Kuhubiri dini kwenye mabasi na standi za umma nao ni uhuru wa kuabudu?

Kuhubiri dini kwenye mabasi na standi za umma nao ni uhuru wa kuabudu?

Ukahaba ulikuwepo toka Enzi za Ibrahimu na Yakobo. Hata Yesu alipokuwa kwa Jinsi ya mwili ukahaba na makahaba walikuwepo so auhusiani na Wahubiri. Tafuta sababu nyingine mkuu.
Uhuru wa kuwatoa watu kwenye imani zao halafu unawapeleka motoni,shauri yenu.Hata chanzo cha dhambi ni tamaa na uongo tangu mwanzo nyoka alienda kwa "Eva na kumwuliza Eti Mungu aliwakataza"
 
Wacha tuhubiri watu wamjue Mungu. Usidanganyike bro, amani ya nchi hii haitokani na kuwa na jeshi zuri juridical mataifa mengine yenye vita ila ni kutokana na hofu ya Mungu ambayo watu wanayo. Na hofu hii huja pale tunapowahubiria na kuwaombea Watanzania. Tuache tuhubiri kama ambavyo kuna Bongo flavor na Sinema kwenye mabasi.
amani ya nchi hii inatokana na wananchi kuwa mazuzu wala hakuna kingine
 
Naona unajitahidi kudhihirisha namna ukivyo na mapepo kwani mtu mwenye mapepo sifa yake moja ni kupinga vitu vinavyohusu Mungu. Nani kakulazinisha umpe sadaka? Mbona mnahonga wanawake, mnakunuwa pombe na kwenda kwenye uganga na huko kote mnatoa pesa. Acha hizobwana mdogo. Waache watu waseme Neno la Mungu. Wapo wanaofaidika na wao kunena mkuu. Sadaka ni msukumo wako na hakuna mtu anayekukaba au kukushikia dimbo umpe sadaka.
Makanisa yapo acheni upumbavu na utapeli.
 
Tabia hii inazidi kukua kila kukicha japo inaudhi. Hawa watu wanalipwa na nani na wanatoka wapi?

Lazima ifike mahali tukubaliane kwamba kila mtu ana imani yake kulingana na alivyolelewa na kwamba swala la imani ni binafsi na kuna maeneo mahususi ya kuabudu.

Makanisa ya kilokole kina Mwamposa na wenzake wanaoibuka kila siku kama uyoga. Hawa huwapata wale waliopoteza matumaini na dini zao za asili.

Hawa huamini kwamba wafuasi wao wanapatikana popote hata kwenye mabus na stand siijawahi kumuona padre wa RC wala askofu achilia mbali shemasi akihubiri barabarani. Nadiriki kusema na kuamini kwamba hawa wanaofanya mahubiri yao barabarani na kwenye mabasi ni walewale wenye asili ya kuhani musa na mzee wa upako.

Waislamu, hawa shughuli zao huishia misikitini na kwenye makusanyiko ya warming wao. Japo na wao wanatumia vipaza sauti ambazo mara nyingi huwa ni kero kwa wasiohusika lakini hutolewa kwenye maeneo maalum tu.

Wapagani na wasio na dini, hawa ni pamoja na wqnaoamini katika miungu ya kale (waliowengi hawajitanabahishi) lakini hukereka sana na wapo wengi.

Unakuta mtu mmepanda kwenye usafiri wa umma au mkiwa stand kila mtu akielekea kwenye mambo yake tena na mawazo tofauti mtu anawasha speaker yake ya mchina na kuanza kuhubiri dini? Aliyewambia mungu yupo kwenye daladala au standi ni nani?

Ni kweli kuna uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa sheria lakini kila uhuru unamipaka yake. Kwa kutambua hilo ndo maana serikali imetenga maeneo maalumu ya kufanyia ibada ambako warming hukutana huko na kumuomba huyo mungu.

Utaratibu wa kuhubiri kwenye mabasi ya umma na vituo vya mabasi ni utaratibu holela na unakiuka haki za watu wengine wasiopenda kusikia habari za Mungu kwa wakati huo.

Wale mnaowapa pesa watu hawa pia mngezielekeza pesa zenu kwa wahitaji moja kwa moja ili zimfikie huyo mungu na mupate baraka muwe na mafanikio zaidi hata kama wengi wenu ni wezi wa mali za umma, waongo, wazinzi, waasherati na wasengenyaji (baada ya kutoka kwenye nyumba za ibada).

Uhuru wako uishie mwisho wa pua yako, vinginevyo ni vurugu!

Nawasilisha.
Upuuzi..... Neno litahubiriwa popote,kuamini ni maamuzi yako. Katika kundi la watu 100 akiamkni hata mmoja tu ni ushindi mbinguni. Ukiona unakereka kusikia neno la Mungu basi ujue shetani kakukamata.
 
Upagani nao ni sifa mkuu. Sio Kila mtu anaamini kwenye hizo dini zenu. Si sahihi mtu kuanza kutoa mahubiri kwenye sehemu za umma bila ridhaa yao. Kama ww unaamini katika dini yako, andaaa sehemu maalumu, wanaoamini unachoamini watakuja kujiunga na ww, na sio kwenye basi unatemea watu mate na dini yako ya mchongo.
Tindo,"aka "Kinoa Miguu
 
Sasa wimbo kama wameloa sijui kamatia chini, mara weka nikukaze au linanipwelepweta mara una roba hizo zinafundisha nini? Inaonekana mzee una Mapepo dhahiri kabisa. Sema upo wapi tukuwekee mkono yatole hayo.
Mbona album za nyimbo za dini zipo nyingi tu akina Rose Mhando,akina Bukuku,AICT,Moravian,RC,KKKT,Anglikan kwa nini msiwaambie maderva wawekee badala ya kusumbua watu.
 
Kelele tu
Sijui kwanini wanaruhusiwa.
Wafate taratibu wafungue makanisa waeneze injili zao kwa amani sio mabarabarani.

Na maduka kufunga maspika kelele
NEMC sijui wapo wapi.
Ila wasanii kuimba Barabarani ni sawa. Bara kuwa Barabarani hazina kelele. Kuwepo na machangudoa yanayojiuza Barabarani ni swafiiiii? Vipazasauti vya nisikitini navyo swafiiii ila mtu akihubiri ndio vita. Aiseeeeeeee
 
Mimi nikiwaita matapeli watu wanakuja kusema kuwa usidharau dini za watu huu ujinga umepitliza.Makanisa yapo kila siku hao wahubiri feki wako kama waganga wa kienyeji tena afadhari hata waganga wa kienyeji kuliko hao matapeli.Mtu unasafiri mara linakuja lijitu kukuvurugia mipango yako.Huu utapeli mimi siupendi hata kidogo.
upo sahihi kabisa mkuu, yaani inakera sana unanihubiria habari za mungu wakati nawaza kuchelewa sehemu muhimu? waende makanisani huko wanaotaka wataenda huko siyo kutupigia kelele ili mpate chochote asante kwa konda na dereva wa gari ya posta makumbusho iliyoandikwa {mahubiri na biashara haviruhusiwi humu}
 
Back
Top Bottom