Kuhusu dai la Katiba Mpya, Rais Samia shituka

Hata kama akili ni nywele ila zako ni kipilipili, kwanza katiba sio hitaji la wanasiasa bali kupitia wao ndipo itapatikana katiba ambayo itakua ni dira ya mustakabali wa taifa nan kasema rais aache shughuli nyingine then a stick na katiba mpya? Hilo ni moja wapo la kazi zake. Au unataka hitaji la katiba mpya apelekewe harmorapa?
 
Hela za ndege cash na
Hela za Katiba yako navizazi vijavyo lipi bora
 
Chadema warudishe kwanza hela walizokula kwenye bunge la katiba alafu mwishoni wakatoka nje
 
Ndio tunamuonya samia aachane na hao nyani. Akicheza nao atakula mabua. Wao wanachotaka ni kufanya siasa za kizandiki wakati ccm ina kazi ya kujenga nchi. Tafadhali mama samia usikutane na hao jamaa kwani nia yao ni kuleta madai yasiyokua na tija
 
Mtu akiwa madarakani hawezi ona umuhimu wa katiba mpya ni hadi atakapokuwa nje ya madaraka
 
Chadema warudishe kwanza hela walizokula kwenye bunge la katiba alafu mwishoni wakatoka nje
Lete evidence chaap tung'amue hiyo pesa ya bunge la katiba CDM waliilaje? Kwa kuiba au walijilipilipa wao tu
 
Sijui kama mleta mada unajua kuwa kwa Katiba tuliyo nayo Rais anaweza kuahirisha hiyo miradi ya SGR, JNHPP na kuuza ndege na kuanzisha ajenda yake nyingine bila tabu kabisa?

Tena si ajabu nyinyi wenyewe mkaishia kumshangilia kwa “ujasiri na uthubutu wa kipekee alio nao”!

Na msisahau kuwa hakuna gerentii kuwa Rais siku zote ataendelea kuwa yule mnayemfahamu. Mjifunze; msisahau somo la mwendazake.
 
Wacha uongo, kwani mama ni mkandarasi au engineer kavaa overall yuko site? Hata mama anafahamu umuhimu Wa kuikamilisha katiba, hata Zanzibar baadhi ya malalamiko yao yamo kwenye katiba. Katiba mpya ndo italinda taifa dhidi ya marais wakurupukaji kama watatokea huko mbele. Unadhani kama katiba ingeruhusu kutoa maoni kwa rais serikali ingehamia Dodoma ghafla vile?
 
Sioni ubaya maana katiba ni ya watanzania wote. Anayedai anadai kwa ajili ya watanzania wote na vyama vyote
Kudai katiba mpya ni jambo zuri, lakini Mbowe hawezi kulazimisha au kumshinikiza SSH kuhusu hil;i. Kama anataka katiba mpya atumie hoja lakini akumbuke katiba mpya ni gharama. Pia hawezi akamshinikiza rais eti fanya hili kama sivyo mimi nitafanya hili. Kwani yeye nani kwenye nchi. Hiyo nguvu Mbowe kaitowa wapi huyo mlevi, au anamuonea SSH kwa sababu ni mwanamke. Mbona huo ubabe hakuwa nao kwa Mkapa, Kikwete, na Magufuli. Kwani akikiondoa chama chake kwenye uchaguzi nani anajali.. Kwani hakuna vyama vingine cvya uchaguzi? Kwanza sasa hivi CGHADEMA haina nguvu yoyote. Inakaribia kujifia mbali! Chama chenye mbunge mmoja wa kuchaguliwa nacho kina nguvu ya kushinikiza lolote!
 
CCM bana, mmeanza kumtisha SSH kuhusu katiba mnafIkiri yeye ni kama JK.

Mmesahau kwamba yeye ndiye alikuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba.

Katiba kwa sasa ni takwa la nchi wala si hisani ya CCM
 
Kifo hajali ubondia wako,
Kifo hajali umwamba wako,
Mbele ya kifo hautambi,
Kifoo...kifooo..kifo ni kiboko
yao......nti..nti..nti..nti..nti
Kifo..kifooo...kifo hakina
huruma.
 
Unajua mchakato wa kupata katiba bajeti yake ni shs ngapi?
Pesa yote inayopatikana inaelekezwa kwenye miradi yenye tija, siyo vikao ili wake na Mbowe wapate sitting allowance.
 
Mbowe, Lema, Msigwa wamekuwa wabunge kwa miaka mingi mfululizo kwa tume ipi?
Ubunge/ushindi wao umekuwa ukitangazwa kwa mapambano kweli tena kwa vile hao ni viongozi wakubwa na machachari wa upinzani. Oktoba 2020 ndio mwendazake akaamua kuvuruga kabisa hata kura zao zisijulikane. Tume inaamrishwa na Rais? Ujinga uliokithiri! Nchi haiwezi kuendelea na ujinga wa kiwango hicho.
 
Wanataka katiba mpya si kwa lengo la kuwasaidia watz hapana!

Ila wanafikiri wakipata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi wataenda ikulu kiulaini.

Yani kwa mawazo yao wanafikiri kushindwa kwao ni sababu ya katiba mpya.
Kikwete alipoanzisha mchakato wa katiba mpya alitaka aende Ikulu?
 
Kama wewe umeweza kusema hivi na ni maoni yako, kwa nini wengine walivyosema hivyo unaona ni vibaya? Labda useme hata haya maoni yako ni ya kuangalia, au siyo? Kwa upande wangu, kila Mtanzania ana uhuru wa kutoa maoni yake hadharani isipokuwa tu asivunje sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…