Kuhubiri dini kwenye mabasi na standi za umma nao ni uhuru wa kuabudu?

Upuuzi..... Neno litahubiriwa popote,kuamini ni maamuzi yako. Katika kundi la watu 100 akiamkni hata mmoja tu ni ushindi mbinguni. Ukiona unakereka kusikia neno la Mungu basi ujue shetani kakukamata.
kwahiyo neno la kwenye bibilia linaweza kwenda kuhubiriwa msikitini?
 
Nimekuambia maandishi yanaeleza wewe ni mtu wa namna gani? Unajitahidi kuruka ruka tu toka mwanzo lakini katika yote upendo wa Mungu bado wakuvuta kaka.
Wewe hunifikii kwa lolote hata Yesu alipokuwa anamjaribu Yesu alitumia vifungu tena vya kweli lakini alishindwa.Ukiwa mpumbavu unajibiwa kufuatana na ulivyo soma Mathayo sura ya 23 yote uone jinsi Yesu Kristo alivyowapa makavu Mafarisayo.
 
Kama sijakosea walikatazaga kwenye mabus ila kwa stendi mkuu unaweza kujiepusha kuyasikia kwa kupita njia nyingine vitu vingine tusicomplicate maisha.
 
Anayekereka wakati Injili ya Yesu Kristo inahubiriwa huyo anampinga Kristo hata kama anajiita Mkristo. Hao wanaohubiri huko stendi na barabarani wanawafuata wale ambao huwa hawaendi kanisani. Kondoo wanapopotea ni jukumu la mchungaji kuwafuata walipo ili awarejeshe zizini.
 
Kuna siku nillitaka kumuambia mmoja aache kelele na usumbufu nikishangaa dakika chache baadaye robo ya bus wakaanza kumpa sadaka!
Wanaendekezwa na wenye mahaba zaidi na dini zao.
 
Mpaka pale azana itakapokomaa bhasi na hilii la mahubirii lipo sawaa kabisaaa... mpaka pale mabar yataacha kupiga mziki kwa sauti bhasi maubiri na waubiri wapo sawa kabisa muubiriwa utachagua usikilize au uache
 
Ila wasanii kuimba Barabarani ni sawa. Bara kuwa Barabarani hazina kelele. Kuwepo na machangudoa yanayojiuza Barabarani ni swafiiiii? Vipazasauti vya nisikitini navyo swafiiii ila mtu akihubiri ndio vita. Aiseeeeeeee
Machangudoa kila siku wanakamatwa na shughuli zao ni za kificho, tambua hilo.

Ustaaarabu ni kila kitu kifanyike mahala stahiki,

Ndio maana kuna makanisa na misikiti.
 
Wewe hunifikii kwa lolote hata Yesu alipokuwa anamjaribu Yesu alitumia vifungu tena vya kweli lakini alishindwa.Ukiwa mpumbavu unajibiwa kufuatana na ulivyo soma Mathayo sura ya 23 yote uone jinsi Yesu Kristo alivyowapa makavu Mafarisayo.
Hahaaaaa, sikuwa nataka kucomment huu uzi na nilishakupuuzia ila ulipo sema.na kuandika Yesu alipokuwa anamjaribu Yesu ndio nikarudi. Nimekwambia, maandishi yananena mambo mengi sana. Maandishi yako yananena mengi kuhusu wewe. Fanya mambo mawili, moja Muamini Yesu Kristo leo kwani nafasi bado unayo au lah, achana na haya mambo kwani unajitia aibu dogo.
 
Mimi napinga sana mbona makanisa yapo yale yana kazi gani?Mbona hamwendi kwenye mabaa na guest kuhubiri ila masokoni na kwenye mabasi mnapenda sana.
 
Machangudoa kila siku wanakamatwa na shughuli zao ni za kificho, tambua hilo.

Ustaaarabu ni kila kitu kifanyike mahala stahiki,

Ndio maana kuna makanisa na misikiti.
Nawe machangu wanakamatwa wapi? Wacha zako wewe. Wacha watu wahubirie wenye dhambi pia jitahidini nyie vijana kuchukuliana na watu. Acheni ujuaji.
 
Wewe huna lolote ni tapeli tu kama waganga wa kienyeji wa siku hizi.
 
Kisiwepo chochote, kuwe kimya kabisa. Hakuna mahubiri, mawaidha, muziki au movies.
 
Wale ni matapeli tu
 
Wanaanza kuomba sadaka kwa kisingizio cha baraka.
Sasa kuomba ni kutapeli mzee? We dogo jitahidi kuficha uchi wa akili yako mbele za wenzio. Nimekwambia, Amini au achana na haya mambo kwani huna ujualo zaidi ya kujidharirisha kwa comments na maandishi yako.
 
Kulima kugumu, bora tupambane hivyo hivyo kwenye mabasi, muhimu tunapata sadaka
 
Sasa kuomba ni kutapeli mzee? We dogo jitahidi kuficha uchi wa akili yako mbele za wenzio. Nimekwambia, Amini au achana na haya mambo kwani huna ujualo zaidi ya kujidharirisha kwa comments na maandishi yako.
Usipuuze mawazo ya wenzio kisa hawakubaliani na wewe jambo lolote linapofanywa sehemu ambayo siyo mahala pake huo ni uchafu.
 
Una hoja, Ila binafsi sioni Tatizo la kuhubiri habari za Mungu mitaani.

Mimi ni muislam, Ila kamwe sijawahi kuchukizwa na mahubiri ya wanaomtangaza Mungu.

Hakuna dini inayohamasisha matendo mabaya. Dini zote zinatuhimiza kutenda wema na kuacha mabaya.

Kwa jamii yetu ilipofikia, watu wengi ni wakatili ni vyema neno la Mungu likasambazwa bila kujali kukereka Kwa watu wachache.
Neno la Mungu ni tiba, Kwa mioyo yenye visasi, mioyo yenye husda, mioyo yenye kukata tamaa, mioyo yenye choyo,roho mbaya na mauaji.
Mtu yeyote mwenye hofu ya Mungu ni mtu mwema kuishi nae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…