Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

kwani hawa usalama wa taifa wa nchi yoyote ile wao wanaongozwa au wao ndio wanayoingoza nchi,hivi raisi hata kama akiwa mpinzani atawafanya nn?
anawafukuza kazi wote, si wako chini yake bwana! Imefanyika kwa kagame, museveni na hata bingu wa malawi.
 
enzi hizo kazi ya TISS ilikuwa inatufanya tusiaminiane..maana ilisadikika hata ukinong'ona na hata kama mko wawili tu.... Nyerere anasikia!
 
jaman, mi naitamani sana hii kaz je, ni hatua zip nipitie na nahitajika kuwa na qualification gani?
 
jaman, mi naitamani sana hii kaz je, ni hatua zip nipitie na nahitajika kuwa na qualification gani?

Kama unaweza kupata kazi nyingine yoyote hata kama si ya maana ni bora ufanye hivyo. Inategemea na leongo lako, lakini ni kazi ya mateso, na unaweza kulazimika kufanya mambo ambayo utajuta hadi siku unakufa, na ujue kuwa utashindwa ku-ejoy maisha yako kama mtu wa kawaida. Unless ni kwa kutaka sifa ambazo hazina maana, make it last choice.
 
Hivi nani kawaambia UwT wana kazi ya kufanya background check kwa potential appointees?
 
Kwa mujibu wa mambo yanavyokwenda kwenye swala zima la siasa zetu Tanzania na kuona thread nyingi zinazo husu siasa zetu Tanzania.Kuna picha mbaya ambayo binafsi nimekuwa nikijalibu kutafakari na nimeshindwa kuwa na majibu sahihi nayo ebu wanajf nisaidieni?
1: Je Usalama wa Taifa ni haki ya Serikali au ni Haki ya Umma?
2: Je raia wa kawaida wa Tanzania kujua taarifa za msingi kuhusu kazi [Basic Information] ya usalama wa Taifa lake ni kosa?
3: Je nini objectives and role za Usalama wa Taifa kwa Serikali inayokuwa Madarakani?
4: Je nini objective and role za Usalama wa Taifa kwa Wananchi yani Umma wa Watanzania.
5: Je majukumu na kazi za Usalama wa Taifa zinapaswa kuogopwa [Tisha] Wananchi au zinapaswa kuheshimiwa na hata kusaidiwa na raia wema [wazalendo] kama njia sahihi ya kulinda Taifa na mali zake?
Ebu pata picha inayojengeka kutokana na wachangiaji au waleta thread kama hiz chini

Thread: Ikulu yakanusha JK kuhusika kuvuliwa ubunge Mh.Lema

Hukumu ya leo imeibua mambo mazito …… shinikizo kutoka Ikulu hasa baada ya kuwa amekataa ombi la mmoja wa viongozi wakuu wa serikali wakati huo la kutaka agombee nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi kwa ahadi ya kumpa cheo kikubwa……Aliwataja waliomtaarifu kuanguka kwake kuwa ni pamoja …..na ofisa usalama mmoja wa ngazi ya juu (jina linahifadhiwa).

Thread ya : Kauli ya Nape Juu ya Arusha na Tafsiri Yangu
Bwana mdogo hapa Arusha tumechafukwa roho kwa yote mnayoyafanya. Chaguzi ndogo ni point muhimu ……….. CDM kwani dunia inatazama nini tunafanya hasa ukizingatia tunapambana na CCM, MAHAKAMA, POLISI, USALAMA WA TAIFA, TAKUKURU na TUME YA UCHAGUZI.Arusha tumejikomboa kifikra since Azimio la Arusha……..Nyie mna dola, sisi tuna Mungu.

DSN, idara yetu hii ya Usalama inafanya kazi nzuri sana na yenye maadili kwa ujumla wake, lakini ni ukweli usiopingika kuwa wapo baadhi ya maofisa wake ambao hutumiwa vibaya ama kwa tamaa zao binafsi za fedha, madaraka na baadhi ya viongozi wa nchi, hivyo sio vyema kuionyooshea idara nzima kwa baadhi ya mapungufu.

Pili, wa kuinyooshewa kidole ni sheria inayoiunda Tiss na sio Tiss yenyewe, kwani imenyimwa meno kuwa huru. Panaweza pakawa na jitihada nyingi zinafanywa katika shughuli zao, lakini mwamuzi wa mwisho katika kutia saini ni waziri mwenye dhamana ambaye ni mwanasiasa. Hivyo basi, katika mchakato huu wa katiba, ni vyema tukajadili pia sheria inayounda TISS ili iwe yenye meno na ifanye kazi wananchi waliowatarajia.

Tatu, maswali uliyouliza ni gape lilowekwa makusudi na viongozi, ili gape hilo liwe kichaka cha viongozi kujificha wao na maovu yao, wao na uhujumu wa rasilimali za nchi, wao na nia zao za kutawala nchi na watoto zao. Mfano; Meghji anaweza aseme fedha fulani zilitumika kwa ajili ya usalama wa taifa, hata kama siyo kweli lakini hakuna mwananchi anayeweza kuwahoji Tiss juu ya fedha hizo, na hata Tiss yenyewe hawawezi liongelea hilo hata kama wanajua siyo kweli. Lakini lazima tufahamu pia kuwa, uadilifu huanzia juu ndio uje chini, huwezi niambia mimi niwe mwadilifu ili hali kiongozi wangu anabofya kizenji rasilimali za nchi huku familia yangu inadaiwa dukani kwa mangi....!

Nne, tusitarajie afisa wa tiss aamke siku moja aseme sisi tunafanya hivi au vile, ila katika mchakato huu wa katiba ni sisi wananchi kushauri na kusema tunataka tiss itakayo simamia rasilimali za taifa, tiss itakayo hakikisha kuwa ili mkataba wa uchimbaji madini usainiwe lazima wao waidhinishe kwanza, tiss ambayo itajali raia wake kwanza zaidi ya wageni na mali zao, tiss ambayo itakuwa inaufahamu na kuchukua hatua juu ya hata kiongozi wa nchi aliyekuwapo madarakani au mstaafu, anaweza kuhaatarisha usalama wa taifa na rasilimali zake.

Tano, embu jichukulie wewe (DSN) kwa mfano, ni mwajiriwa kama afisa mdogo tu wa TISS. Unaelekezwa uende kwenye uchaguzi wa ubunge au udiwani sehemu fulani ya nchi, na chakufanya umeambiwa. Swali ndugu DSN, utamakatlia bosi wako huku ukijua huruhusiwi kukataa? Sio kwamba hujui kuwa, bosi wako naye kaambiwa na wake, bosi wake naye kaambiwa na bosi wake, na bosi wake naye kaagizwa na aliyemchagua ambaye anaweza awe ndiye mkuu wa vyote, ulinzi na uslam.

Ni mtazamo tu,

Kibanga Msese
Nawasilisha naomba msaada wenu kujibiwa maswala yangu hapo juu.Kwa kuwa binafsi najiaminisha kuwa Usalama wa Taifa iko kwa ajili ya Taifa na sio kikundi cha watu.Na kuwa majukumu yao ni kutenda na kulinda haki [usalama] isivunje na sio kuingalia haki inavyovunjwa.
 
[h=2]Usalama Wa Taifa: ni kwa ajili ya taifa kama jina lake lilivyo. Kama taifa ndio serikali pekee basi maana itakuwa usalama wa wanaccm na serikali yake. Amua wewe.[/h]
 
Usalama Wa Taifa: ni kwa ajili ya taifa kama jina lake lilivyo. Kama taifa ndio serikali pekee basi maana itakuwa usalama wa wanaccm na serikali yake. Amua wewe.

Warea ni sawa kama jina lake ndio tafsiri yake kuwa n kwa Taifa inakuwaje baadhi yetu wanawatuhumu kama hivi hapa!Je ni umma ndio unawaelewa vibaya na kutoa Tafsiri ambayo inazidi kujijenga kila siku mwisho na wanaingia kwenye kundi la vyombo ambavyo umma unamashaka navyo kama Daudi Mchambuzi anavyochangia hapo chin!!
Bwana mdogo hapa Arusha tumechafukwa roho kwa yote mnayoyafanya. Chaguzi ndogo ni point muhimu ……….. CDM kwani dunia inatazama nini tunafanya hasa ukizingatia tunapambana na CCM, MAHAKAMA, POLISI, USALAMA WA TAIFA, TAKUKURU na TUME YA UCHAGUZI.Arusha tumejikomboa kifikra since Azimio la Arusha……..Nyie mna dola, sisi tuna Mungu.
 
Kwa hiyo kila linalozungumzwa kuhusu usalama wa taifa ni kweli. I wish dunia ya majasusi ingekuwa huru kujibu tungepata taarifa sahihi kutoka upande wao
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Kwa hiyo kila linalozungumzwa kuhusu usalama wa taifa ni kweli. I wish dunia ya majasusi ingekuwa huru kujibu tungepata taarifa sahihi kutoka upande wao
.

Sio kila linazozungumzwa ni kweli ama si kweli kuwahusu lakini,wewe na mimi kama mwananchi na raia mwenye dhamira njema ya uzalendo na Taifa Je sisitahiki au ustahiki wewe au mwananchi mwingine yeyote kujua malengo na kazi zake Usalama wa Taifa ili tupate fulsa kutetea Taifa kwa nia njema na kuwasiadia pale wanapoitaji msaada wa raia yoyote yule kinyume chake baadhi yetu tumeanza kuwa na tafsiri ambayo huku mitaani inaanza kujijenga pole pole kama ambavyo Jeshi la Polisi limekua likilaumiwa mpaka kiasi cha kuanzisha operation ya Polisi Jamii ili kuweka mambo sawa na umma kufahamu mazuri ya polisi na sio kama inavyojikeza umma kutafsiri.

Ebu tiZama Usalama wa Taifa wa Kenya hivi ndivyo wanavyosema kuhusu dira [vision] malengo [Goal] mikakati [Mission]

Goal

"Prompt and quality national intelligence in the service of the people of Kenya."
Vision
"To create, manage and sustain an organisation that is both professional and accountable; founded on firm ethics... "
Mission
"To safeguard the Repubic of Kenya against any threats emenating from within and without

HIZI CHINI NDIO KAZI ZA USLAMA WA TAIFA WA KENYA [WANASEMA WHAT WE DO]

The Intelligence Cycle is the multi-step process by means of which security intelligence is sought, collected, processed and passed on. There are five phases in this cycle:
1) Planning:

The first step in this phase is to determine customer requirements. The Service is guided by its mandate as stated in the NSIS Act, 1998. The requirements are dynamic and change with the prevailing security situation and assessments on anticipated changes. Because of this, the Service is constantly in touch with customers to ensure that requirements are always current and relevant.
Determining customer requirements involves the identification of customer needs as well as translation of requirements into potentially achievable tasks and prioritizing, analyzing, reporting, and monitoring the quality of the product.
Once targets are identified, existing resources are used to gather intelligence but new collection requirements can be drawn depending on the type of information needed for reporting.

2) Collection:
The basic essence of collection is access to the required target. Information from members of the public, friendly governments, and technical operations is combined with information from open sources, including newspapers, periodicals, journals, electronic news media, official documents, and other published material.

3) Exploitation and Processing
This is the conversion of collected information into a form suitable for analysis or the production of intelligence

4) Analysis and Production
This involves analysis, evaluation, translation and interpretation of raw data into finished intelligence.

5) Dissemination

This is the final step of the intelligence cycle and involves passing the finished product i.e. intelligence reports, to the consumers. The quality and relevance of the disseminated reports may lead to re-specification of intelligence collection requirements, thereby completing the cycle.
 
ni hatari sana, maswali yako ni magumu.
tungekuwa wazalendo usalama wa taifa angekuwa ni kila raia wa nchi hii tukiongozwa na wachache katika kutoa na kupokea taarifa, lakini loh! asaiv usalama umehodhiwa na familia chache, imekuwa ni dili kuingizana huko kwenye hiyo idara nyeti, dili kwa makada kuweka watoto wao, wehu uliopitiliza, ndo maana kila mtu sasa anaropoka bar akilewa, anajifanya ni mtu wa TISS, mitanganyika tumelaaniwa na nani sijui.
 
Sina uhakika kama hawaoni kinachoendelea sasa..kukosekana maadili katika utendaji..Nidhamu na heshima katioka uwajibikaji,Rushwa na wizi na ubadhirifu kila idara jamani..kweli kitengo hiki kazi yake nini..watu wanatia aibu kila kukicha hata watoto wanaoanza kukukua sasa wanajua hali ni mabaya kila kona..inaanza nyumbani chakula haba,hospitali dawa hakuna ama feki,baadhi ya bidhaa bandia ama mbovu kabisaaa.

Najiuliza tena kitengo hiki maana yake nini hawa wanaohujumu uchumi hadi tumefikia hapa kweli watanzania wenzetu mliopewa dhamana mpo tuu,ukiondoa Iraq na Afghanstan sisi ni wa tatu kuomba omba,jamani hamuoni aibu..ukiondoa msumbiji sisi wa pili katika umasikini kweli vitengo hivi vinakazi gani katika inchi inakera kidogo.

Ukitaja usalama wa taifa napatwa wazimu hawasaidii lolote katika kuhakikisha hujuma mbaya inayoendelea katika uchumi wa Tanzania..uongo na majigambo yasiyo na msingi vimetuangamiza sana na bila juhudi za makusudi hakuna taifa la tanzania
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Mkuu kuna mambo mawili ambayo tunapaswa tuyafahamu: kuna serikali na dola.
Sasa tujiulize Idara ya Usalama wa Taifa majukumu yake yanaangukia wapi? Katika serikali au dola?!

Kama unafuatilia siasa za Marekani sasa (wakati huu wa kampeni za Republicans); Bwana Santorum na Bwana Romney wote hawa ni wagombea katika hatua za awali kabisa, si wafanyakazi wa serikali, lakini wamepewa ulinzi kutoka "secret service" baada ya kuomba!! Licha ya kuomba, lakini pale Marekani, security service kutoka "secret service" utolewa na wizara ya usalama wa mambo ya ndani kwa mgombea yoyote wa urais kutoka chama kikubwa cha siasa.

Sasa katika mazingira ya hapa kwetu, sijui kama inawezekana kwa Bwana Slaa au Bwana Lipumba kuomba au kupewa ulinzi kutoka Idara ya Usalama wa taifa; na sijui kama mabwana hao wanaweza wakawa na imani na amani kama wakiwa wamepata ulinzi huo!

Sasa kwa mfano huo (ingawa mifumo ya kisiasa haifanani), tunaweza kuuendelea kujadili kama usalama wa taifa ni haki ya serikali au haki ya dola (nimependa niseme dola badala ya umma, kwani dola linajumuisha umma pia).
 
NIONAVYO MIMI:

1. Inahitaji kuboreshwa (Reforms)

2. Inahitaji kuangalia upya juu ya ajira ya watu wake. I'm sorry nikiwaangalia wengine naona kabisa kuwa hawana sifa na hawafai kabisa hata katika kazi za kawaida za utumishi wa umma sembuse kuwa Intelligence Officer?

3. Utamaduni umejengeka sasa polepole nchini ambapo, wakweli na wachapa kazi kwelikweli hawatakiwi! Hapa ndipo penye kiama chetu. Yaani mi ningepewa tenda hata ya miezi sita tu humo TISS nitasafisha haijawahi tokea na uozo uko wazi wazi. Mfano mmoja ni kuwa kunapotokea skendo kubwa kama ya richmond n.k bila kufahamika wala kuripotiwa nao basi Mkuu na wenzake anaachia ngazi.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
DSN, idara yetu hii ya Usalama inafanya kazi nzuri sana na yenye maadili kwa ujumla wake, lakini ni ukweli usiopingika kuwa wapo baadhi ya maofisa wake ambao hutumiwa vibaya ama kwa tamaa zao binafsi za fedha, madaraka na baadhi ya viongozi wa nchi, hivyo sio vyema kuionyooshea idara nzima kwa baadhi ya mapungufu.

Pili, wa kuinyooshewa kidole ni sheria inayoiunda Tiss na sio Tiss yenyewe, kwani imenyimwa meno kuwa huru. Panaweza pakawa na jitihada nyingi zinafanywa katika shughuli zao, lakini mwamuzi wa mwisho katika kutia saini ni waziri mwenye dhamana ambaye ni mwanasiasa. Hivyo basi, katika mchakato huu wa katiba, ni vyema tukajadili pia sheria inayounda TISS ili iwe yenye meno na ifanye kazi wananchi waliowatarajia.

Tatu, maswali uliyouliza ni gape lilowekwa makusudi na viongozi, ili gape hilo liwe kichaka cha viongozi kujificha wao na maovu yao, wao na uhujumu wa rasilimali za nchi, wao na nia zao za kutawala nchi na watoto zao. Mfano; Meghji anaweza aseme fedha fulani zilitumika kwa ajili ya usalama wa taifa, hata kama siyo kweli lakini hakuna mwananchi anayeweza kuwahoji Tiss juu ya fedha hizo, na hata Tiss yenyewe hawawezi liongelea hilo hata kama wanajua siyo kweli. Lakini lazima tufahamu pia kuwa, uadilifu huanzia juu ndio uje chini, huwezi niambia mimi niwe mwadilifu ili hali kiongozi wangu anabofya kizenji rasilimali za nchi huku familia yangu inadaiwa dukani kwa mangi....!

Nne, tusitarajie afisa wa tiss aamke siku moja aseme sisi tunafanya hivi au vile, ila katika mchakato huu wa katiba ni sisi wananchi kushauri na kusema tunataka tiss itakayo simamia rasilimali za taifa, tiss itakayo hakikisha kuwa ili mkataba wa uchimbaji madini usainiwe lazima wao waidhinishe kwanza, tiss ambayo itajali raia wake kwanza zaidi ya wageni na mali zao, tiss ambayo itakuwa inaufahamu na kuchukua hatua juu ya hata kiongozi wa nchi aliyekuwapo madarakani au mstaafu, anaweza kuhaatarisha usalama wa taifa na rasilimali zake.

Tano, embu jichukulie wewe (DSN) kwa mfano, ni mwajiriwa kama afisa mdogo tu wa TISS. Unaelekezwa uende kwenye uchaguzi wa ubunge au udiwani sehemu fulani ya nchi, na chakufanya umeambiwa. Swali ndugu DSN, utamakatlia bosi wako huku ukijua huruhusiwi kukataa? Sio kwamba hujui kuwa, bosi wako naye kaambiwa na wake, bosi wake naye kaambiwa na bosi wake, na bosi wake naye kaagizwa na aliyemchagua ambaye anaweza awe ndiye mkuu wa vyote, ulinzi na uslam.

Ni mtazamo tu,

Kibanga Msese
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Ukitaka kuielewa hii tasisi inayojiita usalama wa taifa rejea kwenye historia. Hapo nyuma dunia iligawanyika kwenye makundi mawili yaani magharibi na mashariki (ubepari na ujamaa). Mifumo wa serkali na utawala ulitegemea nchi ipo upande gani, tanzania ilikuwa mashariki ambapo kinara wa mfumo alikuwa ni Soviet Union. Sasa hapa ndo pana chimbuko la utawala wa ccm, Soviet union kuliwa na KGB hawa ndo wababe hadi leo huko Russia, ni genge la ajabu sana ambalo linaingilia maisha ya kila raia na kumshurutrisha awe mnyenyekevu na mtumwa wa watawala. Wao ndo wajuzi wa kila kitu na wananchi wa kawaida wajibu wao ni kupokea maagizo na kutii.

Na lengo lilikuwa ni kwanza kuhakikisha wananchi wanakubali serkali ya kijamaa bila ubishi wa aina yoyote na pili kuwaandaa na kuwachagua viongozi wa serkali. Usalama wa taifa umejengwa kwenye misingi ya KGB na ni genge lenye mtandao mkubwa kuanzia vijijini hadi ikulu, hawa ndo chimpuko la viongozi wote katika ngazi zote kwenye taasisi zote za serkali. Watu wote wenye kutoa maamuzi kwenye taasis za serkali mfano mahakama, polisi, jeshi, vyuo, mashirika, vyombo vya habari nk nk ni usalama wa taifa tena wanajeuri, wanadharau na wanaamini wao ndo watu muhimu zaidi ya wengine. Hata upatikaji wa vyeo vya kisiasa vinafuata mfumo huo huo wa usalama wa taifa. Kwa kifupi hili genge limejimilikisha nchi kwa manufaa yao na vizazi vyao na hawako tayari kwa mabadiliko yoyote. Ukisikia kuwa ccm ina wenyewe basi wanamaanisha hao wenyewe ni usalama wa taifa.

Tukifuatilia mabadiliko katika nchi zingine za kijamaa mfano Romania, East Germany, Poland, Ukraine, Czech Republic, Slovakia nk walifanikiwa baada ya kuufumua na kuunda upya usalama wao wa taifa. Russia, Belarus, Serbia nk ambao hawakupangua usalama wao wa taifa bado wapo chini ya minyororo ya wakandamijazi. Mabadiliko ya kweli hapa kwetu pia ni lazima yaendane na marekebisho ya utendaji na ukubwa wa usalama wa taifa.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Kwa nionavyo mimi, ww ni mmoja Wao ila umekuja kujaribu kuona tunawaonaje coz JFK ni kioo sana Kifupi ni kuwa u r nothing good for citizen wa kawaida but a threat kama vile nyie ndio wa kwanza kuwapora haki zao ktk uchaguzi, kusaidia wezi wa raslimali zetu kama wale twiga, kusaidia wauzaji unga ambao wanatuua kwa madawa hayo huku mkitumia kodi zetu. Kinauma sana kwa usaliti wenu
 
Kwa kweli kuna idara za serikali ambazo zinahitaji reform, TISS, Polisi, na Takukuru. Atleast jeshi la ulinzi wanazingatia mipaka ya kazi yao, isipokuwa labda kwa viongozi wao wachache, idara nyingi zinahitaji overhaul!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Back
Top Bottom