Kuhusu Godbless: Napingana na wengi, siungi mkono mashambulizi dhidi yake

Kuhusu Godbless: Napingana na wengi, siungi mkono mashambulizi dhidi yake

T
Inawezekana kuna makosa katika kauli zake, hakuna asiyekosea, lakini wanaompinga wameenda mbali zaidi kuliko uhalisia

Lema kuwa karibu na labda kuwa kabila moja na Freeman Mbowe au labda wote kutoka kijiji kimoja isiwe sababu ya kushambuliwa kwake, tuko wengi tuliokuwa karibu na Mbowe nikiwemo mimi na wengine wengi mpaka Tundu Lissu, sasa kwa jambo hilo sidhani kama tunazuiliwa kutoa maoni

Wakosoaji wa Lema ni kama walisubiri akosee ili wamshambulie, kwamba walikuwa na madukuduku yao wakisubiri upenyo, hizo ni siasa za kishamba ambazo hazikubaliki, si kila mchaga lazima apigwe vita, siasa za ukabila ndani ya chadema hazikubaliki.

Kingine ni hiki, Lema hana uwezo wa kushawishi jambo kubwa ndani ya chama hata kama ni mjumbe wa kamati kuu, kwahiyo wenye mashaka naye ondoeni, hii kwa sababu hakuna lolote litafanyika kwa ushawishi wake.

Ifahamike kwamba mimi ni miongoni mwa wale wasiotaka maridhiano na Shetani, hilo kila mmoja wenu analifahamu, sasa kwa andiko hili isitafsiriwe kwamba naunga mkono jambo hilo

Niko Tayari kusahihishwa.

WABHILLAH TAWFIQ
Tatizo kuna watu wako CHADEMA lkn bado wanapambana na Mbowe na kila wanayedhani anaelewana na Mbowe
 
Tattizo kubwa hiii vita inapigwa kiukabila na siyo kujua hali halisi ya tatizo ila imegemea kwenye kupiga vita lile kabila. na inapata nguvu haswaa kwa nature ya ilo kabila kuwa na umakini kwenye maswala ya pesa ukilinganisha na shutma anazotupiwa sijui ni kweli au lah muda utaongea
 
Lema si mweka hazina wa Chadema
 
Viongozi CDM mngepunguza kuongea na vyombo vya habari(naamini wewe ni kiongozi wa CDM), kama kuna tofauti za kimtazamo na kutuhumiana kwa hapa na pale, malizeni huko ndani, then atoke kiongozi mmoja ajulishe jamii.. kama mlivyofanya kwenye tuhuma za tonetone kwa bwana Heche..nje ya hapo mnaharibu na kujitoa kwenye FOCUS..asante
 
Mimi siyo kiongozi wa Chadema
 
Watu wanashindwa kutofautisha siasa na maisha binafsi ya mtu

Salam za rambirambi hata zingetolewa na chama cha chadema kwenda kwa Samia (as a person not president) bado isingekuwa shida coz nje ya siasa Samia ni mtu kama watu wengine, ana ndugu rafiki na jamaa wa dini tofauti na vyama tofauti
 
Viongozi CDM mngepunguza kuongea na vyombo vya habari(naamini wewe ni kiongozi wa CDM), kama kuna tofauti za kimtazamo na kutuhumiana kwa hapa na pale, malizeni huko ndani, then atoke kiongozi mmoja ajulishe jamii.. kama mlivyofanya kwenye tuhuma za tonetone kwa bwana Heche..nje ya hapo mnaharibu na kujitoa kwenye FOCUS..asante
Huu ushauri ni mzuri sana wangeufuata
 
Wewe pia ni msaliti inabidi ufutwe uanachama CHADEMA. Wewe na Lema ni mapandikizi ya Mbowe. Mnamhujumu Heche na Lissu.
Kama unachosema ni sahihi ni kivipi Lema akawa wakala wa kuhesabu kura za Lisu na Lisu akashinda?

Angekuwa ni mtu wa Mbowe angeshindwa kupunguza kura na kumpa Boni Yai wakala wa Mbowe?

Kuna kizazi kimevamia kwa pupa mambo wasiyoyajuwa, ukiwaona Facebook wanavyorusha matusi ukiview profile zao kumbe ni vitoto vya juzi tu havijui lolote.

Nadhani hamjui Chadema kama chama kinahitaji pesa za serikali kwa jina la ruzuku, sasa mnaodhani ni dhambi kuwa na mawasiliano na watu wa serikalini mnajizima data.

Mnajuwa sababu za aliyekuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Imran Kombe kuuwawa?
 
Mara zote naunga mkono Chadema
Ni kweli mkuu nakujua kwa kuunga mkono CDM hata katika kipindi cha Magu alipodidimiza demokrasia, lakini kwa hili la Lema mkuu nakuomba uwe mpole tu maana huyo Lema angekua anahitaji ku solve mambo kwa busara asingeandika mambo ya chama mtandaoni hususani lile swala la Passport ya Heche.

Lile ni shambulio la wazi wazi
 
Back
Top Bottom