Una hoja, Ila binafsi sioni Tatizo la kuhubiri habari za Mungu mitaani.
Mimi ni muislam, Ila kamwe sijawahi kuchukizwa na mahubiri ya wanaomtangaza Mungu.
Hakuna dini inayohamasisha matendo mabaya. Dini zote zinatuhimiza kutenda wema na kuacha mabaya.
Kwa jamii yetu ilipofikia, watu wengi ni wakatili ni vyema neno la Mungu likasambazwa bila kujali kukereka Kwa watu wachache.
Neno la Mungu ni tiba, Kwa mioyo yenye visasi, mioyo yenye husda, mioyo yenye kukata tamaa, mioyo yenye choyo,roho mbaya na mauaji.
Mtu yeyote mwenye hofu ya Mungu ni mtu mwema kuishi nae.