita ya IRAQ.

Pia, kuna rafiki yangu mmoja anataka kufanya kazi Usalama wa Taifa, kuna jinsi ya ku apply? (wapi, lini, kivipi, etc etc)......au ndio "you don't find us, we'll find you?"........

Tanzania hawa jamaa sijui huwa wanaajirwa vipi nasikia wengi wanachukuliwa wakiwa A level na Vyuoni. lakini nadhani kuna other sorce of employment

Naomba kuwasilisha Hoja

Binafsi vile vile huwa uwa niko interested kujua muundo wa hii Taasis yetu.

failure mojawapo niliyoobserve inayoweza kusababishwa na muundo wa kizamani wa hii taasisi ni Kitendo cha rais kuanguka. Hapa alitakiwa mtu aastafishwe au kufukuzwa kazi kwa mtazamo wangu.

Mfano
Analysis yao ya threat kwa rais wetu zimeweka Priority kwenye Physical Protection na sio Health Protection amabay hasa ndio threat kuu kwa rais wetu. So watahakikisha Bullet prooof za kutosha rais kuvaa wanasahau Kisukari. Wanaweza kuhakikisha chakula anachokula hakina sumu lakini wanasahu kujua sugar content ya chakula.

Sina uhakika lakini nashawishika kusema Muundo wa Taasisi yetu hauendenani na challenges na Opportunities za karne hii.
 
Huu unaweza kuwa ndio ukweli wenyewe lakini hii ya kwamba TISS wanaua watu napata shida kuliamini. TISS kuwa chombo cha kuua wananchi wake inahitaji maelezo ya ziada na kina ni jambo linalotisha na halihitaji kuaminika haraka bila upembuzi yakinifu.

Inawezekana ukawa haujasoma vizuri michango ya wenzako na wadau mbalimbali ambao wameweka kando mambo ya ushabiki kuchangia kwa manufaa ya wengi na ukaelewa mawazo na mtazamo wao na ndiyo maana unapata shida kuelewa baadhi ya mambo kama vile kuua.

Kufanya mauaji ni sehemu ya kazi ya TISS na idara yoyote ile ya kijasusi katika nchi mbalimbali ila haiwi wazi inaweza kufanyika kwa kuwekewa sumu ambayo mtu anaweza kufa hapohapo au baada ya siku tatu au hata zaidi kutegemea na aina ya sumu na kiwango chake na pia kuna ajali ya gari ambayo inaweza kuonekana kama ya kawaida kabisa au ya kusababishwa na aina ya hila yoyote ile kama ilivyotokea kwa Diana ionekane alikuwa anawakimbia wapiga picha na kuna ambayo wengi wamezoea ambayo ni ya kumfuata mlengwa na kumpiga risasi mahali popote nyumbani kwake, kwenye mkutano au sehemu yoyote inapopatikana nafasi hiyo.

Ni kweli kuwa kazi ya usalama wa Taifa ni kulinda masilahi ya Taifa lakini na raia wakeila kuna nyakati huwa ni kwaajili ya kulinda wakubwa wachache au serikali husika na masilahi yake na hapa inaweza kufikia hata kuua kiongozi mkubwa na mwandamizi au hata kundi la watu kwa mfano aliyekua waziri mkuu wa Israel Yitzak Rabin huyu alipigwa risasi na ikasemekana ni raia ila ukweli ulivyo yule hakuwa raia wa kawaida alikuwa alinda kile ambacho Waisrael wanakiamini siku zote na PM. Yeyote anapochukua nchi ile anatakiwa akifuate akikiuka siyo mwenzao tena atatolewa kafara kwa namna yoyote ile kuhakikisha Israel inabaki kuwa ilivyo kama wanavyoamini wayahudi na ni wakatili mawako tayari kuona mwarabu anapata anachokitaka okay basi tufanye hivi kule midle east kuna waarabu kibao tena ambao ni wazaliwa Israel kwa nini asitumwe kwenda kufanya yale mauaji lakini yakafanywa na myahudi mwenzake? Angalia wengine kama Rafik Harir wa Syria, na hata marehemu Kombe aliuawa na Polisi wakimtuhumu kuwa ni Jambazi pamoja na kuwa alijitambulisha kuwa yeye ni nani!

Ngoja nikupe mfano mwingine ambao huu utawachanganya wengi na wavivu wa kusoma na kuchunguza tutawaacha mbali sana WTC huko New York ambapo walikufa zaidi ya watu 3000 na kuwasingizia magaidi na kuzua vita ambavyo vimedhulumu maisha ya wanyonge wengi bila kujali aina ya dini kabila au hata utaifa maana walikufa wamarekani na waisilamu wa Iraq na kwingineko duniani na hata kumnyonga Sadam na hali ikawa mbaya Iraq kuliko alivyokuwepo Sadam Hussein na pia kubadilisha mambo mengi duniani ikiwemo kuvujiana heshima na kutuhumiana ugaidi kwa kumpima mtu kwa itikadi yake tu na hata kumdhalilisha

Ni matumain yangu humu JF. Kuna wakandarasi ambao wanaweza kutoa ufafanuzi wa jinsi gorofa linaweza kujengwa namna gani halafu ligongwe na ndege lishuke kama ice cream juani na kuwa vumbi na wanahabari watoe picha ambazo nyingi zinafanana na hasa ukizingatia kwa wenzetu suala TEKNOHAMA wako mbali wana vyombo vingi vya kudugundua mambo mengi HEBU WANAJF.TUSIWE WATU WA MALUMBANO MENGI HUMU NDANI TUPATE MUDA WA KUSOMA NA KUCHUNGUZA MAMBO KWA KINA UTANIELEWA NASEMA NINI HAYA NINAYOYANGEA HUMU

ANGALIZO: Hapa simaanishi magaidi hawapo laa ila magaidi wapo na wanafanya kazi zao na wengine kibao tunao hata hapa kwetu tena wanajishikamanisha vizuri sana wakubwa wa serikali zetu kwa kuifadhili na kutoa michango mbalimbali kwenye serikali na jamii kwa ujumla na ukijidai kuwafuatilia yaweza kukuta makubwa maana baadhi ya wakubwa wana masilahi yao huko.

Hivyo basi moja ya kazi ya idara yoyote ya ujajusi ni kufanya ujasusi na project za siri katika nchi mbalimbali tatizo ni kuwa hapa kwetu na baadhi ya nchi nyingi zinatumia vibaya Idara hizo badala ya kujiletea maendeleo kama Nchi za urusi na Asia na hivyo sehemu kubwa kuishia kulinda kundi la watu wachache na madaraka yao maana hao ndiyo wenye uwezo wa kumpoint mkurugenzi na wengine katika kazi nyeti za serikali iliyoko madarakani.

Idara hii ina watu wengi sana tena wengine hawathaminiki katika jamii kabisa na wanafanya kazi kizalendo zaidi na kutanguliza masilahi ya Taifa mbele lakini wanakwamishwa na urasimu na kutokuchukuliwa hatua kwa wahusika (watu hatarishi wa usalama) na ikumbukwe kuwa idara hizi kwenye nchi nyingi huingia maeneo mengi sana mbalimbali unaweza kumkuta waziri,Mchungaji, sheikhe, mhadhiri,mwana habari, mfagiaji, dereva wa dalala au tax, fundi viatu, mwalimu, padre,mwanamuziki, makahaba na kwa hapa Dsm. Hata muuza samaki (pweza) kwenye sinia anaweza akawa na akafanya kazi kwa ufanisi mzuri kabisa ila mwana usalama wa kweli hana na habebi bango la kujitangaza waziwazi kuwa yeye ni mwana usalama na ndiyo maana ukimwona mtu anajigamba sana ujue huyo ni feki na ana masilahi yake binafsi ukiacha wale ambao wanafanya kazi za wazi za kuwalinda viongozi Top5 kingine kazi ya kukamata wahalifu mara nyingi huwa ni kazi ya polisi na kama kuna ofisa usalam akitaka kukamata anaweza kukamata kama raia mwingine yeyote kulingana na sheria za nchi MZISOME! raia anaweza kumkamata mhalifu ila ikiwa ni lazima sana kwa mwanausalama kufanya hivyo kimabavu anaweza kufanya hivyo akishirikiana na polisi na vyombo vingine vya dola kama vile PCCB, Uhamiaji, TFDA, Jeshi nk. TENA IKUMBUKWE KUWA OFISA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA HAKAMATI MVUTA BANGI MARA NYINGI ATAKUWA RAFIKI YAKE ILI AWEZE KUJUA BANGI INALIMWA WAPI NA KUPELEKWA KUUZWA WAPI HAWAKURUPUKI TU. Lakini sio mbwembwe ambazo watu wengi wanapenda kujionyesha nazo kuwa wao ni wana usalama na kuwakera wengine.

Kwa kwa kuongezea ni kuwa hakuna jambo lolote la hasara na aibu ambalo linaipata nchi hii ambalo vyombo husika na Rais mwenyewe hana Taarifa nalo kila kitu kinajulikana na kutolewa ufanunuzi na hasra zake LAKINI KIKUBWA NI KWAMBA HUPUZWA KWANI WASIKA WENGI HUWA NI MASWAIHIBA WA RAIS AU WAZIRI MHUSIKA NA HATA VIONGOZI WAANDAMIZI Na ndiyo maana mara nyingi Rais anashindwa kuchukua maamuzi magumu maana yanaweza kumgusa yeye mwaneyewe au yalianzia kwake mwenyewe. Lakini idara ina heshima zake na kukusanya taarifa mbalimbali za kiulinzi na usalama na hata kiuchumi lakini hazitiliwi maanani zinawekwa kapuni na kama unabisha mtafute rafiki yako yeyote wa karibu muulize kiundani kama hawahui mambo yanyoendela nchi hii lakini hana namna ya kufanya.

OMBI NA TAHADHARI:
IDARA HII ISIBEZWE NA KULAUMIWA KWA KUWABEBA WANASIASA NA KUTOKUFANYA KAZI YAKE IPASAVYO NI KWA SABABU YA MFUMO WENYEWE ULIVYO KAMA NDANI YA JESHI NA IKUBUKWE KWA WALE WALIOPITIA HOJA ZANGU ZA MWANZO NILIONYESHA JINSI WANAVYOTOA KAZI KUANZIA NATIONAL SERVICE KWA MAANA HIYO IDARA HII NI PARAMILITARY NA KUNA CHAN OF COMMAND AMBAYO KILA MTU ANAIFUTA KULINGA NA ORDER ALIYOPEWA NA AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI NI RAIS MWENYEWE WA JMT.

ILA NA WAO WAMECHOKA NA UOVO UNAOENDELEA SERIKALINI MPAKA HUKO KWENYE MAJESHI NA HII NI HATARI SANA INAWEZA KUJA KULETA MACHUFUKO SIKU ZA USONI KAMA IVORY COAST NA KWINGINEKO MAANA HAWANA UHAKIKA NA MAISHA YAO YA BAADAYE YA WATOTO WAO NA NDUGU ZAO MAANA KILA KITU KIZURI NA CHENYE MASILAHI KIMESHIKWA NA WAKUBWA NA WAJANJA WACHACHE.
 
Habari hizi ni nzuri sana. nakushauri wewe mwenye wazo la kutafuta hiyo kazi nitafute nikufanyie assessment, huenda ukapata kama ukionekana unafaa.
Asante kwa kunipa ufahamu zaidi.

kuna jamaa aliniambia kwamba Usalama wa Taifa wapo makundi mawili wale wa wazi na wa kificho. Kundi la wazi ndilo hilo la walinzi wa viongozi na wengine ambao sina maelezo zaidi na wengine ni majasusi ambao ni wa kificho. Hata hivyo, suala la watumishi hao kujiweka wazi wao wenyewe ni kinyume na maadili ya kazi yao.

Wanasema hata kwenye ulinzi wa viongozi usije ukadhani walinzi wa wazi wako peke yao bali kuna kundi kubwa la kificho linalochanganyika na wananchi wa kawaida. Kwa kifupi jamaa aliniambia kwamba kuwa Afisa wa wazi na kificho inategemea na aina ya kazi ya ujasusi unayofanya.

Kwa hali hiyo, na mimi naamini kwamba kuwatambua hawa jamaa kwa aina ya majukumu yao sio kigezo pekee kwamba wako wazi kwa kazi zote wanazofanya.
 
Binafsi vile vile huwa uwa niko interested kujua muundo wa hii Taasis yetu.

failure mojawapo niliyoobserve inayoweza kusababishwa na muundo wa kizamani wa hii taasisi ni Kitendo cha rais kuanguka. Hapa alitakiwa mtu aastafishwe au kufukuzwa kazi kwa mtazamo wangu.

Mfano
Analysis yao ya threat kwa rais wetu zimeweka Priority kwenye Physical Protection na sio Health Protection amabay hasa ndio threat kuu kwa rais wetu. So watahakikisha Bullet prooof za kutosha rais kuvaa wanasahau Kisukari. Wanaweza kuhakikisha chakula anachokula hakina sumu lakini wanasahu kujua sugar content ya chakula.

Sina uhakika lakini nashawishika kusema Muundo wa Taasisi yetu hauendenani na challenges na Opportunities za karne hii.

Mtazamaji nimeipenda hii analysis yako.....ila kwenye hizo kazi za CIA ni kwamba tungependa TISS wafanye hivi...... lakini tatizo Tanzania patriotism/uzalendo umeenda na Mwl Nyerere....sasa hizi ni ufisadi tu...ukiwa na hela, ukiwa na nyumba ukiendesha gari zuri ndio kitu....oh, bila kusahau ukiwa usalama wa taifa (hata kama hufanyi kazi ya maana).

Ila mi nitaendelea kuuliza mpaka tujue, naamini Usalama wa Taifa au jamaa zao wakaribu watasoma hii thread na kurekebisha panapohitajika.
 
Habari,

Nimekuwa interested na mada iliyopo bandikoni, ila ningependa kufahamu kutoka kwa wana JF...

Jeshi la Ulinzi wa Taifa na Usalama wa Taifa nani superior kwa mwenzako? Kwasababu kwa mtazamo wangu ni kwamba they both play vital roles in the security of our nation.Kuna mtu mmoja ni mechanic ktk garage ya kaka'ake inayotengeneza gari za Ikulu, so the guy kind of shows of kuwa yeye ni UWT, anatembelea GX 100 ambayo windscreen haija bandikwa chochote, alichowahi kunikera ni kwamba alikuwa ananishawishi nijiunge na Police ila nikamtania kuwa its better nijiunge na TPDF but jamaa akaniambia wanajeshi ni WAS*NGE! I was a bit infuriated...

Naomba mnifahamishe nani ni nani?Tafadhali
 
Back
Top Bottom