DSN, idara yetu hii ya Usalama inafanya kazi nzuri sana na yenye maadili kwa ujumla wake, lakini ni ukweli usiopingika kuwa wapo baadhi ya maofisa wake ambao hutumiwa vibaya ama kwa tamaa zao binafsi za fedha, madaraka na baadhi ya viongozi wa nchi, hivyo sio vyema kuionyooshea idara nzima kwa baadhi ya mapungufu.
Pili, wa kuinyooshewa kidole ni sheria inayoiunda Tiss na sio Tiss yenyewe, kwani imenyimwa meno kuwa huru. Panaweza pakawa na jitihada nyingi zinafanywa katika shughuli zao, lakini mwamuzi wa mwisho katika kutia saini ni waziri mwenye dhamana ambaye ni mwanasiasa. Hivyo basi, katika mchakato huu wa katiba, ni vyema tukajadili pia sheria inayounda TISS ili iwe yenye meno na ifanye kazi wananchi waliowatarajia.
Tatu, maswali uliyouliza ni gape lilowekwa makusudi na viongozi, ili gape hilo liwe kichaka cha viongozi kujificha wao na maovu yao, wao na uhujumu wa rasilimali za nchi, wao na nia zao za kutawala nchi na watoto zao. Mfano; Meghji anaweza aseme fedha fulani zilitumika kwa ajili ya usalama wa taifa, hata kama siyo kweli lakini hakuna mwananchi anayeweza kuwahoji Tiss juu ya fedha hizo, na hata Tiss yenyewe hawawezi liongelea hilo hata kama wanajua siyo kweli. Lakini lazima tufahamu pia kuwa, uadilifu huanzia juu ndio uje chini, huwezi niambia mimi niwe mwadilifu ili hali kiongozi wangu anabofya kizenji rasilimali za nchi huku familia yangu inadaiwa dukani kwa mangi....!
Nne, tusitarajie afisa wa tiss aamke siku moja aseme sisi tunafanya hivi au vile, ila katika mchakato huu wa katiba ni sisi wananchi kushauri na kusema tunataka tiss itakayo simamia rasilimali za taifa, tiss itakayo hakikisha kuwa ili mkataba wa uchimbaji madini usainiwe lazima wao waidhinishe kwanza, tiss ambayo itajali raia wake kwanza zaidi ya wageni na mali zao, tiss ambayo itakuwa inaufahamu na kuchukua hatua juu ya hata kiongozi wa nchi aliyekuwapo madarakani au mstaafu, anaweza kuhaatarisha usalama wa taifa na rasilimali zake.
Tano, embu jichukulie wewe (DSN) kwa mfano, ni mwajiriwa kama afisa mdogo tu wa TISS. Unaelekezwa uende kwenye uchaguzi wa ubunge au udiwani sehemu fulani ya nchi, na chakufanya umeambiwa. Swali ndugu DSN, utamakatlia bosi wako huku ukijua huruhusiwi kukataa? Sio kwamba hujui kuwa, bosi wako naye kaambiwa na wake, bosi wake naye kaambiwa na bosi wake, na bosi wake naye kaagizwa na aliyemchagua ambaye anaweza awe ndiye mkuu wa vyote, ulinzi na uslam.
Ni mtazamo tu,
Kibanga Msese