Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Kuna shimo moja liko katika kijiji kimoja mkoani Lindi ambalo sio man made ila ni shimo ambalo hakuna mtu amewahi kuingia. Ni giza tupu, inasemekana ndilo Wajurumani walilitumia kuwatumbukiza watu waliokuwa wasumbufu kwenye utawala wao.
Ni shimo refu sana kiasi kwamba hata anayekutumbukiza hajui nini hatma yako huko ndani ila anajua tu kuwa ni mwisho wako wa kuonekana duniani.
Turudi kwenye mada,
Kuhonga maana yake ni kumpa pesa au vitu mtu wa jinsia nyingine ili akupende zaidi. Ingawa sasa hata watu wa jinsia moja huongana.
Kadri unavyohonga ndivyo unavyotupa pesa au mali shimoni. Usitarajie matokeo chanya. Never. Ukitaka kujua kuwa kuhonga ni sawa na kutupa kitu kwenye shimo refu wewe ishiwa.
Au mdanganye huyo unayemuhonga kuwa biashara yako imekufa hivyo akusapoti angalau laki moja au milioni moja au hata milioni 10 kulingana na jinsi ulivyojiweka. Subiri jibu.
Au mwambie umefukuzwa kazi au mkataba wako kazini umekwisha hivyo akupe angalau mtaji wa pesa kidogo. Subiri majibu.
Pesa mpe mtu ambaye rasmi mnakwenda kufunga ndoa, hiyo hatuiti kuhonga ni upendo na support.
Unailaani kazi yako kwa kuhonga.
Mungu anakupa fursa ya kukuingizia kipato wewe unatumia hicho kipato (fedha) kumshawishi mtu ili uzini naye.
Hakuna mwisho mwema wa mwongaji.